Upotoshaji uendanao na tochi za usalama barabarani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Pana upotoshaji mkubwa kuhusiana na hizi tochi za usalama barabarani ikipelekea kuwakandamiza madereva pasipo uhalali wowote.

Si kweli kuwa camera hizi ziko fool proof na eti kuwa kila zinazochosoma ndiyo hivyo hivyo.

Namna gani mpigaji alikuwa steady, hali ya hewa wakati huo, visibility, state of calibration, na hata uwepo wa magari mengine ni factors ambazo zina count mno.

Camera hizi hupaswa kuwa calibrated na certified agencies angalau mara moja kwa mwaka. Hizi zetu anayejua ni Sub hana u Wataala pekee.

Angalia hapa:

The truth about speed cameras

Hivi serikali haiwezi kushirikisha wadau kuona inawatendea haki wananchi wake?

Ni taste mbaya sana wananchi wanapohisi kuibiwa hata kama mapato ya jinsi hii yanaelekezwa kwenye SGR.
 
Wewe fuata vibao vya speed sio kuanza kulia tuuu
Ila kwa utaratibu huu kweli sio adabu
images.jpg
 
Pangekuwa na nia njema, polisi hawakupaswa kujificha, na sheria za barabarani zingekuwa uniform kwa watu wote. Zisingetambua STL wala PT.

Vile vile kwa hoja zao zisizokuwa na mashiko, na huko bank si wajifiche ili majambazi wadhanie hawapo ili wawakamate?

Palipo na nia njema twaona matangazo hata ya kuwapo mbwa wakali, kuwapo mitambo maalumu ya kuzuia wezi, kutegwa umeme nk.
 
Kiuhalisia ni wizi unaofanywa na serikali dhidi ya wananchi wake.

Nimewahi kufanya cross checking mara 4 kati ya speed ya gari, gps niliyokuwa nayo ndani ya gari na torch ya traffic police; torch ilisoma 8km/hr zaidi ya uhalisia. Traffic wanapokuwa na torch ya namna hiyo wanafurahia sana maana wanamkamata karibu kila dereva anayepita.
 
Kweli kabisa mkuu. Na ndio maana kwa wenzetu speed 70miles/hr highway lakini kama unatembea chini ya 80miles/hr traffic hakugusi sababu wanajua sometimes tochi haisemi ukweli.
 
Kweli mkuu! Kwa uzoefu wangu kidogo ukizidisha hata 5 to 15 miles sio mbaya ila bongo ukizidisha hata speed 1 tu wamekudaka
 
Pangekuwa na nia njema, polisi hawakupaswa kujificha, na sheria za barabarani zingekuwa uniform kwa watu wote. Zisingetambua STL wala PT.

Vile vile kwa hoja zao zisizokuwa na mashiko, na huko bank si wajifiche ili majambazi wadhanie hawapo ili wawakamate?

Palipo na nia njema twaona matangazo hata ya kuwapo mbwa wakali, kuwapo mitambo maalumu ya kuzuia wezi, kutegwa umeme nk.
BONGE LA POINT MKUU [emoji106][emoji106][emoji106]
 
Back
Top Bottom