Upotoshaji kuhusu mizimu


Asante kwa kuelewa
 

Hizi dini ni uongo na ukiwa unaomba baraka haziji kwako zinaenda kwao wenye mungu wao ndo mana watu weusi tuna makanisa na misikiti mingi maendeleo hakuna.
 
Huu ndio ukweli unaotusumbua watu weusi, Wazungu wana dini yao, Waarabu wana dini yao, Wahindi wana dini yao, Wachina wana dini yao, na wanaziishi dini zao, ila cc waafrika tulizikataa dini zetu.

Upo sahihi ila kinacho waumiza watu weusi ni kwamba hawataki kukataa uongo na kukubali ukweli kuwa hizi dini hatukuzitaka kwa hiari bali tulilazimishwa kwa nguvu kuzikubali.
 
Africans ni viumbe pekee dunian tunaotapatapa kwenye kila sekta, hii yote inasababishwa na kuikana asili yetu yani saiv hakuna utumwa wa nguvu tupo kwenye utumwa wa kifkra; leo hii africans tunakana majina yetu kwa kisingizio Cha din(ubatizo), tunakana lugha zetu kwa kisingizio Cha kuelimika, tunakana teknolojia zetu kwa kisingizio Cha kuitwa uchawi, mifano ni mingi....ila yote kwa yote africans Kama tunataka maendeleo ni lazma tuwe huru kifkra, kuanzia dini mpk teknolojia. Ukiangalia madhara ya kuiga iga tamaduni za watu ni umaskini tulionao. Leo hii ukimwangalia mzungu utaona anaishi lifestyle tofaut kabsa na ya mchina, mhindi n.k....lakn ukija africa watu tumegawanywa kuna waliomfata mzungu,mwarabu n.k...
Africans lazma tujitambue kwa kusoma history tujue hizi din na vitu tunavyoviona vipo kwa sababu gani?
 
uzi wako ni mzuri bt bado unahitajika kujifunza zaidi kuhusu haya mambo, mizimu hiyo hiyo inatumiwa na wachawi katika kufanikisha mission zao za kuuwa/kuwatupia uchawi watu.

nikiwa shule nimewahi pitia matatizo ya kuumwa kichwa na kutoona vizuri nikatumia dawa wapi... nikaambiwa kwa sababu natumia jina la babu basi mizimu wananitaka ninunue mazaga yao nikafanya hivo bt matatizo ndo yakazidi, nikafanyiwa hadi matambiko lakini wapi, kilichofuata nikachoma kila kitu na kutoamini tena upuuzi huo ndipo hali ikawa sawa nikaendelea na shule, mambo ya mizimu ni mambo ya kipumbavu sana.

kitu pekee ulichopatia katika uzi wako ni "mungu halisi hatoi adhabu wala hahitaji kunyenyekewa"
 
Hizi dini ni uongo na ukiwa unaomba baraka haziji kwako zinaenda kwao wenye mungu wao ndo mana watu weusi tuna makanisa na misikiti mingi maendeleo hakuna.
Ni kwa sababu maendeleo hayatokani na sala Bali kufanya kazi kwa bidii na kuyatawala vyema mazingira yako.
 
MUNGU AKUPE REHEMA YA KUJUA KWELI, By the way hata yao wazungu nao hufa..so nao pia wanakuwa mizimu sio!? So nao wanawaabudu Kama unavyotuambia hapa kuhusu africans tuitunze mizimu!?

Mzee..kilichokufa kimekufa..ni sawa na mwembe uliokauka..usitarajie mwembe yataota juu yake.
 
Mizimu ni MAJINNI yaliokaa sehemu sehemu tangu enzi za mwanzo wa dunia
Na kufahamu mila tamaduni za eneo husika na kuzirithisha kutoka kizazi hadi kizazi nawe ukiwafatilia basi utawarithisha
Watoto wako

MTOTO
"mama jana nimelala nimeota mtu mweusi ana madevu na shuka jeupe kashika kirungu akakaa pembezoni mwa kitanda akawa ananiongelesha mimi sikumuelewa"
MAMA
"Huo ni mzimu wa babu yako kesho twende kwenye MZIMU kule kweye mbuyu tukatambike
Inabiki apatikane kuku mweusi na mtama robo mchele robo uwele robo
Na kaniki 1"

Kesho hao wanachukuzana kupanda milima na mabonde wanajichosha kutembea kufata mzimu msituni huko

Kumbe yule alomtokea ni JINNI alojivika sura ya marehemu babu yake
Nia na dhumuni kuwahadaa tu wanadamu walokosa mahalifa sahihi
 

Hiyo ni hatua ya kwanza ya kufahamu mambo
 
Mbona Wazungu nao walipelekewa Injili kama sisi lakini wameendelea.Maana ukweli ni kwamba nao walikuwa na dini zao,walipelekewa Injili wakaachana na dini zao za asili,...tusihalalishe kutokuendea kwetu kwa sababu nyepesi.
 
Hizi dini ni uongo na ukiwa unaomba baraka haziji kwako zinaenda kwao wenye mungu wao ndo mana watu weusi tuna makanisa na misikiti mingi maendeleo hakuna.
Una akili sana wewe, Mungu akubariki daima👏
 
Mbona Wazungu nao walipelekewa Injili kama sisi lakini wameendelea.Maana ukweli ni kwamba nao walikuwa na dini zao,walipelekewa Injili wakaachana na dini zao za asili,...tusihalalishe kutokuendea kwetu kwa sababu nyepesi.

Wazungu hawakupelekewa injili yoyote wazungu ndo Roman Empire wao ndio waanzilishi wa hiyo injili Soma mqmbo ya First Council of Nicaea. Mkutano Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Hapo ndu ukristo ulipoanzishwa
 
Okay...hivo ndo umeelewa ww,lkn ukisoma Kitabu cha Matendo ya Watume utaelewa jinsi Injili ilivoenezwa kutoka Uyahudi kwenda Asia,Ulaya na maeneo mengine.Hao Rumi hawakuwa Wakristo hapo kwanza,walikuwa na miungu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…