Hata sikumbuki....ila misamaha leo imeisha!!
Natumaini kwa Asha utapata nafasi ya kuweka vibegi vyako!!:A S cry:!😛hone:
Basi nimetubu mamii, usiende kwa kolokuwini
Kosa gani mimi nililokukosea wanitupa
Mrembo mwenye hadhi, pokea tena waraka
Usome na kuhifadhi, Yote nilioyoyandika
Nilipi lililokuudhi, Hebu niambie haraka
Fanya haraka muhibu, unipe hili hakika
Uneleze taratibu, Nipate kutoa shaka
Ni ipi hiyo sababu, Ilokupa kunepuka
Muhibu Lizzy nasema nawe, Hebu mwepushe shetani
Nyonda sinizuzuwe, Kanitia fedhehani
Toka kuniepuka wewe, Nimengia matesoni
Usione ni mzaha, mwenzio ni maradhini
Umenitia jeraha, La huba ndani kwa ndani
Naishi sina furaha, Kwa yondi lako Fulani
Kukurai si aibu, maadamu nakutaka
Na lau kama muhibu, Liko kosa limetuka
Basi mwana nimetubu, Msamaha nautaka
Kaditama tafadhali, wata kunihangiasha
Mwenzio kucha silali, Kwa huba huwa nakesha
Kumbuka na jambo hili, Kwako mahaba sijesha