boniuso
JF-Expert Member
- Mar 13, 2013
- 944
- 1,335
UKIFAHAMU KUWA BINADAMU TUPO TOFAUTI MAISHA YAKO YATAKUWA TOFAUTI
Katika ulimwengu tunaoishi watu wengi hawajui kuwa tupo tofauti sana hata kama tunaonekana tunafanana.
Kwa hali hii baadhi ya watu huonekana hawaeleweki katika jamii kwa kuwa tofauti kitabia na mienendo yao.
Haramu itabaki haramu hata kama kila mtu anafanya na halali itakuwa halali hata kama hakuna anaefanya.
Watu tumetofautiana sana kwanzia kwenye ubongo tupo tofauti na muonekano wa maumbile na tabia
Utumwa mkubwa ni hali ya mtu kushindwa kujua aishi vipi .
Wanaume wamegawanyika katika makundi matatu
Kundi la kwanza ni
1. ALPHA MALE
Hawa ni wanaume ambao hufanikiwa sana kuwa viongozi,hupenda maisha ya juu sana, hujiamini sana hasa wanapokuwa na vyeo,kipato,cheo au umaarufu na huwa wajeuri sana na wenye viburi.
Alpha male huanzisha fashion,sheria, kuanzisha biashara,hufanya vizuri sana wanaposifiwa sana,hupenda kuwa na marafiki wengi sana. Huathiriwa sana na fashion,taarifa mpya za kila wakati,hupenda kuishi kama watu wengi wanavyoishi
Ukiwasifia huzidisha mbwembwe,huwa wanataka kukubalika sana na kila mtu,huwa wana nguvu kubwa sana ya ushawishi,wanawake huwapenda sana kwa sababu huwa watu wa fashion na wanaokwenda na wakati.
Hupenda vitu vipya,pesa nyingi,vyeo, umaarufu,kuwa juu kwa watu wengine,huwa,huwa wanapenda sana mikusanyiko, sherehe, matukio ya kuonekana sana mbele za watu.
2. BETA MALE
Hawa ni wanaume wapole,wakimya,mabwana ndio yaani wafuata bendera, chochote Alpha watasema wao hufuata,huwa wakimya sana na wasiotaka kuwa juu,hawa kuwatalawala ni rahisi kwa sababu huwa wanakubali chochote kinachokuja,
Hawana uwezo wa kujitegemea kimawazo badala yake fashion yoyote ikija wao hufuata mkumbo,huwa wanajipendekeza kwa viongozi,hutaka kuonekana waungwana na kuepuka kutoa au kufanya tofauti na matarajio ya viongozi.
Wanaume wengi ni Alpha huku beta idadi ikifuatia.
Alpha huwa wanakuwa na wanawake wengi yaani (play boy) kwa sababu furaha yao ni vile kukubalika sana katika jamii,
3. SIGMA MALE
Hawa ni wanaume wachache sana duniani mwenye kwenda tofauti na matarajio ya watu wengi.
Kwanza huwa wanakaa kimya sana kama umekutana nae mara ya kwanza haonekani kukuchangamsha mpaka akuzoee kidogo
Wanapenda upweke lakini wanajali sana watu hivyo hajaishi atakuwa na rafiki au hana anabaki na furaha,
Wanakuwa na akili sana kwa kutafakari kupita kiasi,huwa hawana muda wa kujadili umbea,hawana habari za kufuata fashion,
Huwa wanajirekebisha tabia wao wenyewe bila kuambiwa,hujikosoa sana wa na kujirekebisha,huwa wanajali watu wote kwa kiwango sawa
Hawana unafiki wa kuwatendea watu wengine tofauti au kumpendelea huyo na kumnyanyasa mwengine,hupenda haki,
Hawafuati mkumbo,hawavai nguo zinazo valiwa na watu wengi,hawapendi kukaripiwa,hawapendi kufuata taratibu za watu wengi kwa sababu huwa wanafikiria tofauti sana na wengine
Wepesi kubadilisha matatizo kuwa fursa,huwa hawataki sifa ,anakuwa kiongozi lakini hana muda wa kumnyanyasa mtu yeyote,
Tabia zao huwa za kipekee sana,hawana marafiki wengi kwa hawana muda wa kujadili umbea
Huwa wabunifu sana,wenye upendo wa dhati,wacheshi sana,hupendwa sana kama mwanamke anataka mtu wa kudumu nae,
Wenye huruma sana na ukiwapenda sawa au usipowapenda sawa,hawana muda wa kulalamika
Huwa hawahitaji kupewa motivation ili wajitume,hata kama jamii nzima tabia ni mbaya wao hawafuati tabia za watu wengi
Huwa wanatazama maisha kwa jicho tofauti,huridhika na vitu vichache,hupenda ubinadamu kuliko mali,cheo, umaarufu
Hawawezi kukaa na watu wenye mtazamo hasi,ukijaribu kuwalazimisha wabadilike tabia wanavunja urafiki na wewe
Huwa wanaishi uhalisia wao hivyo unaweza kuwachukia kwa sababu watu wengi huishi maisha fake
Huwa wapo huru kifikra na maadili,hujiongoza wao wenyewe,wazuri sana kubadilika kuendana na mabadiliko
Wanajipenda sana vile walivyo na hupenda watu wengine wajipende kwa uhalisia wao.
Hupenda kujiajiri,hutafuta maarifa mapya kila wakati,huwa na mtazamo tofauti na ule wa watu wengi,
Wasiri kupita kiasi, hawezi kueleza habari za mahusiano yake kwa watu wengine,huwa waaminifu sana ila hawaamini watu wengine kiurahisi
Wanaweza kuona vitu watu wengi hawaoni,ukiwa nae kama rafiki huwa wanyenyekevu sana na huwezi kuchoka kuwa nao kama utawaacha kuwa vile walivyo
Hawapendi kumtawala mtu.
Ni vigumu sana kuwaelewa kwa kuwa wanabadilisha tabia kuendana na hali ila wao wanakuelewa sana
Ukitambua upo kundi gani utakuwa sehemu kubwa sana ya mafanikio.
Ukitaka kuwa mwenye furaha usiishi kwaa kufuata mkumbo,
Watu wengi hawafanikiwi sana kwenye maisha hivyo ukitaka kuwa kama watu wengi maana yake unaishi maisha ya kawaida
Watu wengi hawajipendi vile walivyo hivyo ukiishi kama watu wengi utaishia kutamani uwe na sura tofauti,rangi tofauti,uzaliwe sehemu tofauti kwa ujumla watu wengi hawajui wanataka nini.
Mtu ambaye hajipendi vile alivyo hakuna anachoweza kupata akakipenda sana bali ataona kuwa kuna mwengine amepata kikubwa
Kwa sababu wanaume wengi ni Alpha inakuwa tatizo kwao wenyewe kufurahia maisha yao kwa sababu wanataka kuwa juu kwa kushindana na kila mtu kwa kila kitu
Sura, rangi, maumbile, kabila, wazazi,mahali ulipozaliwa sio vitu ulivyoandika barua uwe hivyo ulivyo
Kukasirika kwa sababu ya sura,rangi, muonekano, historia yako,asili yako,matendo yako ya zamani ni kujiadhibu bure.
Kubali kuwa maisha ya zamani yameshapita hivyo kujuta kwa makosa ya zamani, kujilaumu kwa sababu watu wengi hawakupenda tabia zako za kipekee ni adhabu
Ishi uhalisia wako utakuwa mwenye furaha sana.Jipende vile ulivyo kutamani uwe mrefu au mfupi au uwe na historia tofauti ni kupoteza muda
Kubali kuwa haya ni maisha sio movies ni kawaida maisha kuja tofauti na mipango yako wewe
Kinachotokea sio tatizo bali kile unakwenda kufanya ndio kinaweza kuwa suluhu au tatizo
Kinachotokea ni 10% huku 90% ya matokeo ni maamuzi unakwenda kufanya kwa kilichotokea
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam