Hoja zako zina matatizo yafuatayo.
1. Unasema we have equal chances to make changes. We don't. Mtoto aliyezaliwa kwenye familia tajiri mwenye support network nzuri ana chance kubwa ya kufanya mabadiliko anayoyataka kwenye maisha yake kuliko mtoto aliyezaliwa katika familia masikini asiye na connections. Ndiyo maana hapo juu niliongelea suala la privilege na bias, inabidi uelewe somo la privilege na bias.
Watu wakishindwa kubadilisha maisha yao, kwa sababu nyingi tu zilizo ndani na nje ya uwezo wao, wewe unaona huo ni udhaifu wao, wameshindwa ku adapt na mazingira.
Kuna sababu nyingine ziko nje ya uwezo wa watu hawawezi kuzipangua hata wa adapt na mazingira vipi.
We have equal chance but we deserve different Mzee. Some people deserve something big and others deserve medium and other low. Coz kuna watu hata ukiwapa billions of money they will settle at 10k only
Kwahiyo usilazimishe kwamba wote tukitokea chini ndio wote tutakua matajiri, hicho kitu hakiwezekani bro.
Kuhusu privilege and bias always will favor those who deserve it.
Mfano wote tupewe 1 billions Tsh kama mitaji alafu awepo mbongo, mchina, Arabs and Indian nafikiri hata wewe unajua ni nani atakua wa mwisho hapo.
But we all have equal chances.
Mfano mwingine ni wachina wengine wanalima pilipili na wengine wapo huko vijijini kabisa wanatafuta dhahabu, Je! Nalo hili unataka tuseme aje??? Mchina kaona fursa anapita nayo mbongo anasubiri mpaka serikali ndio imwambie😳😳🤔
2. Unasema jambo jema ni kuli address tatizo si kulaumu. Hujui hata kama watu wanaelewa jinsi ya kuli address tatizo. Pengine kulaumu, ku vent, ku connect emotionally ndiyo stage ya kwanza na baada ya hapo ndipo watu wataanza kujiuliza, now what, what is our action plan? Pengine watu washapiga hesabu washaona hili tatizo kubwa sana hakiishi leo wala kesho, nhoja tu vent tu hapa. Na wewe unayepiga kelele za "solution, solution" bila hata yavju appreciate tatizo ndiyo usiyeelewa mambo hapa.
Naamini wewe umekwenda shule, Kuna hatua sita kama sio Saba za problem solving. Je! Hizo ulizozitaja hapo ni hatua Gani kati ya hizo sita au Saba???
Nitakusaidia kuzilist hapa
1.Identify / Recognize the Problem
Notice that something is wrong, incomplete, or needs improvement.
2.Define & Understand the Problem
Clarify exactly what the problem is, gather information, and determine its root causes and boundaries.
3.Generate Possible Solutions
Brainstorm a wide range of options without judging them yet (divergent thinking).
4.Evaluate & Select the Best Solution
Weigh the pros, cons, feasibility, risks, and resources of each option, then choose the most suitable one.
5.Implement / Execute the Solution
Put the chosen plan into action.
6.Review & Evaluate the Results
Check whether the solution worked, learn from what happened, and adjust if needed (this stage often loops back to earlier stages).
Ukielewa hapa bhasi utajua umeandika non-sense, kwasababu no matter tatizo ni kubwa kiasi Gani ni lazima tupate solution zake bhasi. Kwahiyo niko sahihi kuuliza solution kwasababu tatizo haliwezi kuachwa.
Pia ninapozungumzia kuliaddress tatizo nazungumzia hizo hatua hapo juu. Kijana unaonekana ulienda shule lakini hujui ulienda kufanya Nini.
3. Hoja yako ya kibinafsi ya kila mtu kujinunulia gari ili kupambana na jua la Dar inaonesha si tu ubinafsi wako, lakini pia contradiction. Unaongelea kuwa solution oriented, lakini hujafikiria kuwa kila ntu akinunua gari na mitaa kujaa magari kutakuwa na tatizo la foleni, carbon emissions, na joto litazidi.
Umeshindwa hata kufikiria mfano wa a good public transport system itakayokuwa environmentally friendly and sustainable. This is not being solution oriented, this is just selfish in a very myopic way. You are being selfish and saying "I don't want to hear complains of your hunger while I am having my good time and eating steak you peasants".
😂😂😂😂😂 I have to laugh.
Kwanza hakuna mtu ambaye sio mbinafsi, unless otherwise niambie wewe unaweza kufa kwa niaba ya nani? Au huwa unamgawia nani nusu ya kipato chako??
Pili nature is selective my friend, unapowaza kununua gari la AC Kuna wenzako watakua wameshayachoka pia wameshachoka kukaa kwenye magari ya chini, sahivi Kuna magari yanayopaa.
Alafu pia hicho unachokiwaza ni kwamba hakipo mambo yatajisettle yenyewe tuu. Kuna watu hawataona huo umuhimu.
Nikupe tuu mfano, wakati ninyi mnatamani maji ya kunywa ya baridi, mimi Huwa sinywi maji ya baridi na nimekutana na watu wengi tuu hapo dar hawanywi kabisa maji ya baridi.
Pia hizo AC mnazozitamani wengine ndio kabisa hatuzipendi na zinatupatia mpaka kikohozi.
Nataka kusema hivi,usilazimishe kwamba ukinunua gari na mwingine atanunua gari, what do I mean ni kwamba always try to solve your own prob, kwakuwa tatizo lako haliwezi kuwa tatizo langu pia.
Kuna shida Moja nimeiona kwa jamii kubwa na hata hapa pia nimeiona, watu wanaamini kwamba ukiwa na pesa unakua umesolve matatizo yote, kitu ambacho sio kweli.
4. Huyo Mzee mwenye mashamba ya mbao Njombe mimi ni baba yangu sasa, yeye ana mashamba huko huko Njombe, anatembelea gari kubwa hivyo hivyo, kama hilo, ingawa si model hiyo kwa hiyo najua si yeye exactly, anachanja mbao hivyo hivyo, anapangisha watu nyumba zake Oysterbay na Mbezi Beach na kulipwa US dollar nzuri tu, akichoka kukaa Tanzania anakuja Marekani muda anaotaka kutuona watoto na wajukuu wake kila mwaka. Mwaka jana kapewa offer na mtu anataka kununua nyumba yake moja, $3 million, USD, kakataa, hana shida.
Simuongelei huyo, but nashukuru kwamba umenielewa hapa. Huyu mzee ninaemsemea anakaa bush sana, yaan huwezi hata kumzania kwamba anapesa ndefu hivyo.
Lakini pia nilitoa mfano kuna madogo wa 20+ ages wameshika mitaji ya 60milions plus hapo njombe.
Lakini ana historia ndefu sana ya kusomeshwa na nchi, kuwa mentored na wenzake kazini, kupata advantage za network ya familia aliyoikuta, hata kutangulia kusoma wakati Tanzania wasomi ni wachache tu kwa kiasi kwamba kijana anaye graduate leo kama yeye alivyo graduate miaka hiyo, hana chances zilezile tena.
Na hapo ndipo hoja yako ya kwamba wote tuna nafasi sawa inaposhindwa. Huyu mzee ame graduate chuo kikuu nje in the early 70s huko, kafanya kazi miaka mingi, kanunua mashamba kemkem na kujenga nyumba miaka hiyo bei rahisi, kapanda ngazi siku hizo hakuna wasomi wengi, utasemaje kijana anayeanza maisha leo naye ana nafasi ya kufanikiwa hivyo hivyo wakati idadi ya watu kuongezeka kwenye competition tu inaondoa msingi wa hoja yako?
Mkuu utakubaliana namimi kwamba Kila zama zinakitabu chake, I can tell you wazee wetu walikua wanapewa mashamba Bure kabisa tena ni maekari kwa maekari.
Kwasasa mashamba yanauzwa bei za kawaida tuu, huko mikoani ukiwa na laki unapata ekari na kuna sehemu zingine ukiwa na laki Tano unakatiwa eneo kubwa tuu hata zaidi ya ekari kumi.
Sasa hiki ndicho namaanisha kwamba we have equal chances kwasababu wazee wetu walipewa ardhi lakini fedha kwao ilikua ni ngumu sana kuipata, sisi hatuna ardhi ya Bure lakini tunaweza kupata fedha kwaajili ya kununua ardhi Sasa je unataka Nini kifanyike ili mambo yabadilike???
We have equal chances to make it. Coz hata internet ilipokuja ilikua ni fursa kwa watu wachache tuu lakini sahivi ni fursa kwa watu wote. Mtu unaweza kufanya kazi remotely Yaani pasipo kuwepo ulaya na ukafanya kazi ulaya.
I have my own young bro, nilimshauri asiende chuo bali akomae kusoma mtandaoni DATA SCIENCE, sahivi dogo analipwa zaidi ya mili20 kwa mwezi alafu yupo hapa hapa bongo, hiyo fedha anayoingiza hata mimi amenizidi kwasababu yeye ni uhakika kuipata, Sasa how come useme hakuna equal chances???
Dunia imeshakua Kijiji, zama za Giza zilishapitwa na wakati, vijana tujitahidi kutafuta taarifa na maarifa alafu tuingie kwenye mashindano.
Achilia mbali huyo, hata mimi mtoto wake, nilivyoanza maisha tu nina advantage mshua msomi, ana kazi ya maana, mazingira ya nyumbani naona mazuri. Nilikuwa najivunia sana utashi wangu na utamaduni wa kusoma vitabu, nikisema watu wengine ni wazembe, hawasomi sana, na mimi nina jitihada binafsi sana za kusoma (currently reading Jared Diamond's new book "Profits, Prophets, Coaches and Kings: (When) Do Leaders Matter?"), until my friends exposed my privilege, kwamba pengine ndiyo kuna juhudi binafsi, lakini ulikulia Oysterbay, kwa mzazi msomi, ukapelekwa Tanganyika Library na kufundishwa umuhimu wa vitabu tangu mdogo, ukajua British Council na USIS. Mama yako alikuwa anazungumza Kifaransa nyumbani wakati Watanzania hata Kiingereza kiliwatatiza. Tena akifanya kazi Ikulu enzi za Nyerere anakutana na Nyerere na wapambe wake kila siku. Wakasema "Check your privilege".
Mkuu inawezekana wewe ulipata privilege kubwa sana na hata Leo unaprivilage kubwa sana lakini still i can take you down when we race.
It's not about who is who but it's who is sharp on making things happen.
Mkuu nakubali haya yote lakini we have equal chances ya kumake kwenye hili life.
Nani alimuamini Elon Musk? When Bill Gates is at the top??? Nani alimuamini Jack Ma when Amazon is at the top?
Hata hapa bongo Kuna magepu mengi tuu ya kupita nayo na kuwaovertake Hawa akina Mo dewji.
Sasa, na wewe unaposifia watu walioweza kufanikiwa, surely kuna element ya juhudi binafsi pengine imechangia, hatukatai. Lakini je, umeangalia privileges zao zote vizuri?
Kuna watu wanahizo privilege but are not making.
Kuna jamaa angu hapa bongo, baba yake anamashamba, majumba, magari na anamiliki private jet lakini kijana wake anawaza kufanya uchuuzi wa kununua suti huko Uturuki aje kuziuza Kariakoo😂😂😂
Kuna siku nikamwambia mwanangu wewe unachezea bahati, Mtumie Mzee wako akupe Hela ufungue viwanda au umiliki hata limgodi la dhahabu lakini jamaa anawaza kuwalala dada zetu tuu.
Rafikiake sana huyo dogo sahivi ndio amekua brand ambassador wa yule wa kampuni *** lakini naye huyo dogo kwao ni wameshika posho vibaya sana huyo dogo anabwia maunga pia wanasema ni gasho😔😔😔💔
Sasa hapa privilege imesaidia Nini??? Nikwambie ni akili ya mtu binafsi tuu inayokufanya ufanikiwe Wala hata sio background na kama ni background bhasi inakupa mabawa ya kupaa na sio kutembea au kukimbia.
Na unapowasema wasiofanikiwa, hivi hii nchi ina mifumo kweli mpaka umlaumu mtu kwa kutofanikiwa?
Sijamlaumu mtu yeyote kwa kutofanikiwa, najua msoto wa hii nchi. Nimeshalala selo mara nyingi sana, nimeshaombwa rushwa sana, nimeshapoteza mitaji zaidi ya mara mbili hivyo najua msoto wake na najua kwamba sio Kila mtu anamoyo wa chuma kama wangu.
Na hapa ndio nasema we deserve different even though we have equal chances.
5. Umeangalia masuala ya maadili, yanayoweza kumfanya mtu brilliant anayefuata maadili asifanikiwe, na mtu mjinga asiyefuata maadili afanikiwe kwa wizi tu?
As I speak before INTELLIGENT IS HOW YOU ADAPT TO CHANGES, hakuna maadili yoyote kama hutoweza kuitumia akili Yako vizuri.
Mostly of people sio kwamba ni maadili ni kwamba they are cowards.