kwedikwazu
Member
- Dec 17, 2016
- 18
- 15
WANAHARAKATI wa masuala ya kisiasa akiwemo aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbpo la Mkuranga Kunje Ngombale Mwiru, wamewataka watanzania kuachana na siasa ‘uchwara’ wanazodai kufanywa na vyama vilivyotangaza kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.
Mwiru pamoja na mwanaharakati mwenzie anayeiwakilisha taasisi ya Society Awareness Felix Makuwa, pia walimtaka Msajili wa vyama vya siasa kuvihoji vyama vilivyotangaza kujitoa ili aweze kubaini kama kweli maamuzi yao hayo yalitokana na makubaliano ya halmashauri kuu ya vyama hivyo au ubinafsi wa viongozi wachache.
Walisema wanachoaamini viongozi wa ngazi wa vyama hivyo wametoa maamuzi hayo bila maamuzi ya vikao halali ndani ya vyama hivyo wakidai kuwa mara nyingi viongozi hao wamekuwa wakurupukaji wanaofanya mambo yao kinyemela suala walilosema limekuwa likiua demokrasia ndani ya vyama hivyo.
“Wanayoyasababisha haya yote yanayoendelea ni viongozi wa juu wa vyama vya upinzani, tena baadhi yao wameenda mbali na kukejeli kuwa vyama vingine katika uchaguzi huu havina hata wabunge bungeni hata vikiamua kushiriki, hiyo ni kejeli zaidi msajili anapaswa kuvifuatilia ili kuona kama vilijitoa kutokana na maamuzi ya halmashauri kuu ya vyama hivyo” alisema Kunje.
Alisema anachoamini vyama hivyo vyenye wabunge ndiyo hasa vinavyoua suala la upinzani kwa kuwa mara nyingi wabunge wao hutoa ahadi hewa kwa wananchi kwa kuwatajia mambo mengi ambayo endapo watapewa ridhaa watawafanyia lakini mwisho wa siku huishia kuvimbisha matumbo yao bila kutekeleza jambo alilosema huwapa hasira wananchi hao na kukataa kuwapa kura zao kipindi kingine.
“Tena itapendeza kama msajili wa vyama vya siasa atawashughulikia wabunge hao ambao baadhi yao wamekuwa wakichukua posho za bure bungeni bila hata kuingia katika vikao vya bunge zaidi wamekuwa wakipiga kelele zisizo na tija na kusababisha maneno ya hovyo katika jamii.
Alisema alipotangaza kumuunga mkono Rais John Magufuli wakati akigombea Ubunge Mwaka 2015, aliona hakuna sababu ya kupoteza kura yake kumchagua rais asiye faa zaidi ya kiongozi huyo ambaye hadi sasa ameweza kuipa thamani kura yake kwa kufanya mambo mengi ya kimaendeleo.
Kwa upande wake Makuwa alisema kama ingewezekana uchaguzi ujao asimame mgombea yoyote katika nafasi ya kiti cha urais na kumuacha Rais Magufuli aendelee na nafasi yake ili kuokoa fedha ambazo zingetumika katika kampeni yake ziweze kwenda katika kuhudumia maendeleo.
“Rais aachwe katika nafasi yake, tutachague wabunge tu, anafanya mambo mazuri katika taifa hili ambayo kila mtanzania anayaona” alisema Makuwa na kudai kuwa amezoea kuona tabia ya kususa kutoka katika vyama vya upinzani hivyo siyo jambo la kushangaza kuona vikisusia tena auchaguzi wa Serikali za mitaa.
Alisema hata katika mchakato wa katiba mpya katika utawala wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, wapinzani hao walisusa ambapo aliwataka wafuasi wao kuacha kuwaunga mkono viongozi wao wanaoanzisha migomo hiyo kwa madai kuwa wananyima kutumia haki zao za kidemokrasia kuwachagua viongozi wanaowataka.