Upinzani umeshinda katika hili pia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani umeshinda katika hili pia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eliphaz the Temanite, Oct 25, 2010.

 1. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuna picha za akina mama wenye watoto hapa wanahudhuria mkutano wa campaign wa Dr Slaa. Picha hii imenifanya niadike thread hii. Kwa mda mrefu sana vyama vya upinzani vimekuwa vikipakwa matope kuwa ni vyama vya wenye fujo na vurugu akina mama wenye watoto kama hawa wasiwenza kuhudhuria campaign. Makubwa yamefanyika kuifuta dhana hii na taratibu wananchi wameanza kutuamini!

  Nafahamu hii ni habari mbaya kwa CCM maana mlizoea kula vya gizani!


  Ila mgombea wenu nae katia fora! Kuambia njoo kwenye mdahalo! Kaingia uvunguni! Wakamwambia basi uje huu madahalo wa STAR TV Slaa atakuwa mbali wewe Dar yeye mwanza, mpelekeni kinana!!!!

  Hawezi kusimama na mtu aliye safi!!! Ataongea nini???
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hii ndo gharama ya kuwa mchafu na mfisadi....Unaona aibu hata kwa kivuli chako,shame on him!
  Ndio maana huyu jamaa anaona nafuu kukaa nje ya nchi na kusafirisafiri tu, maana huku nchini anaona soni..pheeeeeew!
   
 3. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Aibu kubwa sana!!
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Ila JK amekuwa low sana kukwepa midahalo.
   
 5. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  PJ,
  Kuna wakati huyu jamaa alipokuwa akija Arusha watu wanajipanga barabarani ili tu wamwone Kipenzi chao. Hata mie nilijikuta nimo! Tena Kaskazini kukawa na bahati kweli, maana hata waziri mkuu alitokea huko. Mara naye Nancy Sumari akawa mrembo! Ikawa furaha tupu huku kaskazini. Misafara ya Rais akienda Ngurdoto, Waziri Mkuu akienda Monduli na Longido , Nancy akiwapungia watu wake mkono mrembo wa furaha.....
  Lakini wapi bwana, Panya ni panya tu, hata avae ngozi ya chui. Ghafla EL akatoa meno yake, JK akaonyesha sura yake halisi: tukabaki tumeduwaa....tunajiuliza, hivi huyu ndiye JK? Huyu tuliyekuwa tunamwabudu kama Mungu? huyu ambaye tulidhani aliporwa ushindi wake na Mkapa mwaka 1995? Tukaanza kuona aibu kwa kujitangaza wafuasi wake. Roho zikatusimama juu, maana kila kona akaweka mashushu , ukiropoka tu unalo!
  Nikaanza kuamini ya Mwalimu, kumbe aliona mbali. Ile dhana ya kuwaita wahuni nikajua maana yake sasa.
  Na akamalizia kwa usanii wa mwisho: Kwa kuwainua mikono wale aliowashambulia kwamba ndiyo wameyumbisha serikali kwa ubadhirifu....alipoanza kwa EL, tukajua kumekucha: Akafuata kwa Chenge, Mramba , RA.
  Halafu akawageukia makamanda wa ufisadi: Mbunda wa Arusha ( Mkurugenzi) amefutwa kazi.
  Mkurugenzi wa Hai, amefutwa kazi.....
  Kamanda wa TAKUKURU Kilimanjaro amefutwa kazi...
  Sijui ni wangapi tutabambikiziwa kesi za ujambazi, kufutwa kazi nk baadaye kama JK atashinda....
  Ni kilio na kusaga meno.....
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kinyume chake, Kina mama wenye watoto hawewezi kuhudhilia mikutano ya CCM, kwa sababu wanabebwa kwenye malori. Pemba wasababisha vifo, Karatu wamepeleka watu toka Arusha mjini kwa malori. Wanambiwa habari ya bodi ya maji wamenyamza, hawajui bodi ya maji.
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Inawezekana hayo ni maelekezo ya kitaalamu ya Shehe Yahya Hussein kuwa muungwana asishiriki mdahalo wowote.
   
 8. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  chadema gooo we have to win this battle on 31
   
 9. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Siwezi kusema ni wapinzani wameshinda hakuwa na ubavu huo. Hivi sasa si CCM v.s CHADEMA no ni CCM v.s WANANCHI upo hapo. Kwa bahati Chadema wamekuwa upande wa wananchi.
   
Loading...