Upinzani Tanzania umenunuliwa rasmi

Upinzani Tanzania umenunuliwa rasmi

Kwa jpm kutokushinda nakupinga 100% ila kwa wabunge hao 40 naweza kukuunga mkono 95%. JPM had sasa wakiweka picha yake igombee na maza inapita kwa zaidi ya 70% 😁😁😁
Kwa Tume HII ya Uchaguzi iliyopo pamoja na ma DED na ma PoliCCM, hapatakuwa na mapya, matokeo si mtajipangia wenyewe jinsi mtavyotaka yasomeke
 
Rais Samia jikite kufungua na kuanzisha miradi, jikite kupambana na mfumuko wa bei, jikite kuhamasisha viwanda .
Viwanda ndiyo vitanunua mazao ya wakulima ,viwanda ndiyo vitazalisha ajira nyingi sana.
Huwezi kupeleka nchi uchumi wa kati kwa kukutana na Mbowe mara kwa mara.
Juzi Prof Lipumba amenukuliwa akisema Rais Samia atashinda kwa kishindo mwaka 2025!!
Zito Kabwe ndiyo hivyo tena amekuwa kasuku wa ccm kila siku ni kusifia tu.
James Mbatia ndiyo hivyo tena kutwa kusifia mama anaupiga mwingi.

Inasikitisha sana chadema kununuliwa, Lisu na Lema huko wanakolelewa wamekuwa kama misukule hawajui washike lipi waache lipi maana mwenyekiti wao hatabiliki, muda wowote anabadili gia angani kama alivyofanya mwaka 2015 kwa kununuliwa na Lowasa.
Mbowe alipotoka tu jela akakimbilia Ikulu kwenda kunywa chai badala ya kuwashukuru kwanza waliompigania!!.

Sasa tumaini pekee liliobaki kwa wapenda mabadiliko na ulinzi wa kweli wa rasilimali za nchi yetu ni UMOJA PARTY.
Mungu ibariki Umoja party ipate usajili haraka .
tulishawaambia tanzania hakuna upinzani kuna wasaka tonge tu tuombe Mungu atokee kigogo mwenye nguvu na anayejali maslahi ya nchi aanzishe chama chake ili twende naye 2025.
 
Back
Top Bottom