Pamputi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2016
- 982
- 724
Mwanadamu mmoja alikua akisafiri na mkewe wakitumia usafiri wa punda yaanai wakiwa wamempanda punda yule lakini wakiwa njiani katikat ya safari yao wakakutana ma wanadamu wakawapazia sauti wakisema
''ninyi watu hamuoni ya kuwa mnamuumiza punda huyo iweje ninyi wote wawili mumpande punda mmoja?
Jamaa kuskia hivyo akaona isiwe shida akaona amwambie mkewe ashuke apande yy peke yake na mkewe akakubali safari ikaendelea lakini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine wakamdhihaki tena bwana yule wakisema
''Wewe mbona ni mwanaume usiye na huruma yaani wewe umepanda punda huyo na kumwacha mwanamke wako atembee em kuwa na huruma hata''
jamaa akaona isiwe shida acha nishuke apande mke wangu na safari ikaendelea
Wakiwa njiani tena wakakutana na wanadamu wengine tena na walipomtazama tu bwana yule na mkewe wakaangua vicheko vya dharau wakisema
''Tazama mwanaume yule asivyokua na akili yaani yeye anatembea kwa miguu na kumuacha mkewe apande punda?''
jamaa kusikia vile akaona mke wangu isiwe shida acha tushuke sie na kumuacha punda atembee mwenyewe sie tutembee kwa miguu basi wakafanya hivyo na safari ikaendelea lkini walipofika mbele wakakutana na wanadamu wengine nao walipowaona tu wakawadhihaki wakisema
''Tazama wajinga wale watembea kwa miguu ilihali wana punda na wanaweza kumpanda''
Basi baada ya mambo yale jamaa akawaza ni jambo lipi lilio jema kwa mwanadamu hata umfurahishe akakosa
Nimekumbuka kisa hiki nikawatazama na wapinzani wetu nkajikuta nacheka sana
Leo wanapinga ufisadi
Kesho wanatetea ufisadi
Leo wanadai huyu mtu natumia ilani yetu
Kesho huyu mtu hazingatii utawala wa sheria
yaani ilimradi tu waseme
Mungu ibariki Tanzania