Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Inasikitisha sana Tanzania kutuaminisha kuna Upinzani wakati hakuna mawazo mbadala. Ilitegemewa kama wanaona CCM inakosea waseme wao wangefanyaje katika kuwaletea Wananchi Maendeleo!
Mfano Rais kaamua kubana matumizi ya Serikali na kukusanya mapato ya Ndani ili kupunguza pengo la utegemezi wa Serikali kwa Wahisani.
Ajabu anaamka mtu anayejiita Mpinzani na kulaumu Serikali ya CCM kunyimwa Misaada ya MCC badala ya kutoa mapendekezo ya Nchi kujitegemea na kuachana na Misaada yenye Masharti ya ovyo.
Serikali inachukua hatua za kusimamia Sheria ikiwamo ya Mazingira kwa kubomoa nyumba zilizojengwa bila kuzingatia Sheria za Mazingira, anajitokeza mtu kuwatetea waliobomolewa jambo ambalo ni unafiki mkubwa na dalili za kujitafutia umaarufu usio na tija kwa Nchi.
Serikali inachukua hatua ya kutumbua Majipu , anajitokeza mtu kwamba Wafuasi wa UKAWA wanaonewa! Shameful! Ajabu hakuna Siku hata moja Wapinzani wamependekeza kubana matumizi kwa kukataa posho zao Bungeni.
Tungewaona wa maana kma wangelisimamia hilo kwa Vitendo ili waoneshe wana dhamira ya kweli ya kumkomboa Mtanzania, lakini wapi! Ubinafsi tupu!
Wapinzani kama kweli wapo waje na Mawazo Mbadala ili hata kama tukiamua kuwajaribu tuwe na uhakika japo kidogo nini watafanya. Kinyume chake wasitarajie kuchukua Nchi maana bado hawajakomaa na ndio maana siku zote hata Mgombea Urais hawana! Watapewaje Nchi! Watasubiri sana labda 2050!!