Upinzani mmejisahau sana kuhamasisha watu kujiandikisha daftari la wapiga kura!

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,402
74,004
Mmedhamiria kutosusia uchaguzi Mkuu ujao. Sawa, wazo zuri. Lakini mmesahau kuwahamasisha wapiga kura kujiandkisha! Kosa la kwanza.

Achana na hoja ya maridhiano, CCM wanajua wanalolifanya, siyo kuwa hawana akili ya kuona maovu (zuri na baya), yao, wanayaona ila kwa vile wameshika mpini, hawana haja ya maridhiano! Achana na agenda hiyo. Lugha hiyo hawawezi kuisikiliza. Lugha wanayoweza kuisikiliza ni ipi? Hakuna wa kuwasikiliza kwa lolote. Wahimize watu wa CHADEMA ni Msingi wahamasishe watu.

Kosa la pili, mnajua fika , for sure, if not double sure, kuwa yale yale ya uchaguzi wa serikali za mitaa yatatokea uchaguzi ujao, pengine hata zaidi, mmejiandaa vipi na hilo?

Mmenyamaza, kosa la pili.
 
Suluhisho ni Tume huru tu ya uchaguzi,unaweza ukahamasisha watu wajiandikishe na wakajiandikisha,wakakupigia kura lakini mwisho wa siku ukapigwa!
 
kampeni hii ina sura ya kitaifa hivyo ingepaswa kuratibiwa na makao makuu (viongozi wa kitaifa). viongozi wa majimbo eg wabunge au wilaya au mikoa au kanda wangeongezea nguvu tu.

lakini kwa ugaidi wenu CCM mmewakataza viongozi wa kitaifa, kimkoa na kanda kufanya mikutano isipokuwa wabunge tu tena ndani ya majimbo yao.

kama kweli unashauri kwa dhati na sio unafiki ilikupasa uelewe kwamba chama chako cha kishetani kinamzuia Mbowe kuhutubia Bunda, au Zitto kuhutubia Masasi au Mnyika kuhutubia Itigi
 
Mkuu sisi kazi tunafanya na hatutaki publicity. Kama ungejua sababu ya Serikali ya CCM na chama chake kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ungeelewa ninachosema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanga kwa taarifa yako mimi nawaunga mkono CDM in all aspects of their strugle. Najua hayo yote ya kuzuiwa kufanya kazi ya siasa. Acha hao hata mimi nina haki yabjufanya mkutanonwa siasa as longbas nimefuata taratibu, lkn nakatazwa kwa ubabe /udikiteita wa jiwe.
kampeni hii ina sura ya kitaifa hivyo ingepaswa kuratibiwa na makao makuu (viongozi wa kitaifa). viongozi wa majimbo eg wabunge au wilaya au mikoa au kanda wangeongezea nguvu tu. lakini kwa ugaidi wenu CCM mmewakataza viongozi wa kitaifa, kimkoa na kanda kufanya mikutano isipokuwa wabunge tu tena ndani ya majimbo yao. kama kweli unashauri kwa dhati na sio unafiki ilikupasa uelewe kwamba chama chako cha kishetani kinamzuia Mbowe kuhutubia Bunda, au Zitto kuhutubia Masasi au Mnyika kuhutubia Itigi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtazamo tu kamanda, Democrats kupitia Congress walimhukumu Trump kuwa anasigina katiba lakini Republicans kupitia Senete wamemsafisha Trump kuwa anaheshimu katiba.

Wangalau wao wanamfumo ya kuhoji kuwa rais wao naheshimu katiba. Hapa kwetu je? Narudia tena Magufuli naheshimu katiba
 
Chadema hawana shida ya kuhamasisha wapiga kura wala kudai tume huru ya uchaguzi!
Shida yao kubwa ni Membe agombee wampe kura iwe ccm au upinzani basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmedhamiria kutosusia uchaguzi Mkuu ujao. Sawa, wazo zuri. Lakini mmesahau kuwahamasisha wapiga kura kujiandkisha! Kosa la kwanza.

Achana na hoja ya maridhiano, CCM wanajua wanalolifanya, siyo kuwa hawana akili ya kuona maovu (zuri na baya), yao, wanayaona ila kwa vile wameshika mpini, hawana haja ya maridhiano! Achana na agenda hiyo. Lugha hiyo hawawezi kuisikiliza. Lugha wanayoweza kuisikiliza ni ipi? Hakuna wa kuwasikiliza kwa lolote. Wahimize watu wa CHADEMA ni Msingi wahamasishe watu.

Kosa la pili, mnajua fika , for sure, if not double sure, kuwa yale yale ya uchaguzi wa serikali za mitaa yatatokea uchaguzi ujao, pengine hata zaidi, mmejiandaa vipi na hilo?

Mmenyamaza, kosa la pili.
Hadi waruhusiwe na mabeberu wanakojikomba kila uchwao
 
Ni kweli wapo busy na mambo meengiiii sana wanasahau hapa wanapo jiandikaisha watu vijana wengi hawaji kujiandikisha wapo busy kudai tume huru wakija kupewa tune huru wapiga kura hawapo upande wao
 
Kwani upanzani pake yao ndy wanatakiwa kuhamasisha watu kujiandikisha? Ccm wao wameshajiakikishia ushondi hata bila watu kujiandikisha?
 
kuna sheria imetungwa na serikali ya awamu hii ,inakataza kuhamasisha
 
Back
Top Bottom