Upinzani Bandia na Wapinzani bandia

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Linapokuja suala la siasa za upinzani hapa Afrika huwa niña kigugumuzi kwakweli.Hii inanirudisha mwaka 1992 wakati wa ile tume ya maoni ya wangapi wanataka vyama vingi na wangapi wanataka kuendelea na mfumo wa chama kimoja ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania tulianza kuutumia mwaka 1965 baada ya Mwalimu Nyerere kufuta mfumo wa vyama vingi.

Hapa majibu ya ile tume yalikuwa kama ifuatavyo aslimia 80 walitaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja wakati asilimia zilizobaki (20) walitaka mfumo wa vyama vingi.Hapa lazima ujiulize ni wakina nani walioanzisha hivyo vyama vingi? na walitoka wapi? na nani aliwapa nguvu ya uanzishaji wa hivyo vyama? Katika haya maswali utagundua ni wazi kabisa walioanzisha vyama vya upinzani nchini Tanzania ni kutoka katika lile kundi la asimilia 80 ambao walitaka mfumo wa chama kimoja na hiki ndo kinapelekea nchi hii kukosa wapinzani wakweli.

Wanasiasa endeleeni tuu kutushika Masikio
Siku tukishtuka Magari ya kubebea Ng'ombe mtapanda wenyewe kwenda kujaza viwanja.

#TatizoSioMfumo
#TatizoNiWatu
 
Labda nisubiri comment,binafsi sijaelewa!Ila ngoja nikuulize maswali machache:
-Idadi ya watanzania walikuwa wangapi wakati wa upigaji kura huo?
-Ulitaka wapinzani washuke kutoka mbinguni?
-Hiyo 20% unayosema,haikutosha kuanzisha upinzani?Kwanini useme wametokana na 80%?Umejuaje kama waliopiga kura ya kukataa mfumo wa vyama vingi ndio walianzisha upinzani?

Kila jambo nadhani lina mwanzo wake!
 
Kwanza unauhakika gani hayo matokeo yalikuwa sahihi na sii fake? unafikiri Nyerere aliposema hata kama ni wachache wanaotaka mfumo wa vyama vingi wapewe na serikali ikakubali unafikiri hakujua kuwa matokeo yalikuwa yakupika/fake.

Vyama vingi ndivyo vilimuweka Nyerere madarakani, yeye akatumia dola kuviua, ila ndani ya mioyo ya watu bado vilikuwepo, hivyo Nyerere alijua wazi mchezo uliochewa na serikali yake ya zamani ya kuchachua matokeo, sasa ili kuua nguvu upinzani ndio serikali yenyewe ikaanzisha vyama vyake vyenyewe, na mpaka sasa vipo vingi vya aina hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom