Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,515
- 4,230
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema mtu mmoja amekamatwa nchini Poland akiwa na kobe zaidi ya 100 wakitokea nchini Tanzania bila ya kuwa na vibali vya usafirishaji wa wanayama hao.
Dkt. Ndumbaro ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amesema kuwa tukio hilo limetokea wiki mbili zilizopita nchini Poland na kwamba inaonekana kuna uzembe ulifanyika katika Uwanja wa Ndege nchini Tanzania kutokana na mtambo wa ku-scan kutokufanya kazi ipasavyo.
Ndumbaro ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara ya usafirishaji haramu wa Binadamu ambacho kinaundwa na maofisa wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha, ndumbaro amewataka katika majukumu yao, kikosi hicho waongeze juhudi kudhibiti usafirishaji wa rasilimali za nchi hasa katika maeneo ambayo ndio malango ya watu hao.