Upigaji unarudi kwa kasi. Kobe 100 wa Tanzania wakamatwa Poland

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,494
4,206
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema mtu mmoja amekamatwa nchini Poland akiwa na kobe zaidi ya 100 wakitokea nchini Tanzania bila ya kuwa na vibali vya usafirishaji wa wanayama hao.

Dkt. Ndumbaro ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amesema kuwa tukio hilo limetokea wiki mbili zilizopita nchini Poland na kwamba inaonekana kuna uzembe ulifanyika katika Uwanja wa Ndege nchini Tanzania kutokana na mtambo wa ku-scan kutokufanya kazi ipasavyo.

Ndumbaro ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara ya usafirishaji haramu wa Binadamu ambacho kinaundwa na maofisa wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, ndumbaro amewataka katika majukumu yao, kikosi hicho waongeze juhudi kudhibiti usafirishaji wa rasilimali za nchi hasa katika maeneo ambayo ndio malango ya watu hao.
20220723_140529.jpg
 
Ni serikali ya wapigaji expect anything.

Walitaka waanze kusafirisha wanyama mkapiga kelele sasa wanasafirishwa kimia kimia.

Kama mtambo wa scanning haukua unafanya kazi maana yake madawa ya kulevya yaliingia, watu waliingia kwenye ndege na vitu visivyoruhusiwa na kila aina ya uovu.

Nchi ya kuupiga mwingi.
 
Hii taarifa imetangazwa,
Itajadiliwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari alafu itakuwa imekwsha wanaendelea na issues nyingine Wala hakutokua na kauli ya kuweka sawa, maana hizi ni biashara ya watu ni vile Poland wamewacboma na hapo watakuwa wanawaza Kobe wakiachiwa Poland wamfikie vipi mnunuzi wao. Ooh my country 😩
 
Mbona hiyo kawaida sana.toka atutoke mpambanaji wa kweli biashara ya meno ya tembo,utoroshaji madini,ufujaji was Mali za umma umekithiri sana.Airports zetu zimekuwa vichochoro vya kupitisha huu uozo.wtz kila siku tunaona na pakupeleka hizo taarifa hamna maana ukijifanya kwenda polisi unabambikwa kesi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema mtu mmoja amekamatwa nchini Poland akiwa na kobe zaidi ya 100 wakitokea nchini Tanzania bila ya kuwa na vibali vya usafirishaji wa wanayama hao.

Dkt. Ndumbaro ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amesema kuwa tukio hilo limetokea wiki mbili zilizopita nchini Poland na kwamba inaonekana kuna uzembe ulifanyika katika Uwanja wa Ndege nchini Tanzania kutokana na mtambo wa ku-scan kutokufanya kazi ipasavyo.

Ndumbaro ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara ya usafirishaji haramu wa Binadamu ambacho kinaundwa na maofisa wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, ndumbaro amewataka katika majukumu yao, kikosi hicho waongeze juhudi kudhibiti usafirishaji wa rasilimali za nchi hasa katika maeneo ambayo ndio malango ya watu hao.View attachment 2301126
Ungerudi kwani wangekamatwa? Aliyetoa taarifa ni Waziri husika kwa hiyo huna cha kutuambia..

Mwisho na wewe piga kama unaweza.Sukuma gang hadi saizi hamjaleta jibu la upigaji wa Til.1.2
 
Ungerudi kwani wangekamatwa? Aliyetoa taarifa ni Waziri husika kwa hiyo huna cha kutuambia..

Mwisho na wewe piga kama unaweza.Sukuma gang hadi saizi hamjaleta jibu la upigaji wa Til.1.2
Hio trilion alichukua nani we kiazi? Mnayumbishwa na mlamba asali zito kabwe ambaye yeye alifungiwa mrija wa hela. Cheap propoganda mkimaliza mnarejea kwa Ben Saa8
 
Back
Top Bottom