Upi ni uhalisia kuhusu pundamilia?

Upi ni uhalisia kuhusu pundamilia?

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
4,700
Reaction score
1,093
Ndugu wana-jamvi

Hii inaniumiza kichwa naombeni mnisaidie kujua rangi ya pundamilia,
Je Pundamilia ni mweusi ana mistari myeupe au ni mweupe ana mistari myeusi.Nawasilisha
 
hii ipeleke chit chat, kule utapata majibu bila wasiwasi
 
Subiri wataalamu wa viumbe hai watakupa jibu zuri
 
Hiyo unatumia akili yako tu hakuna haja akili ya kuambiwa. Punda milia ana mistari yenye rangi ulozotaja.
 
Pundamilia ana maajabu sana kwenye rangi zake,ana rangi nne,mbali ya zile nyeupe na nyeusi unazoziona ana kijani na nyekundu pia,ukifuta nyeupe inajitokeza kijani,ukifuta nyeusi inatokea nyekundu,jaribu siku moja utaona
 
Hizo hua sio rangi! Pundamilia hua wanavaa jezi za New castle .
Kumbe na umri wako wote ulikua hujui kitu simpo kihivi ?
Haya ushajua sasa watangazie na jiranizo .
 
230px-Beautiful_Zebra_in_South_Africa.JPG
 
pia inasemekana kuwa hakuna pundamilia anayefanana na mwingine katika ile mistari yake. yan kila mmoja ana mistari ya aina yake pekeyake!
 
Pundamilia ana maajabu sana
kwenye rangi zake,ana rangi nne,mbali ya zile nyeupe na nyeusi
unazoziona ana kijani na nyekundu pia,ukifuta nyeupe inajitokeza
kijani,ukifuta nyeusi inatokea nyekundu,jaribu siku moja utaona

Unatumia ufutio gani nami nikajaribu?
 
Back
Top Bottom