einstein newton
JF-Expert Member
- Oct 18, 2015
- 1,969
- 2,684
We Ni Professor mkuu?Watanzania siyo wasahaulifu
1. Wamelia sana vyuma kukaza
2.Wakalia sana uonevu wa nyumba uliofanyika mbezi-Kimara huku wale wa mwanza wakaambiwa nyinyi msivunjiwe
3.Wakalia sana sheria ya bodi ya mikopo ya 15%
4.Leo hadi taulo za wanawake zinakatwa kodi
5. Wana Kagera wakaambiwa "Wanataka hela sababu ya tetemeko kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko"
6.Watanzania wamenyang'anywa Bunge LIVE leo imegeuka MTU live
7. Watanzania wanakumbuka vizuri kuwa nyongeza za mishahara ya wafanyakazi zilizopo kwa mujibu wa sheria hazipo
8.Watanzania wana kumbukumbu nzuri ya manunuzi ya wanasiasa na kuwatia gharama kurudia chaguzi
9. Wakulima wa korosho wana kumbukumbu nzuri sana walichotendwa
10. Wa mikoa ya kaskazini hawawezi kusahau kauli waliyoambiwa kuwa miaka yote ilikuwa wao tu wangoje na wengine wafaidi
11. Vijana wanaomaliza vyo vikuu utawaambia nini, mwaka wa nne huu ajira za manati
12. Watanzania wapenda ustaarabu wanaona jinsi Wanasiasa akina Lema, Sugu, Mdee, Mbowe, walivyonyanyaswa, kesi zenye dhamana hawapewi dhamana etc
13. Watu wana kumbukumbu nzuri tu ya ripoti za CAG na trilion 2.4 amabzo maelezo yake yamepinda
14. Watanzania Hawajamsahau Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na wengine
15. Wana Singida hawatopata Shida kumlilia kijana wao Tundu Lissu, iliwauma, inawauma na itaendelea kuwauma
16. Binti Akwilina aliliza wengi, aliumiza wengi
17. Unafikiri Watanzania wamesahau nyodo za Mwanamfalme wa Dar, Dharau zake, kudekezwa kwake, Wanasubiri tu moto uchanganye wafanye maamuzi ya ghadhabu hapo 2020
18. Asidhani tumesahau Trilion 2.4 hazina maelezo yaliyonyooka zimekwenda wapi
19. WanaYanga wanamkumbuka Manji wao, Wana Simba walimlilia sana Mo kwa wiki mbili
20. Wauza mbaazi hawajasahau old good days
21. Watanzania bado wanakumbukumbu nzuri za Magazeti ya zamani yenye uchambuzi bila hofu, wanasikitishwa na magazeti yaliyojaa uoga leo, kujipendekeza pendekeza, lakini nani aliyetufikisha hapa?
22. Watanzanai watasahau vipi kwa mfano walipokunywa chai bila sukari kwa uhaba wa sukari mwaka 2016?
23. Wazazi wa watoto waliopata ujauzito shuleni waliumia sana kuambiwa kuwa "sisomeshi wazazi"
24. Na wastaafu wanaosumbuliwa nenda rudi, mafao yao hakuna lakini kuna hela zakujenga uwanja wa ndege Chato huzuni yao haipimiki
25. Unafikiri wamachinga wanapenda kulimwa 20000 ya vitambulisho, tena kwa tozo ambayo haijaidhinishwa na bunge?
26. Vipi wale waliotumbuliwa majukwaani kinyume cha taratibu za utumishi,“ jamani nitumbue nisitumbueeee?, tumbuaaaaa”,
27. vipi wafanyabiashara waliobambikiwa kodi?, kilio cha machozi yao hakiwezi kukaushwa na kikao kimoja mbele ya TV Live, vipi familia zao ziliteseka namna gani, ziliumia kiasi gani, vipi mtaji wao?
28. Vipi kuhusu Trilion 425, Vipi waliotajwa kwenye ripoti ya Makinikia kuwa ndo waliotufikisha hapa, ameshakamatwa nani?, kesi zao ziko mahakama gani?, hatua gani zimeshachukuliwa dhidi yao?, Hizo Trilion 425 tunazipata lini?
29.Eti 5000 za kung'arishia viatu?,Madereva wameumizwa sana, wametozwa nyingi, wamepigwa tochi sana, hawajasahau hii
30. Na wavuvi waliochomewa nyavu, walionyang'anywa nyavu, nani atawarudishia mitaji yao?, nani alisikia hisia zao?
Kwa hakika
1. Mikoa ya Kusini atapata tabu sana
2.Mikoa ya kaskazini ndiyo kabisaaa
3. Mkoa wa Singida kwa brother Lissu ndo asahau kabisa
4. Dar es salaam ya waelewa wanahitaji mtu jasiri tu wa kusema nam'goa
5. Mbeya ndo asahau
6. Kule kwa Ruyagwa Zitto huko ni waelewa sana
7. Kagera huko bora asahau bado kumbukumbu ya Tetemeko ingali hai
8. Kule Zanzibar kwa BRAZA Maalim asahau moja kwa moja
Atabaki na Mwanza na Nyanda za juu Kaskazini, na shinyanga na Geita, kwenda Katavi, Dodoma na Kidogo Pwani
Membe akichukua fomu patachimbika!
(Nyie Ndio Wana Jf wenyewe)