Upepo umegeuka, Marafiki wa Lowassa wapinga swahiba wao kwenda CHADEMA, Apson Matatani

Lizaboni

Mkuu LISABON nimekuwa ninafuatilia michango yako hapa JF kwa karibu sana, na kwa sasa ninaomba nikujulishe haya kwani ni kwa faida yako:
1. Ukimtaja EL kuwa ni fisadi ni moja kwa moja kuwa viongozi wakuu wako nao ni mafisadi (hii haitaji justification)
2. Kama Mwenyekiti wenu alishindwa kumfukuza au kumkemea mbele ya watanzania wote, basi nafikiri jibu unalo.
3. Kama mna amini kweli ni fisadi basi mwambie mwanasheria wa serikali au chama chenu ampeleke mahakamani ( hapa mtakuwa wengine mashahidi au washitakiwa wakubwa, nafikiri unaelewa maana yake)
4. Huyu mtu tumchukulie kama binadamu yeyote. Na jaribu kufikiria mchango wake kwa taifa. Haikutakiwa kumdharalisha kama mlivyofanya DODOMA. Na sababu zenyewe hazikuwa za kimsingi (hapa tunaweza kuwaita wakina Dr. Nchimbi, Mhs Simba, na Mhs Adamu .. ni malaika wateule)
5.Ikumbukwe katika hali yoyote ile ya kumtendea mtu mabaya na hasa kumyima haki, basi matukio kama haya yatatokea na ndiyo maana unaona hili swala linashika kasi!

ONYO:
Ni viongozi wengi ndani ya chama chako na hasa wale wenye nyazifa kuliko wewe kada wa Lumumba wamekaa kimya kwani wanajua hasa KOSA liko wapi. Na hutaona wanalopoka kuhusu huyu mhs EL kwa sababu anajua mengi mabovu ambayo yakiwekwa wazi hakauna atakaye salimika. Ni bahati mbaya wewe unacheza ngoma USIYO IJUA.

LENGO:
Hapa lengo kubwa ni kubadiri mfumo mbaya wa kuruhusu vitendo vya kifisadi. Ingeleikuwa rahisi kwenu kumuacha EL agombee lkn mnakubaliana kuuvunja mfumo wenu ulio ota mizizi ya kifisadi.

Mkuu ukisema kanyimwa haki una maana gani? Alizuiwa kuchukua fomu? Alizuiwa kutafta wazamini au vp mkuu? Alikatwa kama wenzake walivokatwa mbona wenzie wametulia ye ni nani hasa hadi iwe nongwa .ccm haiogopi mtu amekuja huko mnapomuabudu
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Mkuu. Pole na wewe
Nami niongezee, "Pole sana!" Uliwakusanya wapi na ukawahoji wakakueleza hayo? Ama ni kikao gani walichokaa wakapitisha hayo maazimio na wakakuchagua kuwa msemaji wao? Kwa nini unamchukia sana huyu Apson Mwang'onda? Wafuasi wa Lowasa wanajua fika hatua za kufuata na kwa bahati nzuri wengi wao walishachukua hatua na wala hawadanganyiki wala kubabaishwa na hekaya za Lizaboni!
 
Lizaboni unavituko ndugu yangu.Haya huyu Regina Lowassa ni kati ya marafiki zake au ni mkewe?Umeongea mpaka umejichanganya.

Sasa mlitaka aondoke amekwisha ondoma tena mnarudi mnasema hamtaki aondoke mnanishangaza kweli kweli.Muda mfupi uliokwisha ulikuwa uko busy unawananga Chadema ghafla upepo umebadilika.

Amakweli ukitaka kuona 'Nyeti za kuku'Subiri upepo ukivuma.

Kiberiti kimetingishwa kumbe ndani hakuna njiti duh!Sasa kesi ya mahakama ya Kisutu kesho imehamishiwa wapi?

Lizaboni angalia yai hili visa likakupasukia wenye nalo wako safari Australia wameenda kuangalia Kampuni yao kama inaendelea vyema.

Mdogo wangu achana na Lowasa,vita vya Tembo hivyo utaumia.Waache wenyewe waminyane kaa mbali,utajanikumbuka ndugu yangu.

Fanya yako hajakutana barabarani hao shauri yako....
 
hili jamaa lileta mada jinga kweli,linachezewa mind game na team EL-UKAWA na lenyewe linacheza kweli,kila siku linakuja na mada zinazomuhusu EL, mpaka linasahau kuja na thread za kumnadi mgombea wake makufuri.ama hakika mwaka huu kazi wanayo maccm.

Ni ngumu sana kukumbuka afanyayo katika kipindi hiki. Maana yanayotokea hawakuwahi hata kuyafikiria, acha wachanganyikiwe, inaweza ikawasaidia labda.
 
Pasco.,shemeji yangu ndiyo umemtupa nduguyo? Maana Lizaboni hakuliki hakulaliki ni Lowassa lowassa.duh,Hivi rafikiyo hana mtoto wa kike?Labda Lizaboni anataka kuoa au kuolewa huko...Mpaka tumechoka na hii riwaya.
 
Lizaboni unavituko ndugu yangu.Haya huyu Regina Lowassa ni kati ya marafiki zake au ni mkewe?Umeongea mpaka umejichanganya.

Sasa mlitaka aondoke amekwisha ondoma tena mnarudi mnasema hamtaki aondoke mnanishangaza kweli kweli.Muda mfupi uliokwisha ulikuwa uko busy unawananga Chadema ghafla upepo umebadilika.

Amakweli ukitaka kuona 'Nyeti za kuku'Subiri upepo ukivuma.

Kiberiti kimetingishwa kumbe ndani hakuna njiti duh!Sasa kesi ya mahakama ya Kisutu kesho imehamishiwa wapi?

Lizaboni angalia yai hili visa likakupasukia wenye nalo wako safari Australia wameenda kuangalia Kampuni yao kama inaendelea vyema.

Mdogo wangu achana na Lowasa,vita vya Tembo hivyo utaumia.Waache wenyewe waminyane kaa mbali,utajanikumbuka ndugu yangu.

Fanya yako hajakutana barabarani hao shauri yako....
Kwani mkeo hawezi kuwa rafiki yako? Tehetehetehe! Tetty, umechanganyikiwa na nini?
 
Back
Top Bottom