Upendo wa kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upendo wa kweli!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, May 6, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Upendo wa kweli!


  Upendo wakati mwingine hufananishwa na kupanda na kushuka kwa nyuzi joto.

  Ni ukweli usiopingika kwamba upendo ambao hutokea wakati wa uchumba ni tofauti na ule wa kwenye ndoa.

  Pia katika hatua ya uchumba wahusika wengi huwa na mtazamo wa kufurahishana ili kufahamiana kunakopelekea kuoana; wakati kwenye ndoa ni maisha, majukumu na kazi.

  Wengi huamini kwamba kwa kuwa wanapendana sana kwenye uchumba basi safari ya ndoa yao itakuwa tambala kama mawindoni kitu ambacho si kweli kwani kitendo cha kuvalishana pete (hata kama dhahabu inatoka south pole au sayari nyingine) pamoja na kipande cha karatasi unachotia saini haviwezi kukufanya uwe mzuri kumpenda mke wako au mume wako ambaye umefunga naye ndoa.

  “True love is a Process”


  Unapokuwa engaged unajisikia raha sana (in your fantasy land) kwani zile hekaheka za mipango na maandalizi ya ndoa/harusi, matarajio ya honeymoon, furaha ya kumpata kiumbe ambaye ulikuwa unamsubiri miaka yako yote duniani hukufanya ujisikie raha na binadamu uliyebarikiwa.

  Hata hivyo itafika siku wala si mbali hizo feelings hazitatosha kuifanya ndoa yako idumu na kudumu.


  Utatakiwa (unatakiwa) kuendelea kuijenga ndoa hatua kwa hatua kila siku na kuendelea kumsoma mwenzi wako kufahamu ni vitu gani anavipenda na akivipata basi humfanya ajione anapendwa (mwanamke) na anaheshimiwa (mwanaume).


  Je, unapompa mke wako au mume wako zawadi huwa unatafuta zawadi ambayo wewe unaipenda au anayoipenda yeye?

  Je, unafahamu kwamba hata namna ya kuipokea zawadi kutoka kwa mpenzi wako ni vizuri kujua jadi yao?


  Kuna wengine unapopokea zawadi bila kushukuru kwa kuruka ruka (excitement) huku ukamwambia kwa kumthibitishia kwamba umeipenda na ulikuwa unapenda sana kupata kitu kama hicho maishani mwako hata kama zawadi anayokupa haigusi moyo wako.

  Watu kama hao usiporukaruka kuipokea watakwambia hujaipenda na vita kuu yab tatu ya dunia inaweza kuanza!


  Wapo wengine akisafiri na siku amerudi ile kukutana mara ya kwanza lazima utoe machozi kuonesha ulimkumbuka (ulim-miss) bila kutoa machozi na kutengeneza kamsiba kakiana atahisi huna feelings na yeye na kwamba humpendi!


  Kupenda ni kazi na kazi kubwa ni kumsoma mwenzako maeneo ambayo unaweza kumfanya ajisikia ana mtu bora duniani anayempenda na kumjali.


  Mungu akubariki

  God bless you

  Gott segne dich

  Que Dieu vous béniss

  Må Gud välsigna er

  神の祝福あれ

  قد بارك الله فيك
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Asante kwa maneno yako ya hekima umegusa mioyo ya wengi!

  Nakuunga mkono ndoa ni kama second employment you have to work hard to earn and keep it! Hakuna vya bure bure hapa!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante mama mia umeolewa unafaa kuwa mkwe wangu kwa Mwanangu ?
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mmmmmh!!
   
 5. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli mtupu unapoingia kwenye ndoa ndo true Love itaonekana, mengine ni maigizo tupu, Thanks Mama Mia
   
Loading...