Upendo wa ajabu wa wanyama

Spartacus boy

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
1,864
Reaction score
3,684
Huyu mbwa anaitwa George. Hana furaha na mawazo baada ya kumpoteza rafiki ake wa miaka 12, aitwaye Labrador. Haijulikani baadae kuwa huyu bata alitokea wapi . Inaonekana alitokea kujua hali ya huzuni aliyonayo huyu mbwa . Aliguswa sana na majonzo yake. akaamua kulala karibu nae kumfariji. Inashangaza sana bata kuja nyumbani kwako na kuchangamana na mbwa wako. Haijulikani huyu bata alitokea wapi ila tangu amekuwa karibu nae,George amekuwa halii tena. Toka baada ya hapo George anatabasamu tena.

Tuna la kujifunza hapa.
Credit :Mtandao wa Quora.
 
Niliona mbuga flani huko South Africa mtoto wa tembo aliokolewa baada ya mama yake kuuwa na wawindaji haramu. Wanasema ni vigumu sana kumlea asipokuwa na mama yake, kwanza anagoma kula na anakuwa na mawazo sana. Hivyo walihisi atakufa tu, lakini kuna mbwa pale mbugani akajenga urafiki na huyo mtoto wa tembo, akaanza kula upya na kuwa mwenye furaha. Muda wote wako wote, wanacheza wanakimbizana wanalala wote.

Wanyama wanaelewana huenda wanakuwaga wanapiga story pia.
 
Interesting
 
Quora bhana...!

Tangu nisome fact moja hivi nimekuwa mtu wa kupingapinga mambo mengi sana
yanayotupiwa mitandaoni.

Jamaa aliandika fact zake nyingi nyingi za maana ila fact ya mwisho kabisa ilikuwa inatafsirika hivi;

"90% ya fakti zinazoandikwa mtandaoni ni UONGO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…