Upendo Peneza (CHADEMA) amlipua Rais Magufuli, amtaka alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake

Huwa mkikaa kimya mnakuwa kama vile kuna kitu kinatekenya mwilini.

Unazungumzia umaskini wa nchi kana kwamba umeumbiwa umasikini mpaka siku yako ya kufa!!.

Jitahada zote za kuanzisha na kufufua viwanda lengo lake ni kuondokana na hiyo label ya umasikini.

Mahubiri yote misikitini na makanisani yana lengo la kumpa mtu kiburi cha kuanza kutafuta maisha yaliyo bora zaidi.

Tanzania sio masikini labda tatizo ni sisi wenyewe vichwani mwetu. Kumbuka kuwa hao wanasiasa wa upinzani ambao wewe pengine ni mmojawapo, walikuwa tayari mpaka kutengeneza mifumo ya kimafia kwenye mitandao ili kuihujumu tume ya uchaguzi.

Sijui unaweza vipi kuwahakikishia wanaokusoma kwamba hao waliotumia mabilioni ya fedha wangekuwa na uthubutu wa kutopokea mishahara na marupurupu mengine ya urais.

Phillipo mbona ni kama umehama mada ya nsingi kuhusu mshahara? Nilitaraji ungezungumzia kuhusu huo mshahara. Hiyo dhana ya umasikini mbona ipo tu hata tika tulipokuwa na viwanda. Mbona hata hao viongozi wameepukana na umasikini walipopata madaraka? Huoni wakikosa hayo madaraka wanarudi kwenye umasikini?
 
Alafu anakomaa wananchi tulipe kodi,alitakiwa awe mfano.hata ile kampuni yake ya ujenzi sijui kama kodi analipa.ila mi skuizi wala simlaumu rais na serikali yake,wajinga ni sisi tunaokubali kuishi kindezi hivi.
 
Phillipo mbona ni kama umehama mada ya nsingi kuhusu mshahara? Nilitaraji ungezungumzia kuhusu huo mshahara. Hiyo dhana ya umasikini mbona ipo tu hata tika tulipokuwa na viwanda. Mbona hata hao viongozi wameepukana na umasikini walipopata madaraka? Huoni wakikosa hayo madaraka wanarudi kwenye umasikini?
Hizi ni mada nyepesi na pengine ni za kitoto. Rais anapewa kila kitu bure ili atumikie watu, ili akili yake maarifa na ubunifu wake vizame kwenye kuwafikiria watu badala ya kufikiria bling bling za kimaisha.

Kwangu mimi kwa hii dedication ya Magufuli, sijali kama yeye binafsi halipi au analipa kodi. Ningeumia sana kuona kodi yangu inamtunza rais anayefikiria wizi mkubwa wa mabilioni, anayefikiria kuwa dalali wa kimataifa badala ya kuwa mwakilishi wa hisia/maoni/matarajio ya wanyonge.
 
Kwa hiyo hawezi kulitumikia taifa lake mpaka apate kila kitu bure? Usipolipa kodi ndio unaweza kulitumikia taifa zaidi!?
 
Yaani hata kodi halipi na mtu uko comfortable kabisa huku hata indirect tax nayo haikugusu maana kila kitu unagharamiwa na serikali kuanzia chakula,mavazi,n.k.

Wakati baadhi ya nchi tajiri maraisi wao hawataki hata kupokea mshahara ili fedha hizo zitumike kwa maslahi ya Taifa.

Mama ntile analipa kodi ila Raisi wa nchi halipi kodi tena yeye akiwa ndio Raia namba moja!!

Africa hatujitambui haya mambo ni bora yafanywe na nchi zilizoendelea.
This comment fit again to this thread, as time goes, we are seeing something wrong with, and if you continue posting lower-minded thinking thread like this, my friend, trust me, people who previously used to cheers at you, should have to treat you with caution. Going forward, why can't you come with a well-thought, synthesized and clearly analyzed thread. I'm just trying to make you not loosing your credibility, as Salary Slip we used to know.

All the best,
K
 
Alipe Kodi. Fullstop.
 
Kwa hiyo hawezi kulitumikia taifa lake mpaka apate kila kitu bure? Usipolipa kodi ndio unaweza kulitumikia taifa zaidi!?
Kutolipa kodi kwake mpaka sasa hivi sio mzigo kwenye maisha yangu binafsi na kwa wengi tu ambao wanaguswa kwa wema wa maamuzi anayochukua.

Kutolipa kodi kwake kama kunasababisha watu wapewe haki zao, sioni gharama yoyote kubwa ya kumtunza mtu wa aina hiyo.

Kama anaifungua mikoa kama Kigoma, Lindi na Mtwara, kumtunza yeye na familia yake ni gharama ndogo sana.

Kutolipa kodi ni mzigo mkubwa kama anayetunzwa ana hulka za kujijali yeye na familia yake, kama anazo tabia za kuwatenganisha watu badala ya kuwaunganisha, kama anawagawa watu kwa namna yoyote ile.
 
This comment fit again to this thread, as time goes, we are seeing something wrong with, and if you continue posting lower-minded thinking thread like this, my friend, trust me, people who previously used to cheers at you, should have to treat you with caution. Going forward, why can't you come with a well-thought, synthesized and clearly analyzed thread. I'm just trying to make you not loosing your credibility, as Salary Slip we used to know.

All the best,
K
Kama wewe huu ndio mtazamo wako,alieko kijijini je?
 
My friend, don't rush on this, just think critically, as time goes, you don't know at what rate your credibility is felling down. Just try to re-evaluate it, the way you used to be, and your current logical-thinking status.
All the best,
K
 
Kutolipa yeye kodi au kulipa sio sio la muhimu kwa wanakijiji wanaopatiwa maji sasa hivi.

Kutolipa yeye kodi au kutolipa ni suala la humu mitandaoni, who cares kule mpanda au kibondo ikiwa analolifanya ni kwa faida ya maisha yao mema ya baadae au leo hii??.

Mnatafuta mada kila kukicha, wakati huo yeye kichwa kinamuuma akifikiria namna ahadi zake zinaweza kuwa ni sehemu ya maisha ya aliowaahidi.

Ikifika 2020 mkipoteza majimbo ya uchaguzi, muwe na uhakika kuwa sababu ni kuendekeza mada za kitoto kama hii.

Naona hujamuelewa mleta mada, kulipa kodi ni muhimu kwa kila raia. Swali linakuja kwanini yeye halipi kodi wakati anahimiza watu walipe kodi? Na Katiba yetu inasema hakuna mtu aliyejuu ya Sheria kwanini yeye sheria ya ulipaji kodi haimgusi? Hata marais wa Nchi tajiri wanalipa kodi iweje nchi maskini kama Tanzania Rais halipi kodi au hakatwi kodi kwenye mshahara wake ikiwa kila kitu anahudumiwa na Serikali?
 
Ikitungwa sheria ni lazima atalipa kodi. Lakini kama mnatumia kigezo cha yeye kulipa kodi kwa nia ya kuongea maneno ya kebehi na dharau kama ilivyo kawaida yenu, basi you are just wasting your time.

Watu wengine bana kazi kutetea upuuzi wa wahuni serikalini.
 
Yaani hata kodi halipi na mtu uko comfortable kabisa huku hata indirect tax nayo haikugusu maana kila kitu unagharamiwa na serikali kuanzia chakula,mavazi,n.k.

Wakati baadhi ya nchi tajiri maraisi wao hawataki hata kupokea mshahara ili fedha hizo zitumike kwa maslahi ya Taifa.

Mama ntile analipa kodi ila Raisi wa nchi halipi kodi tena yeye akiwa ndio Raia namba moja!!

Africa hatujitambui haya mambo ni bora yafanywe na nchi zilizoendelea.
Halafu anatudanganya kwamba atatuonyesha salary slip.
 
Naona hujamuelewa mleta mada, kulipa kodi ni muhimu kwa kila raia. Swali linakuja kwanini yeye halipi kodi wakati anahimiza watu walipe kodi? Na Katiba yetu inasema hakuna mtu aliyejuu ya Sheria kwanini yeye sheria ya ulipaji kodi haimgusi? Hata marais wa Nchi tajiri wanalipa kodi iweje nchi maskini kama Tanzania Rais halipi kodi au hakatwi kodi kwenye mshahara wake ikiwa kila kitu anahudumiwa na Serikali?
Hilo lina muda wake wa kujadiliwa, lipelekwe bungeni. Rais hajiamulii mwenyewe kulipa au kutolipa kodi.

Hao wabunge wanaoshindwa kujenga hoja mpaka ikapitishwa kisheria kwamba rais alipe kodi, wanafanya kazi gani ya wao kustahili kulipwa mishahara na marupurupu??.

Vipo vitu vyenye kustahili mjadala endelevu lakini hili ni suala la kisheria na kikatiba. Wakati wake ukifika ni lazima lijadiliwe na kupatiwa ufumbuzi.

Timing ya mleta mada ni mbovu.
 
Swali linakuja kwanini yeye halipi kodi ikiwa kila Mtanzania analipishwa kodi hata wakina mama ntilie wanalipa kodi yeye aliyepangishwa na kile kibabu Lubuva bila ya ridhaa ya watanzania pale magogoni kwanini halipi Kodi? Watanzania tuna haki ya kuhoji bila ya kusubiria bunge. Mshahara wake ndio kodi zetu tuna haki ya kuhoji chochote bila ya kupitia bungeni na hakuna sheria inayosema tusihoji bila ya bunge.
 
Kutolipa kodi kwake mpaka sasa hivi sio mzigo kwenye maisha yangu binafsi na kwa wengi tu ambao wanaguswa kwa wema wa maamuzi anayochukua.

Kutolipa kodi kwake kama kunasababisha watu wapewe haki zao, sioni gharama yoyote kubwa ya kumtunza mtu wa aina hiyo.

Kama anaifungua mikoa kama Kigoma, Lindi na Mtwara, kumtunza yeye na familia yake ni gharama ndogo sana.

Kutolipa kodi ni mzigo mkubwa kama anayetunzwa ana hulka za kujijali yeye na familia yake, kama anazo tabia za kuwatenganisha watu badala ya kuwaunganisha, kama anawagawa watu kwa namna yoyote ile.

Una uhakika ana maamuzi mema? Una uhakika anatoa haki sawa kwa wote? Kufungua hiyo mikoa unayosema hataweza mpaka asilipe kodi? Una uhakika hatengi watu kwenye jamii ya watanzania?
 
Hilo lina muda wake wa kujadiliwa, lipelekwe bungeni. Rais hajiamulii mwenyewe kulipa au kutolipa kodi.

Hao wabunge wanaoshindwa kujenga hoja mpaka ikapitishwa kisheria kwamba rais alipe kodi, wanafanya kazi gani ya wao kustahili kulipwa mishahara na marupurupu??.

Vipo vitu vyenye kustahili mjadala endelevu lakini hili ni suala la kisheria na kikatiba. Wakati wake ukifika ni lazima lijadiliwe na kupatiwa ufumbuzi.

Timing ya mleta mada ni mbovu.

Mkuu unaamini mjadala huo unahitaji tusubiri bunge? Toka lini mijadala huru ikasubiri bunge kisa ni suala la kikariba? Mbona kuna watu wanasema jamaa aongezewe muda wa kukaa madarakani tena mbele na wala hawachukuliwi hatua kwa kutamka kinyume na katiba? Kibaya zaidi wengine ni wabunge na viongozi wastaafu, mbona hao hawasubiri bunge lipitishe? Je bunge linalofanya kazi kumfurahisha rais unategemea litaacha kupitisha muda wa yy kukaa madarakani?
 
Watu wengine bana kazi kutetea upuuzi wa wahuni serikalini.
Mpuuzi ni wewe na mhuni ni wewe ambaye unashindwa kujenga hoja za kueleweka.

Unataka kuniambia huyu wa sasa ndiye rais wa kwanza kutolipa kodi?. Jenga hoja, hizo hasira zako peleka kwa mumeo au mkeo.
 
Swali linakuja kwanini yeye halipi kodi ikiwa kila Mtanzania analipishwa kodi hata wakina mama ntilie wanalipa kodi yeye aliyepangishwa na kile kibabu Lubuva bila ya ridhaa ya watanzania pale magogoni kwanini halipi Kodi? Watanzania tuna haki ya kuhoji bila ya kusubiria bunge. Mshahara wake ndio kodi zetu tuna haki ya kuhoji chochote bila ya kupitia bungeni na hakuna sheria inayosema tusihoji bila ya bunge.
Usichanganye hoja za kishabiki na zile zenye mantiki. Ongea kama mtu ambaye hoja zake zina msaada kwa wanajukwaa wengi.

Unao ushahidi upi kwamba Mzee Lubuva ndiye aliyempangisha rais pale Magogoni?. Mlikuwa mnataka yule mzee wa hotuba za dakika tano ndio aende ikulu?. Mlikuwa mnataka wapigaji wamtumie mzee yule kuifanya nchi hii kuwa ya wachache na wengi wabakie kudhulumiwa na kuonewa?, imekula kwenu mazima.

Kutolipa kodi kwa rais ni sawa sawa na kutoshtakiwa kwake, haya sio mambo ya kuongea yale maongezi ya kwenye bar. Ni mjadala mrefu wenye kuhitaji fikra za watu wengi.
 
Back
Top Bottom