Katika mjadala wa leo bungeni, mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoa wa Geita, Upendo Peneza amlipua Rais Magufuli ya kwamba anapaswa kuonyesha mfano katika kulipa kodi kutoka kwenye mshahara wake ambao kwa sasa haukatwi kodi..
Hali hiyo ilizua taharuki ambapo waziri wa ofisi ya Rais, TAMISEMI Simbachawene aliinuka na kuomba kutoa taarifa. Katika kutoa kwake taarifa waziri alisema mshahara wa Rais haujadiliwi popote pale, ikiwa ni sharti ndani ya katiba ibara ya 43.
Mbunge Peneza katika kukataa taarifa hiyo alisema hoja yake ya msingi ni kutaka Rais aonyeshe kuongoza kwa mfano kwa kulipa kodi kama anavyosisitiza wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi.