Upendo haumo katika maneno

Upendo haumo katika maneno

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini wadau marafiki


Ninaoposema kuwa Upendo haumo katika maneno bali ni vitendo
ni kitu ninachomaanisha hapa kwani tumeona wengi wakisema bila
kutenda wala kuonesha kile wakisemacho kwa udhahili kabisa

Upendo ule wa kweli husukumwa na vitendo ambavyo hutoka ndani
ya moyo wa mtu, si wa kulazimisha bali ni wa kutenda kwa kupenda
bila unafiki, wala kujionesha mbele za watu, au kujifanya unazo bali
ni pale ambapo umeguswa na yule umpendaye na kuonesha hisia zako
kwake kuwa unamjali , mpenda, na kumthamini pia

Marafiki kwanini nimegusia jambo hili hapa na kwanini nimeamua
kuwashirikisha kitu hichi yaani upendo, nasi twatambua kuwa
upendo hutoka kwa Mungu kwani yeye ni upendo. hebu soma:
1 Yohana 4:16"Mungu ni upendo, naye akaaye
katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu
hukaa ndani yake".


Na kipengele hichi pia:
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo;
kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda
Mungu ambaye hakumwona.

Kwa hiyo marafiki zangu nimependa kuwashirikisha jambo hili kwenu
yote ni kuwaambia kuwa tuna marafiki wenzetu hapa mjengoni ambao
waliwapoteza wazazi wao na ndugu zao wa karibu sana wako marafiki
wengine ambao walishikamana nao katika kipindi chote cha msiba hiyo
iliyotokea hivi karibuni tukaletewa bandiko hapa, na wako wengine walishindwa
kutokana na umbali au kutopata taarifa mapema. Hivyo marafiki ningependa
tujumuike pia kuwa karibu nao ndugu zetu marafiki zetu hawa kuwatia moyo
kuwapigia na kuwa karibu nao kwani wao ni sisi na nsisi ni wao
Tuwakumbuke katika maombi hawa wafuatao: Money Stunna aliyempoteza mzazi
wake, Mr Rocky naye aliyempoteza baba yake pindi warudipo jukwaani msisite
kuwafariji na kuwapigia kama ikiwezekana kufanya kitu kwao kwani tu marafiki
kama kuna wengine niliowasahau waliowapoteza ndugu zao msisite kunijuza


TUONESHE MOYO WA UPENDO WA AGAPE AMBAO MUNGU ALITUPENDA SISI
NASI TUONESHE HUO UPENDO KWA WENGINE BILA UNAFIKI.
KWANI UPENDO HAUMO KATIKA MANENO BALI NI VITENDO

CC: BAK NJOO UWEKE WIMBO WA AMBWENE : UPENDO

 
Last edited by a moderator:
Haya Best, BAK alipita hapa kutimiza ombi lako.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom