Upelelezi wabainisha Khashoghi ameuliwa na Saudia Arabia

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,692
Upelelezi Nchini Uturuki wabainisha kuwa Mwandishi wa Habari Mr. Jamal Khashoggi aliuliwa baada ya kuhojiwa, alipoingia Ubalozi wa Saudia Arabia kisha mwili wake ukakatwa mapande !!

Kwa hisani ya Rasi Ngimbwa....

My take:
Hii inamaanisha saudi arabia imemuua mwanahabari huyo aliyekuwa amekimbilia nchini uturuki akihofia maisha yake kutokana na kuingia kwenye mzozo na serikali ya saudi Arabia.. mr Jamal alikuwa mkosoaji kubwa wa sera za mambo ya nje za serikali ya saudi Arabia hasa mauaji ya raia yanayofanywa na ndege vita za saudi arabia huko yemen..

Mwanahabari huyu alikuwa katika harakati za kuoa na alienda na mchumba wake katika ubalozi wa saudi arabia ili apate clearance form ambayo zitaonyesha kuwa ana vigenzo na anastahili kufunga ndoa..

Mr Jamal alienda na mchumba wake ubalozini ila akamwacha nje ya ubalozi nae akaingia ndani,mchumba wake alipoona mume wake mtarajiwa amechelewa kutoka ndipo akatoa taarifa polisi na hali hiyo ikaamsha mgogoro mpya wa diplomasia kati ya uturuki na saudi Arabia...

Uturuki inasema ina ushahidi kuwa maafisa wa ubalozi huo wakimtesa na kumuua bw khashoggi pamoja na kumkakata vipande na kuundoa mwili wake toka ubalozini ndani ya mabegi maalum.. uturuki inasema Mr Jamal alivaa saa maalumu iliyokuwa imeunganishwa na simu yake aliyoiacha ndani ya gari na ikawa inarekodi video zote ndani ya ubalozi wa saudi arabia katika kile alichokuwa anatendewa...

Duru za kijasusi ndani ya uturuki zinasema siku ya tukio maafisa wa kidiplomasia 15 wa saudi waliwasili uturuki na ndege maalumu na waliondoka na mizigo maalumu ambayo hata hivyo haikukaguliwa airport coz begi za kidiplomasia uwa hazifanyiwi ukaguzi.. uturuki inaamini maafisa hao 15 walitumika kuuondoa mwili wa Mr Jamal toka uturuki hadi saudi arabia ndani ya viroba..

Marekani imeapa itaiadhibu kwa vikwazo saudi arabia iwapo itagundulika imemuua mwanahabari huyo, nayo saudi arabia imeapa kulipiza kisasi iwapo itawekewa vikwazo na marekani au NATO..

Wadau wengi wana wasiwasi kama marekani inaweza kuiadhibi Saudi Arabia ukichulia saudi Arabia ni mteja mkubwa wa silaha za marekani hasa ndege vita na mitambo ya ulinzi wa anga..

Marekani pia ina kambi kubwa ya kijeshi pale Saudi Arabia ikilinda maslahi yake ya mafuta..

Na Hillary A Silayo.......
 
Mbona wala hata hatujaomba picha mzee baba?au umeamua kuniharibia asubuhi yangu?
 
Inabidi Sheria za diplomacy and consular relationship ziangaliwe upya.
Itakuwa ngumu sana baadhi ya sheria kubadilishwa hasa ibara ya 22 na 24 ya mkataba wa viena convention of diplomatic relations.

Ibara hizi 22&24 inapinga na kukataza maafisa uchunguzi wa nchi mwenyeji kuingia kwenye balozi na makazi pamoja na kukagua diplomatic bags.

Hii ni kutokana pamoja na kazi za ubalozi kuwa ni za kiuwakilishi lakini kwa asilimia nyingi kazi za kibalozi ni kazi za kijasusi taifa moja kuchunguza nyendo za taifa lingine na ndio msingi wa kazi hizi za kibalozi.

Itakuwa ngumu sana kuondoa vifungu hivi kwa kuwa vinawafaidisha wakubwa zaidi.
 
Inabidi Sheria za diplomacy and consular relationship ziangaliwe upya.
Kazi bure hii mijitu myeupe inajijua yenyewe walahi
Wanakutungia sheria ambazo wao wenyewe hawazifuati walahi
Dawa ni kutatua matatizo nchini kwako walahi
Usa na Saudia ni pete na kidole, usa kachacha maana mrusi anakuja juu, mchina naye usiseme walahi
Khashoggi ni marehemu, choose your battles wisely walahi
Nachagua kuishi walahi
BOB WINE ANA AKILI WALAHI
 
So sad kwakweli '' Raia wa saudia na wa tz nao ni baba mmoja Mama mmoja Aisee ... Yaani jinsi mwenzao alivyo fanyiwa unyama wa kiasi hicho wameshindwa hata Kuandamana "... pumbavu sana



nashangaa Mungu wa ardhi TAKATIFU. na yeye ametulia tu ".. (hizi imani nyingine hizi)
 
Technology imesogea sana na hapa ndipo utakapoona umbumbumbu wa waarabu,yaani walishindwa kujiuliza kwamba huyu jamaa wana ugomvi nae na vyovyote iwavyo lazima amejiwekea ulinzi wake binafsi?
 
Tusubiri sauti ya umoja wa Ulaya, vinginevyo Marekani haina msaada hapa
 
Trump anajikanganya katika hili. Anataka kuwaadabisha KSA lakini pia anataka biashara ya madege yake ya kivita yenye thamani ya mabilioni ya dola isipotee. Kwa vile alishaapa American First, hana ujanja. Keshasema Mfalme hakushiriki na wala hana taarifa ya uhalifu huo. Kwamba wauaji ni "rogue people". Lingekuwa Taifa jingine tayari angeshapeleka madege yake kulifunza adabu. Hapo KSA kagonga mwamba.
 
Back
Top Bottom