Updates za Corona Tanzania

Kinachonisikitisha zaidi ni pale wanaposisitiza watu kutokushikana mikono lakini wanaongea na ku badilishana hewa na ugonjwa unaambukizwa sana kwa njia ya hewa.


Bagwell
 
Mi nadhani serikali iko sahihi kwa hatua inazozichukua. Inawezakuonekana na wengi(wajuaji) kuwa juhudi hazitoshi lakini kwa jicho la tatu na logic tu za kawaida ikawa tuko kwenye njia sahihi.. Tukumbuke huu ugonjwa haujathibitika kuwa upo Tanzania so serikali ikisema ifanyie kazi ushauri kama unavotolewa na wapiga ramli ambao nao tu ni wanasiasa kwa nature ya mawazo yao then tunacreate panic.

Ukishatengeneza panic then tutajikuta athari zimekuwa fatal kuliko ugonjwa wenyewe.. Nadhani screening ya uhakika airport, bandarini na mipakani inatosha kuhakikisha hamna atakaetoka nao nje akauingiza nchini. Hatua unazopendekeza ni radical mno na kama serikali itazifuata matokeo ni kusimama kwa kila kitu hence paralyzed economy kwa sababu watu hawatatoka kutafuta, wanunuzi hawatatoka kutafuta mahitaji na wauzaji hawatafungua biashara, daladala zitapaki nk.

Hivyo tutajikuta tumeua uchumi kwa kufuata ushauri wa wachawi na wenye maslahi ya kisiasa kwa sababu kwa wanasiasa wa kwetu ugonjwa ukiwepo ni mtaji kwenu ila pia uchumi ukianguka kwenu ni mtaji pia.. Naendelea kuamini serikali iko makini kwenye haya mambo kama unabisha ingia nchi ambayo iko declared kuwa na Ebola au homa ya manjano halafu kavuke border uingie Tz..

Kuna screening pale boda na joto likizidi unabaki pale na hata hawa walioko poa mkifika mkoa mnakoenda mnakuwa scanned tena kabla ya kushuka kwenye basi.. So serikali inafanya kazi tuwaachie hili sisi tuendelee na udalali na misheni town zetu
 
Wala hakuna watazamani kuingia uwanjani
Jr
 
Kwanamna viongozi wetu wasivyo serious huu ugonjwa utafika bila shaka nchini,jana tu kuna wachina wamekuja toka China na kupita bila shida pale airport bila kuangaliwa hata kwa siku moja direct wakaja na kuendelea na kilichowaleta,Tz hii hatari inakuja maana tunatamaa sana,wengine tunaita watalii,kuna nchi west africa waitaly waliingia kwa tiketi ya utalii wakatudishwa kwao baada ya kugundulika wanakimbia ugonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…