Updates: Waliofariki Ajali MV Nyerere Wafika 196

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 196, miili 60 imeopolewa kwa leo hadi muda huu na uokoaji bado unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018 na kwamba vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na inatarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.

“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.
 
Uwe una update uzi wako, takwimu leo zinasema 218
 
Hivi huoni hata ' aibu ' kuja na ' figure ' tofauti kabisa hii wakati wenzako sasa wanausaka mwili wa 219 pamoja na mingine ambayo bado inashukiwa kuwa ipo ila imenasa?
 
Mungu awarehem marehem na awape faraja ndugu wote walioondokewa na wapenzi wao.kuna video nilikuwa naiangalia jinsi watu wanavyotolewa mle majini wakiwa wafu nimesikitika sana!

Kifo ni fumbo tulio hai tujifunze kujiandaa,sometimes atakaefuata baada ya wale ni mimi au wewe hakuna ajuae!
RIP
 
Inamaana hiyo. Meli ilikuwa imebeba abilia wangapi?
Ina uwezo wa kubeba watu 105/110 na mizigo 25 tons wao waka overload idadi waliyoitaka wao,na ilikuwa siku ya soko unaweza kuona hatari iliyopo hapo.

Ni balaa kubwa zaidi ya laana!
 
Back
Top Bottom