Mwl. Kaijage
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 216
- 214
Chama cha ACT-WAZALENDO kinafanya Mkutano mjini Iringa. Maandalizi yote ya Mkutano yamekamilika na asubuhi hii ni ufunguzi wa matawi ya chama katika mji wa makambako na maeneo mengine.
Mwami Zitto amewaambia wananchi wa Mafinga kuwa Msinmamo wa chama cha ACT-WAZALENDO ni kusimama na wanyonge. Wakikuta mnyonge mwenzao anapigwa wanamsaidia mnyonge mwenzao. Na Hui ndio msimamo wao wa kusaidiana na wanyonge ktk taifa lao.
Tutawaletea kitakachojiri pamoja na picha na Viongozi wa chama cha ACT-WAZALENDO Leo wameanza na mkutano mkubwa ktk wilaya ya mafinga ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kuwasikiliza wazalendo ambao wameongozwa na kiongozi wa chama Ndugu Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa chama Taifa Mama Anna Maghwira matukio mengine.
Zitto KABWE amesema chama cha ACT-WAZALENDO hakijaanzishwa ili kupambana na mtu bali kimeanzishwa kwa ajili ya kupambana na mfumo mbaya wa chama cha Mapinduzi ili kuwasaidia watanzania kuondokana na mfumo wa CCM unaowakandamiza wanyonge.
ZITTO amezidi kueleza kuwa chama cha ACT-WAZALENDO kinaongozwa na misingi hivyo wanataka kuirudisha nchi ktk misingi yake ya Ujamaa ambapo watu walijivunia kuishi ktk taifa lao, wazee wetu walikwenda kununua vitu katika maduka ya ushirika, viongozi waliwajibika kwa wananchi tofauti na sasa ambapo viongozi wa leo wanawajibika kwa kula rushwa na ufisadi uliokithiri ktk taifa, hivyo chama cha ACT-WAZALENDO kitairudisha nchi ktk misingi yake ili Mwananchi ajivunie kuwa Mtanzania.

![]()
![]()
![]()
Kazi ya kuendelea kukijenga chama cha ACT Inaendelea
ACT WAZALENDO