Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

WAZIRI wa sera na uratibu wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jenista Mhagama amepita bila kupingwa kwa sasabu wakati wa mchakato wa kuchukua fomu za kuomba uongozi ndani ya chama wagombea wenzake wawili waliojitokeza kuwania nafasi hiyo mmoja fomu ilisahiniwa na mtu mwingine ambaye si mgombea na mwingine siku moja kabla ya kuanza kampeni alianguka ghafla chooni wakati akijisaidia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katibu chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea Vijijini Rajab Huonde aliwataja wagombea ambao walishindwa kuingilia kwenye kinyanganyiri hicho kuwa ni Lazaro Komba Bunungu mfanyakazi wa Tanroads mkoa wa Tanga , pamoja na Clement Makaburi Mwinuka mkazi wa Magagula .

Alifafanua kuwa, sababu zilizomfanya bunungu kushindwa kugombea nafasi hiyo ni kwamba baada ya kupata ajali hiyo hakuweza kuleta taarifa yoyote juu ya maendeleo ya ugonjwa wake hadi kampeni zilipokwisha ,na mwinuka fomu yake ya kuomba uongozi ndani ya chama haikusainiwa na mgombea mwenyewe.

Alisema kuwa jimbo la peramiho ambalo linakata 17 wanachama wameridhia kumpitisha Jenista Mhagama kutokana na wagombea wengine kutoonekana siku ya uchaguzi .

Wakati huo huo Mkurugenzi shirika lisilo la kiserikali RUCCODIA Joseph Mhagama amewabwaga makada wenzake nane baada ya kupata kura 5081 ,akifatiwa na profesa Elieuther Mwageni makamu mkuu wa chuo cha Ardhi wa fedha na utawala jijini Dar es salaam aliyepata kura 993, wengine ni Mkuu wa wilaya ya Tarime Glolius Luoga (838), mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya uhamiaji nchini Kinemo kihanamo (734),mkuu wa shule ya sekondari ya kutwa London manispaa ya Songea Christopher Mwageni (200) Limo Mwageni mwalimu shule ya sekondari mpanda (84)

Huonde alifafanua kuwa, wagombea wengine wawili ambao ni Tasilo Mahuwi na Venance Mgaya siku ya mwisho waliamua kujitoa kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi wakati pius mwageni fomu yake ya kuomba uongozi baadaye ilibainika kuwa haikusainiwa na mgombea mwenyewe hivyo ilimfanya akose sifa ya kugombea nafasi hiyo.

Na Stephano Mango, Songea
 
Asubiri Ngoma inogile kutoka Ukawa chini ya Fundi wa siasa za Tanzania Kamanda Lowassa


Kwa kule kwake yeye ni mbunge anayesubiri kuapishwa.

Jimbo ambalo UKAWA wanalitegemea ni hili la Songea Mjini.

Kule Tunduru CUF ina nguvu kimtindo.

UKAWA wanaweza kushinda kule
 
UCHAGUZI wa kura za maoni nafasi ya ubunge na madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma umemalizika kwa matokeo ya awali, mkuu wa mkoa wa Kirimanjaro Leonidas Gama amewabwaga makada wenzake 7 kwa kupata kura 6287 wakati aliyekuwa waziri wa mazingira Dokta Thereza Uviza amepata kura 5600.

Katibu wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Songe mjini Juma Mpeli akizungumza na waandishi wa habari jana asubuhi ofisini kwake aliwataja makada wengine waliokuwa wanawania nafasi hiyo ambao kura zao hazikutosha kuwa ni meneja mwandamizi wa mitandao wa benki ya biashara ya China iliyopo jijini Dar-es-salaam Mussa Gama mtoto wa marehemu Dk Raulence Gama alipata kura 1278,wengine ni katibu wa CCM wa wilaya ya Namtumbo Azizi Mohamedi Fakiri alipata kura 1101,Erick Mapunda mhadhiri wa chuo kikuu cha sayansi na teknorojia Mbeya alipata kura 908.

Mpeli aliwataja wengine kuwa meneja masoko wa Claus FM Radio na TV ya jijini Dar-es-salaam Raymond Mhenga amepata kura 576 wakati mkuu wa wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara Francis Miti alipata kura 475 na mwanasheria wakiri wa kujitegemea manispaa ya Songea Sebastian Waliyuba alipata kura 265.

Alifafanua zaidi kuwa wilaya ya Songea mjini inawanachama waliojiandikisha kwenye kitabu cha orodha ya wanachama wa CCM ni 34,800 lakini wanachama waliojitokeza kupiga kura za maoni ni 17,226.

Wakati huohuo katika kituo cha kupigia kura eneo la Mwembechai kata ya Matarawe vilijitokeza vituko vilivyoonekana sio vya kawaida ambavyo vinasadikiwa kuwa ni vya ushirikina ambapo madawa yanayodaiwa kuwa ya kienyeji yalionekana yamemwagwa chini ya mlango wa chumba cha kupigia kura na radi ilipiga majira ya saa za mchana huku jua kali likiwa linawaka na kusababisha tafrani kubwa kwa wapiga kura.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo Jafari Nindi(Ukuta) amesema kuwa majira ya saa 11 arfajiri katika kituo hicho wapiga kura waliowahi walikuta dawa ya mitishamba imemwagwa katika mlango wa chumba cha kupigia kura.

Na, Stephano Mango, Songea
 
Kupitia hali ya sintofahamu Uvccm Mara wazichapa ngumi mara baada ya kupitishwa mgombea ambaye inasemekana sio mkazi wa Mara ajulikanaye kwa jina la Juliana Masaburi.Hivyo wagombea wengine inasemekana hawakuridhishwa kupita kwa jina la Juliana Masaburi jambo lililopelekea kurushiana ngumi wao kwa wao.

Mwaka mgumu sana kwa CCM.

Chanzo:Habari za saa ITV
 
Hakuna anayesema nimeshindwa kwa sababu nilikua nimeahidi kuwaongoza vizuri na kuwasaidia nikakosea kwenda kushinda kwenye mahotel mazuri mjini huku wao wakiwa hawana hata maji
 
Anapoteza muda hilo jimbo ni la Ukawa,hata akitumia dawa za Maji Marefu, safari hii atajuta kuachia ukuu wa mkoa,amulize Nchimbi moto wa Chadema hapo.
 

Attachments

  • attachment-10.jpeg
    attachment-10.jpeg
    9.5 KB · Views: 1,044
Kumbafu.
Umeshindwa kuipeleka kwenye special thread ya matokeo kule?
 
KUFUATIA vuguvugu la kisiasa ambalo limeendelea kushika kasi na kutishia hali ya amani katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, kutokana na wananchi kuutaka uongozi husika wa chama hicho wilayani humo utangaze matokeo ya nafasi ya ubunge uchaguzi kura za maoni, hatimaye matokeo hayo yalitangazwa kwa jimbo la Mbinga vijijini majira ya saa 5:45 usiku.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo kwa jimbo hilo, kulikuwa na mvutano mkali ambao ulidumu kwa masaa 12, kutokana na kati ya wagombea nane waliokuwa katika kinyang'anyiro hicho, mgombea Gaudence Kayombo kudaiwa kufanya mchezo mchafu wa kutaka kuchakachua matokeo kwa kata ya Ruanda na Kihangimahuka, ili yaweze kumpatia ushindi baada ya kuona hali ya upepo wa ushindi kwa upande wake inamwendea vibaya.

Aidha kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi wilayani humo lililazimika askari wake kuweka ulinzi mkali katika eneo la ofisi hizo za CCM, kutokana na baadhi ya wanachama kuleta vurugu huku wengine wakirusha mawe.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho waliendelea kuandamana maeneo mbalimbali ya mji wa Mbinga, wakitishia kutoondoka katika maeneo ya ofisi za CCM na kuonekana kuranda randa huku wakiimba nyimbo mbalimbali na kutamka maneno "hapa mpaka kieleweke, tunachotaka ni matokeo na sio vinginevyo".

Sinto fahamu iliendelea kutawala katika eneo la ofisi za CCM wilaya ya Mbinga ambapo wanachama wa chama hicho walionekana kuendelea kujawa jazba na kuutaka uongozi husika utangaze matokeo ya nafasi hiyo ya ubunge, kutokana kucheleweshwa kutangazwa.

"Tunataka matokeo, tunataka matokeo, tunataka matokeo hapa mkitaka amani tuleeteeni matokeo vinginevyo tunarudisha kadi za CCM hatukitaki chama tunataka haki itendeke kwa mshindi aliyeshinda", hayo ni maneno ambayo yalikuwa yakitawala katika eneo la ofisi kuu za chama hicho wilayani humo ambayo yalikuwa yakitamkwa na wanachama wa chama hicho.

Kadhalika licha ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho kujitokeza mbele ya hadhira hiyo ambayo ilionekana kudai matokeo hayo katika viwanja vya chama hicho, bado wanachama walionekana kujawa jazba wakitamka maneno ya kutaka matokeo yatangazwe na wengine wakiendelea kutamka hawawezi kuondoka mpaka kieleweke.

"Ndugu zangu tulizeni jazba, lazima tufuate utaratibu wa chama, hatuwezi kuendesha chama kwa mashinikizo", alisikika akisema Shumbusho mbele ya umati huo uliokuwa kwenye viwanja vya CCM mjini hapa.

Baadhi ya wanachama waliendelea wakisema, wanamashaka na viongozi wa wilaya hiyo wakiwemo chama na serikali, huenda wanapanga mpango wa kutaka kuyachakachua matokeo ili atangazwe mgombea ambaye sio chaguo sahihi la wananchi.
Waandishi wa habari ambao walikuwa wakishuhudia juu ya sakata hilo na kumtaka Katibu wa wilaya hiyo, Zainabu Chinowa azungumzie juu ya hali hiyo alisema kuwa mpaka sasa wanashindwa kutangaza matokeo kutokana na jimbo hilo la Mbinga vijijini katika kata ya Ruanda na Kihangimahuka, kuwepo kwa utata juu ya matokeo ya nafasi ya ubunge.

"Ndugu zangu waandishi wa habari chama kimetuma magari huko Kihangimahuka na Ruanda kufuatilia juu ya suala hili, kwa sababu matokeo yanaleta utata kidogo, hivyo yakiletwa na chama kujiridhisha juu ya jambo hili tutayatangaza muda wowote hata kama itakuwa ni usiku nawaomba wananchi waache jazba wakati tunaendelea na mchakato huu", alisema Chinowa.

Kadhalika baada ya kukamilika kwa taratibu husika za chama ndipo matokeo kwa nafasi ya ubunge wa jimbo la Mbinga vijijini yalitangazwa Agosti 3 mwaka huu majira ya saa 5:45 usiku ambapo, Martin Msuha aliweza kuchukua nafasi ya ushindi katika jimbo hilo kwa kupata kura 13,354 na kuwagaragaza chini wagombea wenzake saba, waliokuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho.

Wagombea wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na kura walizopata katika mabano kuwa ni; Humprey Kisika (545), Dokta Silverius Komba (1,289), Edesius Kinunda (2,355), Deodatus Mapunda (2,532), Benaya Kapinga (3,941), Deodatus Ndunguru (7,060) na Gaudence Kayombo aliyepata kura 12,068.

Pamoja na mambo mengine, wilaya ya Mbinga ambayo ina majimbo mawili ya uchaguzi Mbinga mjini na vijijini ambapo kwa upande wa jimbo hilo la mjini matokeo yake kwa nafasi ya ubunge yanatarajiwa kutangazwa leo majira ya jioni, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo ambao unaendelea katika kata ya Kikolo na Uzena zilizopo wilayani humo.

NA STEPHANO MANGO, MBINGA
 
Back
Top Bottom