Updates kesi ya uhaini Part1

Updates kesi ya uhaini Part1

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,883
Reaction score
828,458
Sasa tunaingia kwenye kesi ya pili ya Uhaini

Hakimu anaingia ile sauti ya askari courtttttttttt inasikika

Watu wote wanasimama, Hakimu anaketi then kila mtu anaketi.

Anasimama Karani wa Mahakama anasoma kesi namba PI no. 8607/2025 Rvs Tundu Lissu

Hakimu wa kesi hii anaitwa Mh. Kiswaga. Anawaita upande wa Jamhuri.

Kama kawaida upande wa Jamhuri hawajibu. Anawauliza mnanisikia? Mara ya nne anawaita. Kimya ni kikubwa hapa mahakamani. Hakimu anawaita hawaitiki. Mawakili wa utetezi wameshifika vitabu vya sheria kila mmoja anasoma sijui hata wanajiandaa na jambo gani ila wako bize sana. Kimya bado ni kikubwa jamhuri hawajibu. Tunawaona lakini kwenye screen wamekaaa tu.

Hakimu amewaita mara ya 10 sasa hivi. Ningekuwa mimi Hakimu hawa jamhuri ningesema waende jela hata week mbili ndio waje kuendesha hii kesi. Wana viburi jamani. 😂 sasa hivi simu inaita huko kwa upande wa jamhuri ni kama wanapiga simu

Wanakaribishwa jamhuri tena endeleeeni.

Wamefika sasa wanasema wanasikia. Anasubiriwa Wakili wa Jamhuri anajitambulisha Anaitwa Job Mrema, yuko Nasoro Katuga, Issa Tawabu hao ni mawakili wa serikali waandamizi pamoja na Cathbert Mbilingi wakili wa serikali.

Kwa niaba ya jamhuri tuko wakili hao ambao nimewatambulisha na upande wa utetezi naomba wajitanbulishe.

Upande wa Utetezi anaanza kujitambulisha Wakili Msomi-;

1. Mzee Mpale Mpoki
2. Adv. Alute Mungwai
3. Adv. Dr. Ruge Nshala Mwansjeria mkuu wa chama
4. Peter Kibatala
5. Jeremiah Mtobesya
6. Nashon Nkungu
7. Gaston Garubindi
8. Deus Singa
9. Elben elias Silayo
10. Deogratias Mahinyila
11. Edson Kilatu
12. Cathbert Albert Bandiho
13. Divkson Matata
14. Emanuel Chengula
15. Paul Kisabo
16. Edward Heche
17. Jebra Kambole
18. Maria Mushi
19. Sisty Masawe
20. Ikoti Lissu
21. Fredrick Kihwelo
22. Michael Mwangasa
23. Fredrick Msaki
24. Jacob Mugendi
25. Fikiri Gabriel
26. Florian Francis
27. Hekima Mwasipu
28. Emmanuel Ukashu
29. Ferdinand Makore
30. Matthias Mlimi
31. Matojo Cosotta

We have an observer senior counsel martha Karua from East African Law Society and John Seka.

Hao ni Mawakili wa Lissu jamani. 😂😂 hilo jopo hadi mimi nafurahi kwakweli. Amemaliza kutambulisha. Na Mawakili pia wamependeza wote wamekula suti kali sana. Kuna raha mtu kupendeza halafu ukawa na akili.

Haya tuendeleee wanaitwa mawakili wa serikali, anaanza Job Mrema kuwa shauri hili linakuja kutajwa leo. Lakini mshitakiwa nikiangalia kwenye picha ya mahakama simuoni. Kupitia huu mtandao.

Hakimu anasema kwahiyo unasemaje? Hakimu anasema mara ya mwisho mara ya mwisho alienda magereza.

Wakili wa serikali anasema mtuhumiwa simuoni labda amekaa wapi sijui? Hakimu anawauliza magereza mtuhumiwa yuko wapi? Afisa wa magereza anaulizwa anaongea hapa kuwa mtuhumiwa amekataaa kuhudhuria kesi yake kwa njia ya mtandao.

Hakimu anawauliza jamhuri mnasemaje? Huyu Job Mrema anasema shauri lilikuja kwa kutajwa na tunaomba kuifahamisha mahakama kuwa upelelezi haujakamilika.

Lakini pia mheshimiwa kutokana na taarifa kutoka magereza kuwa mshitakiwa amekataa kusikiliza kwa njia ya video. Basi tunaomba mahakama iweze kutoa amri kwa mshitakiwa aweze kufika mbele ya mahakama hii. Watu wanacheka 😂😂😂 anasema afike kwa njia ya mtandao tunaomba mahakama itupatie tarehe nyingine na mshitakiwa afike.

Na kwa msingi huo kwasbabau upelelezi bado tunaomba ahirisho kwa tarehe nyingine ikizingatiwa kwamba mshitakiwa hana dhamana kwenye shauri hili linalomkabili kwenye mahakama hii. Ni hayo tu anamaliza huyu Bwana Job Mrema Ni mrefu na ana kipara pia kwa kumuangalia kwenye screen kama Cha John Mrema msemaji wa Tume na #Njaa55

Upande wa Jamhuri wamemaliza sasa wanaingia upande wa Utetezi

Part 2 Itaendelea!…….

UPDATES PART2

Wanaingia upande wa utetezi

Anaanza Wakili @MpaleMpoki, kama kawaida anaongea kingereza anasema tuna mambo matano. Na watakaoyawasilisha ni mimi, Mtobesya, Kibatala, Dr. Nshala na Mzee Alute Mugwai hao ndio Mawakili upande wetu watakaosema hapa.

Anaingia Mtobesya kuhusu Juridsction (Mamlaka ya Mahakama) na kwa mujibu wa CPA kifungu cha 248 kinasema yapo masharti ya kuahirisha kesi. Mtu hawezi kuja mahakamani hasemi tu naahirisha kesi. Lazima awe na sababu.

Wakili wa serikali akisema tu upelelezi haujakamilika. Anaishia hapo. Ni kugeuza mahakama eneo la mchezomchezo. Alipaswa kwenda mbali zaidi kujibu swali la kwanini upelelelezi haujakamilika au kuna shida gani? Hili kosa analoshitakiwa nae mteja wetu ni UHAINI na wanasema alifanya kosa hilo kwa kupitia kuwatisha na kusema maneno ya vitisho.

Huo ni kwa mujibu wa hati yao wenyewe waliyolileta mahakamani. Sasa kama mashitaka yanasema alisema maneno ya vitisho na mtuhumiwa yupo mahabusu

Anaendelea kuwa sasa kama tuhuma ni maneno aliyosema na maneno yenyewe yapo kwenye hati ya mashitaka. Sasa wanachopeleleza ni kipi sasaa? Maneno yapo wanayo na yapo kwenye hati ya mashitaka. Kupoteza muda wa mahakama kuwa upelelezi haujakamilika hiki bila kuwavunjia heshima mimi naona na hata wenzangu watakubaliana na mimi kuwa ni kituko. Na mahakama isikubali kuahirisha kesi hii kwa sababu.

Mtobesya anaendelea kusema kuwa upo uamuzi wa mahakama kati ya R VS Deeman TLR 980 ukisoma ukurasa wa 116 na 117 mahakama kuu ilisema katika kesi hiyo: anaongezea kuwa mahakama kuu ilikuwa inaquote kesi nyingine ya mahakama ya rufaa.

Anaendelea kutema madini Mtobesya. Anaongea taratibu. Anaonekana mpole lakini maneno yake yanachoma sana huyu Mtobesya. Unaelewa hata kama usipokuwa Wakili kama mimi.

Ukisoma uamuzi wa kesi hiyo niliyotaja mahakama ilisema kwa kifupi mashauri hayapaswi kuahirishwa kiholela tu na ikitokea sababu zisizo za maana kuahirisha kesi mahakama ikatae sababu hizo na kumuachia mtuhumiwa. Kuendelea kumshikilia ni kuvunja haki zake za kikatiba. Ana haki ya kuwa huru.

Kwa mujibu wa S. 248 ya CPA tunaomba mahakama itoe amri ambazo zitahakikisha mtuhumiwa atakuwa anapatiwa haki zake hadi kesi yake itakapoisha. Sasa hoja ya mahakama kusema aendeleee kuwa mikononi mwa magereza lakini ni muhimu pia mahakama ikakumbuka kuhakikisha kuwa haki za mtuhumiwa ziko chini ya mahakama. Naomba kumkaribisha Mwenzangu nimemaliza mimi.

Anaingia Mzee Mpale Mpoki, Senior Advocate. Nae Kingereza kingi utadhani kazaliwa kwa Malkia Elizabeth

Mheshimiwa Hakimu anawauliza Jamhuri mnasikia.

Wanasema we hear watu wanacheka. 😂

Mpale Mpoki anasema sisi tunaomba shauri hili kusikilizwa katika mahakama ya wazi ili kweli haki ionekane ikitendeka. Haya mambo ya kuendesha shauri kama tunauza bangi sio haki. Hivyo ibara ya 13(6)(a) ya Katiba yetu inataka fair hearing katika mashauri haya. Na hiyo inajumuisha kesi kusikilizwa wazi na pia S. 186 ya CPA nayo pia inasisitiza hilo kuhusu mahakama kuwa ya wazi na watu kuruhusiwa kuhudhuria kesi hiyo na umma wote kufuatilia bila kizuia.

Na kama kuna sababu nyingine ambayo itasababisha isiwe hivyo basi mahakama ndio itaamua umma utakaoshiriki katika kesi hiyo uwe wa watu wangapi ma kwasababu zipi. Kifupi mahakama ndio itaandaa utaratibu wa kesi kusikilizwa na iwe katika mahakama ya wazi.

Huyo ni Adv. Mpale Mpoki anatema hizo nondo na kusema International Ciovenant on civil and political right ICCPR tumeridhia kama taifa inasema kuwa watu wote watakuwa na uhuru wa kusikilizwa kwa haki na kwa uwazi katika mashauri kama haya ya jinai. Sisi kama nchi tumeridhia mkataba huu wa kimataifa. Umekuwa ratified na taifa letu kwahiyo tunalazimika kufuata..

Part 3 itaendelea page inayofuata!….

1745514525803.jpg
 
Huyu hakimu hatari sana, anafunga wahalifu sijawahi kuona.... Jamaa atafungwa sio miaka tu, hata kamba
 
Back
Top Bottom