Update za pilika zangu za kuhitaji mkopo

Update za pilika zangu za kuhitaji mkopo

makua

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2013
Posts
208
Reaction score
40
Katika pilikapilika zangu za kutafuta mtaji wa pesa kwa ajili ya kufanyia biashara, nimeenda katika taasisi fulani ya kifedha na wakanipa vigezo vyao kuwa inabidi niwe na TIN namba ya biashara na leseni ya biashara hapo ndipo nitafikiriwa kupewa mkopo (mean hupati mkopo hadi uwe na biashara)

Kwakuwa kunabidhaa nilisha tengeneza na shida nipate frem ili niuze bidhaa zangu, nikaamua niende TRA kwaajili ya kupata hiyo TIN, wakanipa fomu ili nijaze, na sasa nisha kamilisha kujaza, kesho tar 6/march inabidi nikachukue TIN

Shida itakuwa kupata leseni kwani nimeambiwa inagharim kama laki 2 wakati hapanilipo nina elfu tano tu ya kula, sijui itakuwaje...

Naombeni Ushauri na mawazo yenu wadau kwani naamini SIWEZI BILA NYIE.
 
Na siku unaenda tena bank watakuambia biashara yako i run kwa miezi 6 na waone mzunguko wako!mkopo wa biashara ndogo wala sikushauri itakuwa unawafnyia kazi bank.Bora crdb waweza pata 100m ulipe kwa miaka 5 ila uwe na hati ya nyumba.100m unaweza zalisha kitu
 
Katika pilikapilika zangu za kutafuta mtaji wa pesa kwa ajili ya kufanyia biashara,nimeenda katika taasisi fulani ya kifedha na wakanipa vigezo vyao kuwa inabidi niwe na TIN namba ya biashara na leseni ya biashara hapo ndipo nitafikiriwa kupewa mkopo (mean hupati mkopo hadi uwe na biashara)

Kwakuwa kunabidhaa nilisha tengeneza na shida nipate frem ili niuze bidhaa zangu, nikaamua niende TRA kwaajili ya kupata hiyo TIN,wakanipa fomu ili nijaze, na sasa nisha kamilisha kujaza ,kesho tar 6/march inabidi nikachukue TIN

Shida itakuwa kupata leseni kwani nimeambiwa inagharim kama laki 2 wakati hapanilipo nina elfu tano tu ya kula, sijui itakuwaje...

Naombeni Ushauri na mawazo yenu wadau kwani naamini SIWEZI BILA NYIE.

Mkuu usikate tamaa, cheki na hawa jamaa wanaitwa Advans Bank wako karibu na temeke hospital, wanahitaji TIN leseni kwao sio lazima, ila inabidi uwaelezee kuhusu biashara yako
 
unakula ndani ya biashara mkuu?
 
Sijakuelewa mkuu

namaanisha kwamba, unachozalisha ndicho unachokula?

yani kinachopatikana biasharani mwako ndicho hicho unachotumia kula ama vp?
 
namaanisha kwamba, unachozalisha ndicho unachokula?

yani kinachopatikana biasharani mwako ndicho hicho unachotumia kula ama vp?

Kama nimekuelewa jibu ni ndio.

Natengeneza na kuuza sofa kwahiyo kinachopatikana ndicho nachokifanyia mambo yangu..
Sijui niko sawa na swali lako?
 
Kama nimekuelewa jibu ni ndio.

Natengeneza na kuuza sofa kwahiyo kinachopatikana ndicho nachokifanyia mambo yangu..
Sijui niko sawa na swali lako?

ina maana unakula faida? si ndiyo?

una tabia ya kuweka kumbukumbu ya vitabu vya mahesabu?

biashara yako inakuaje endapo faida ndiyo unayokula?
 
ina maana unakula faida? si ndiyo?

una tabia ya kuweka kumbukumbu ya vitabu vya mahesabu?

biashara yako inakuaje endapo faida ndiyo unayokula?

Nilikua nafanya ki-local yaani bila kunote kumbukumbu zozote kwani haikuwa rasmi ila sasa ndo nimeamua kuifanya ajira yangu.

Pia nilikuwa nakula faida huku nahakikisha mtaji unabaki kama ulivo pia mara nyingi nafanya kazi za order.

Kama nimejibu kwa uzuri, ahsante
 
Nazidi kukata tamaa kwani kila hatua nayoifikia inanijia ugumu.

Ndo natoka TRA kufuata TIN namba, document zote nimekamilisha kujaza sasa hatua nilofikia naambiwa niende BANK nikalipe tsh. 199,000 , ni robo ya kodi ya mwaka nayotakiwa kulipa,,,nahisi zoezi linanishinda, nilipe kodi wakati nimewaambia biashara sijaanza jamani.......

Tanzania mbona kilakitu kigumu jamani.
 
Back
Top Bottom