Kama mheshimiwa makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alivyotangaza kuanza upandaji miti maeneo mbalimbali ifikapo siku ya leo ya oktoba mosi.
Wale mlio kwenye shughuli hiyo muhimu kwa ustawi wa mazingira tupeane taarifa ya zoezi linavyokwenda, vile vile kuwajulisha wengine sehemu ambayo miche ya miti inatolewa kwa wanaopanda miti.
miche na maeneo yakupandia ni changamoto wengi wa wakazi wa dar ni wapangaji na wafanya biashara maeneo hawana pia gharama za kununua miti na upatikanaji wake ni changamoto watapanda wachache inatosha
dah! utendaji kazi ukiegemea kwenye siasa ni mbaya sana. asante ukawa kwa kuwafanya watu wafanye kazi ambazo ambazo hawakuzipanga, kesho pangeni tarehe nyingine ili wapange kazi tena
wewe utaopanda mti wakati maji ya kumwagilia huna? lazima haya mambo mawili yaende sambamba, Dar ni kame, jua la siku moja tu linakausha kila kitu. nasubiri hoja ya maji Dar