Habari wadau!
Nilisikia kuwa Mh. Waziri wa Ujenzi leo atafanya kikao na Wanahabari pale Idara ya habari maelezo kuanzia saa 3 asubuhi, please naombeni updates kwa mlio karibu
Kama uko kwenye huo mkutano naomba umpatie huu ushauri wangu. Anaweza kuuchukua au kuuacha. The ball is in his court
Huyu Dr. Magufuli kakurupuka. Nilimsikia akisema kwamba nchi nyingine allowable tonnes ni pungufu ya Tanzania. Tanaznia ndiyo tunaruhusu uzito mkubwa ie 56 tonnes. Ok that is fine, lakini ni yale yale ya Spika Makinda kuulizwa kitu kingine yeye anajibu kitu kingine.
Hapa kinachogombaniwa ni msamaha wa 5% kwa uzito uliozidi. Hivyo basi solution hapa ni kwamba kama anaona uzito wa 56 tonnes + 5% tolerance limit ni kubwa na unaharibu barabara zetu anachotakiwa kufanya ni kupunguza allowable 56 tonnes mathalani zikawa 51 tonnes + 5% tolerance limit kwasababu zifuatazo.
Kwanza mizani yetu haiwi CALIBRATED on time and on regular basis, hivyo reading ya mzani wa Kibaha ni tofauti na mizani ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tinde (Shy) na Usagara (MZA). Mimi nilishawahi kusafiri kwa bus from DSM-MZA na nilikaa mbele nikaona hiyo variation ya reading inavyotofatiana kutoka mzani moja na mwingine. (Uzito kwenye mizani unasomeka kwenye taa mbele and anybody can read it).
Pili kwa wale mliowahi kufanya biashara ya mbao. Ukapakia mbao zako mathalani kutoka Urambo, Tabora tonnes ziko sawa kabisa eg 54 tonnes. Mbao unazipeleka DSM. Bahati mbaya ukafika Singida mvua ikanyesha, mbao hizo zikalowa na maji ya mvua. Believe me kama mkifika Dodoma mkapima uzito, mbao hizo hazitakuwa tena na uzito wa 54 tonnes, zinaweza kuongezeka hadi 56.4 tonnes, sasa kama hapo hakuna tolerance limit ya 5% tayari utatakiwa kulipa faini. Na hapa ndiyo unaona UZURI wa kuwa na tolerance limit. Mimi (transpoter) sijaleta mvua. Lakini mvua imenyeshea mbao zangu, zimeongezeka uzito, hivyo hiyo tolerance e limit itanisaidia because it was not my intention kuzidisha uzito in the first place.
Kuna mtu hapo juu amesema kwamba Utafiti wa kisayansi uliofanyika ulionesha kwamba mizani yaTanzania ina Standard errors up to 4%. Sasa kwanini Magufuri adharau utafiti huo wa kisayansi na kufuta hiyo 5% tolerance limit. Uzito unaweza kuonekana umezidi kwasababu ya hiyo variation ya reading ya mizani yetu.
Politicians Wa Tanzania hata awe msomi vipi lakini mamuuzi yao hayafuati ushauri wa Wasomi hapo Dr. Magufuri ametokota!.