update mwanamke aliyekatwa mguu tarime

Ilisolokobwe

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,850
803
wanajf hamjambo????
kama wiki 2 zilizopita hapa jf kulikuwa na topiki ya mwanamke kukatwa na mumewe hapa tarime!!!,mimi kama mwanajf sikuchangia chochote ktk mada ile'
jana mchana nilifika nyumbani kwao ghati chacha kwa ajili ya kumjulia hali maana sasa ametoka hospitalini,kweli nimkuta akiwa ameketi ktk kiti pembeni yake kuna jani la mgomba kwa ajili ya kufukuza mbu walimsumbua.
Ama kweli hujafa hujaumbika,ndugu zangu nishindwa kuyazuia machozi kwa hali niliyomkuta nayo yule binti mrembo.niliongea naye kwa muda wa masaa2 baadaye nikaondoka zangu.
kwa mujibu wa maelezo yake alisema yeye hakuwa na ugomvi wowote na mumewe chacha mwita. siku ya tukio walipotoka shambani ghati alipika wakala wote kisha mumewe akaaga kwenda sokoni na kaahidi angerudi baada ya muda mfupi lakini hakurudi mchana ule mpaka ilipofika saa 2 usiku alirudi akiwa amelewa na akagonga mlango huku akimuuliza ghati nani amekuoa hapa nyumbani?ghafla maskini akampiga na panga kichwani akaanguka chini na akaanza kumkata mguu wake hadi kautenganisha kabisa(picha ya kipande cha mguu ninayo,niliipata polisi jana).naye pia nilimpiga picha.
Tangu siku ya tukio mumewe yupo ndani ila kuna tetesi kuwa ndugu zake wana mpango wa kumtoa jela.
katika kipindi hiki ghati anakabiliwa na changamoto mbalimbali ukosefu wa pesa maana kwa muda huu alitakiwa awe bugando hospital kama alivyoshwauriwa na madaktari wa hospital ya wilaya tarime.
kibaya zaidi anaambiwa na ndugu za mumewe kuwa amesababisha ndugu yao kafungwa na anateseka jela kwa ajili yake.
Baada ya maelezo marefu bila shaka mmeelewa hali ya ghati ikoje mpaka sasa.
 
Ndio ulimwengu na walimwengu...salamu za pole kwa Ghati.
 
Naomba uendelee kufuatilia, na kama/mume akiachiliwa tuambie tuanzishe petition. Please follow up na utujuze, au ni-pm mimi.
 
Hili tukio linasikitisha sana. Huwa najiuliza sana kwa nini mtu anafikia uamzi wa kufanya unyama kama huu.????
 
Dah...inasikitisha sana.
Cha ajabu hapa kwetu tz hakuna umoja maana wanawake wote tulitakiwa kuamka ktk hili na kupinga huu uonevu,, kama mmeona movement ilifanywa na wanawake kenya kwa ajili ya yule binti aliyebakwa. Huyo mume wa Gath hatakiwi kuachwa huru maana amempatia mkewe kilema cha maisha.
 
mi nashangaa sana hao ndugu wa mwanaume kwa hiyo ndugu yao ni wa thamani sana kuliko huyu dada na unyama aliotendewa ni halali ila si halali ndugu yao kukaa jela kweli hakimu atakayemtoa huyu mtu ndani na apate maafa kila kukicha..amuhukumu maisha kha...jitu katili halafu eti bado watu wanaleta fyoko..mi ningekuwa ndugu wa huyu dada hamna namba hao ndugu wa mwanaume wasingesoma tena kwa usahihi....
 
naomba uendelee kufuatilia, na kama/mume akiachiliwa tuambie tuanzishe petition. Please follow up na utujuze, au ni-pm mimi.
poa kaka tupo pamoja maadam naishi kijiji kimoja pindi hicho kidume kitakapotoka gerezani nitawajuza
 
Dah...inasikitisha sana.
Cha ajabu hapa kwetu tz hakuna umoja maana wanawake wote tulitakiwa kuamka ktk hili na kupinga huu uonevu,, kama mmeona movement ilifanywa na wanawake kenya kwa ajili ya yule binti aliyebakwa. Huyo mume wa Gath hatakiwi kuachwa huru maana amempatia mkewe kilema cha maisha.

Division 5 zinatumaliza watz. Kuna mengi sana ya kusimama na kusema noooooooooo! Lakini hatuwezi! Unafikiri Division 5 mchezo!
 
Juzi watu wa human right wamemtembelea ghat na wakamshauri mama mzazi amchukue mwanae(ghati)amuuguze mwenyewe asije akadhuriwa na ukoo huu mbaya usiokuwa na chembe ya huruma.mama ghati aliahidi leo jumatatu atamfuata mwanae.hakika uchungu wa mwana aujua mzazi,leo nitawawekea picha za ghati ili mjionee anavyoendelea
 
Back
Top Bottom