Upauaji wa nyumba kulingana na maeneo

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
834
1,060
Watanzania tuna waste materials na space. Nataka niwaambie, hizi paa ndefu maana yake kuna space kubwa kati ya dari na paa ambayo hatuitumii kabisa.

Wenzetu wazungu wanaitumia hiyo nafasi kati ya dari na paa, inaitwa 'Attic' kwa sababu uezekaji wao sio kama wetu ambapo mbao zinakuwa zinasongamana kule juu, wao hazisongamani.

So tungeweza kuezeka kama wao ile nafasi najua kutokana na joto tusingeweza kuishi lkn tungeitumia kama stoo ya kuhifadhi vitu. Sasa unakuta jumba kubwa, paa limeenda juu maana yake kuna volume kubwa juu hatuitumii.

Na pia upauaji wa nyumba hulingana na Hali ya hewa,Kwa mazingira ya joto tunashauri paa liwe refu, kwenye mazingira ya baridi paa linakua fupi.mfano ukija Arusha nyumba nyingi paa ni fupi, na nyumba haiwi ndefu,ila Ukienda ukanda wa pwani-Dar es Salaam paa hua ndefu kutokana na joto.

Picha hapo chini ni mfano wa mapaaya wazungu wanavyoyatumia kuhifadhia vitu.

Nimeandika Kwa msaada wa face book.

Mwenye mawazo mapya

Karibuni

Screenshot_20230909-141350.jpg
 
Back
Top Bottom