Upasuaji wa Mgongo kwa Njia ya Matundu wafanyika Dar, Wagonjwa 13 wafanyiwa upasuaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kufuatia Kongamano la Kimataifa la Madaktari Bingwa wa Ubongo na Mgongo na Mishipa ya fahamu (Global Neurosurgery course) imeelezwa limechangia Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuanzisha huduma ya upasuaji wa mishipa ya mgongo kwa njia ya matundu (Endoscopic neurospine surgery).

Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano Kati ya Taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani limeshirikisha ambapo ya Wataalam 120 wanashiriki kutoka Mataifa mbalimbali Duniani limefanyika Jijini Dar es Salaam.
WhatsApp Image 2024-03-28 at 17.30.22_c8183921.jpg

WhatsApp Image 2024-03-28 at 17.30.23_0f82bcf2.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Prof. Abel Makubi amesema tayari Wagonjwa 13 wa mgongo wamefanyiwa upasuaji kwa mafanikio katika siku mbili (Jumatano na Alhamisi) toka kuanza kwa huduma hiyo.

Amesema uanzishwaji wa huduma hiyo inayotumia teknolojia ya kisasa inayotawala Dunia kwa sasa na itasaidia kuwapunguzia Wananchi gharama za kufuata matibabu ya aina hiyo nje ya nchi na kukuza tiba utalii hapa nchini.

“Hii ni kwa mara ya kwanza kwa MOI na ni mara ya kwanza kwa Taifa kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu (Endoscopic Spine Surgery), kwa dhati tunakishukuru Chuo Kikuu cha Weill Cornel cha Marekani kwa ushirikiano huu muhimu na kwa niaba ya menejimenti naahidi tutauenzi,” amesema Prof. Makubi.
WhatsApp Image 2024-03-28 at 17.30.25_5bfe3887.jpg

Prof. Abel Makubi
WhatsApp Image 2024-03-28 at 17.30.24_9da511de.jpg

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Taasisi ya MOI, Dkt. Hamisi Shabani

Upande wake Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornel Marekani, Prof. Roger Hartl ameahidi kuendeleza ushirikiano na Taasisi ya MOI katika kuendelea kuwajengea uwezo wataalam, kuwezesha tafiti za kisayansi na vifaa tiba vya upasuaji ili iweze kuwa kituo mahiri cha upasaji wa mgongo barani Afrika.

“Lengo letu kuiona MOI ikiwa kituo cha umahiri kwenye kutoa tiba na mafunzo kwa mataifa mengine juu ya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu, nimefurahi kuona namna ambavyo MOI inathamini ushirikiano wetu na ninaahidi kuuendeleza,” amesema Prof. Hartl
WhatsApp Image 2024-03-28 at 17.30.27_f83248e2.jpg

Prof. Roger Hartl
 
Back
Top Bottom