Mkuu pole sana kwa kuumwa. Kuna mambo kadhaa hapo ambayo hujaelezea kiasi kwamba kujibu swali lako au kukupatia ushauri inakuwa vigumu kidogo.
1.huyo dactari anayekuhudumia ni internal medicine au umeshaonana na gastroenterologist ?
2.Ulishafanya kipimo kama EGD nadhani huko home mnaita EGI (Esophagogastroduodenoscopy) ili kufahamu GERD yako inasababishwa na nini ? Hernia au malfunctioning valve?
3.Umetumia dawa gani na kwa muda gani ? Ulifuata masharti ya dawa ? Kwa mfano group la proton pump inhibitors kama omeprazole inabidi umeze dawa kwenye tumbo tupu kisha usubiri angalau saa moja kabla hujala kitu.
4.Huyo dactari wako amekuambia ni surgery ya aina gani ? Nakupa mifano miwili hapa
A.The transoral incisionless fundoplication--Hii wanapitia mdomoni kwa hiyo hakuna incision kwa nje,kisha wanatengeneza valve kama tatizo lako linasababishwa na malfunctioning valve etc etc.
B.A Nissen fundoplication jina jingine ni laparoscopic Nissen fundoplication nayo ni procedure nyingine na imakuwa inatumika kwa miaka mingi sana.
Sidhani kama nimejibu swali lako ila kama utanipatia information zaidi naweza kukupatia mwanga. Pole sana kiongozi.