Upasuaji Saratani ya Matiti kufanyika bila kuliondoa

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1061556



Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya imeandaa mkutano wa kisayansi wa kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa kufanya upasuaji wa saratani ya matiti kwa kutoa uvimbe bila kuondoa titi lote kwa wagonjwa wenye dalili za mwanzoni.

Mkutano huo wa kisayansi ambao ni wa kwanza kufanyika katika Hospitali ya Mloganzila umefunguliwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence, umelenga kukumbushana namna bora ya kuwapatia matibabu kwa njia ya kisasa wagonjwa ambao wamethibitika kuwa na saratani ya matiti.

Mafunzo hayo yanashirikisha wataalam 30 kutoka Muhimbili pamoja na Hospitali za rufaa nchini ambazo ni Bugando, KCMC, Mbeya na Hospitali binafsi ya Besta.

Kupitia mtaalam mbobezi kutoka Nairobi, Kenya Dkt. Peter Bird, wataalam hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa muda wa siku nne ambapo pia mada mbalimbali zinazohusu utoaji wa matibabu ya saratani ya matiti zitawasilishwa.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru kampuni ya dawa ya Roche kwa kushirikiana na hospitali yetu ili kuwajengea uwezo wataalam hapa nchini kwani wataalam watakaofaidika na mafunzo haya wataenda kuwajengea uwezo wataalam wengine”. Amesema Prof. Museru

Akifafanua amesema saratani ya matiti inachangia vifo kwa wanawake duniani kwa asilimia 25 hadi 35, pia saratani ya matiti ipo kwa kiwango cha juu katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea japokuwa vifo vingi vinavyotokana na saratani hiyo hutokea katika nchi zinazoendelea kutokana na wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu.
 
Back
Top Bottom