Upande Mbaya wa Mitandao Jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upande Mbaya wa Mitandao Jamii

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Apr 14, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Upande Mbaya wa Mitandao Jamii

  Kuna watu wanapenda kutuatilia watu wanaopenda mawazo na maoni yao kwa njia ya mtandao kama sio podcast basi ni kwenye makundi ya facebook au kwa njia ya twitter .

  Njia hiyo ya kufuatilia taarifa na habari za watu , makundi au shuguli fulani imeleta mapinduzi katika dunia ya mawasiliano kwa kiasi kikubwa uzuri ni kwamba unaweza kufuatilia mtu hata kwa njia ya simu ya kiganja au habari fulani hivyo hivyo

  Hata hivyo kuna baadhi ya matendo na ishara zinazoonyeshwa kwenye ufuatiliaji wa habari hizi kwa watu wengine ambapo unanyima wengine fursa ya kujadili kile anachoona kinafaa kwa jamii ya wengi kutokana na kundi hilo kuwa na msimamo fulani .

  Fikiria umefungua mtandao fulani tena ina watanzania wenzako lakini ukatakiwa ujisajili ili uweze kutoa maoni yako unapojisajili msimamizi wa mtandao huo anakataa usajili wako endapo umetumia jina lako kamili .

  Na fikiria kwamba unafuatilia blogu fulani kwa njia ya barua pepe lakini blogu hiyo mara ghafla maoni yanaanza kubadilika kuanza kushambulia baadhi ya makundi katika jamii kwa misingi ya dini , kabila au jinsia unapojaribu kuhoji kwa jina lako tu usajili wako unaishia hapo hapo .

  Pamoja na kwamba mitandao jamii pamoja na mtandao wa kimataifa wa kompyuta umepewa nafasi pekee maishani mwa watu wengi kwa kuamini kila wanachoona au kusoma kwa njia ya mtandao pamoja na kushiriki baadhi ya mijadala kwa njia ya mtandao watu inabidi wawe waangalifu sana .

  Kwa sababu kila siku inavyozidi kwenda watu wanazidi kusajili na kuingiza kazi na mambo yao kwa njia ya mtandao haswa mitandao jamii kama facebook , tagged na hi5 , ndani ya mitandao hii kuna vikundi vya watu wa aina mbalimbali kama vinavyochochea ubaguzi huko afrika ya kusini , mambo ya fujo na aina nyingine ya uchafuaji wa hali ya amani kwenye jamii .

  Baadhi ya mitandao jamii imeanza kuweka sheria kali kwa wanachama waliojisajili kwenye mitandao hiyo na kufuatilia baadhi ya vitu vinavyoandikwa na wanachama wa mitandao hiyo au kufuta vitu hivyo mkakati huu umefanikiwa sana kwa nchi kama uchina , korea kaskazini na irani lakini kwa nchi za kimagaribi hali imeonekana mbaya zaidi kwa sababu watu wa jamii hizo wanataka uhuru zaidi wa mambo yao na katika kutumia mitandao hiyo .

  Kwahiyo mabadiliko yanayofanyika kwenye mitandao jamii yanayohusu watu wanavyotumia na wanachosema yamekuwa tata sana kwenye nchi ambazo zina uhuru mkubwa wa maoni haswa yanapokuja masuala binafsi .

  Kwa kudhibitisha hali hii angalia mtandao wa facebook ulivyojaribu kufanyia mabadiliko sheria za kulinda watu wa umri mdogo kwenye mtandao huo ulivyoleta tabu kwa nchi nyingi za ulaya lakini pia angalia magaidi watoto wengi wanaokamatwa nchi za pakistan na afghanistan wengi wameonekana kutokea nchi za magaribi ambapo asilimia kubwa walitumia mitandao jamii kuwasiliana na wenyeji wao huko walipoalikwa .

  Angalia wale vijana 4 wa kimarekani ambao wanashikiliwa kwenye jela moja ya kijeshi huko pakistan , angalia kijana mmoja wa kinaigeria ambaye alijalibu kujilipua huko detroit ambaye aliishi yemen lakini muda mwingi ni london uingereza , angalia yule askari aliyeuwa wenzake 5 huko huko marekani nae aliwacha ujumbe kwenye anuani yake ya facebook .

  Hii ni hali inayozidi kukuwa kila siku kwenye mitandao jamii wale watu ambao wanaendesha chuki , vurugu na aina nyingi ya hujuma sasa wamepata nafasi nyingine mpya ya kutuma ujumbe wao kwa wafuasi wao au hata kupata wafuasi wapya wa shuguli zao mbali mbali

  Kwenye mitandao hii pamoja na hizo chuki kwa watoto wadogo wanaweza kuonewa au kupata unyanyasaji fulani ndani ya mitandao hiyo na hali hiyo inaweza kuwaumiza kwenye maisha yao ya kila siku .

  Kama wewe ni mzazi unamruhusu mtoto wako achungulie mitandao jamii jaribu kufuatilia kujua yeye anafuatilia makundi gani au kina nani ili apate taarifa zao na yeye anafuatwa na nani kwenye mtandao wake , marafiki zake ni kina nani na vitu kama hivyo .
   
Loading...