Upandaji wa shamba la mkonge

Jun 7, 2022
14
21
Vyanzo vya miche bora ya Mkonge

1. Maotea/Matoto ya Mkonge Mkubwa (Suckers)
2. Vikonyo vilivyokuzwa katika kitalu

Hasara za kutumia maotea
1. Si rahisi kupata miche inayo lingana urefu, umri na uzito
2. Ni vigumu kupata maotea ya kutosha shamba zima
3. Mkonge hukomaa na kutoa milingoti mapema
4. Ni rahisi kueneza magonjwa na wadudu waharibifu

Faida za kutumia Vikonyo
1. Ni rahisi kuvikusanya pamoja kwa wingi
2. Ni rahisi kuvipanga katika madaraja
3. Hutoa Mkonge wa Kimo sawa shambani

Miche ya Kupanda
-Miche ya kupanda iwe kati ya sentimita 50 hadi 70 na uzito wa kilo 2 hadi 4 Aidha miche ipandwe kulingana na ukubwa wake kwenye boma.
-Mizizi ya miche ipunguzwe kwa uangalifu bila kuharibu shina (Kitunguu) na majani yaliyo kauka yaondolewe
-Inashauriwa kutumia miche bora
-Baada ya kun'golewa miche hiyo inashauriwa iachwe kwa muda wa majuma matatu kabla ya kupanda ili inyauke (Curing)
-Mkonge upandwe mwezi mmoja hadi wiki mbili kabla ya mvua kuanza ili kuepuka kuoza mashina haswa kipindi cha masika
-Shimo liwe kati ya sentimita 8 hadi 10 na mche ushindiliwe vizuri na hakikisha sehemu zote zenye mizizi zimetumbukizwa kwenye shimo
-Kwa sehemu zenye miteremko ni muhimu miraba ipandwe kukata mteremko au kutumia kontua
-Mkulima anashauliwa baada ya kupanda sehemu ambazo mkonge umekufa zirudishiwe ndani ya miezi 6 hadi 9
-Mkulima anashauriwa kupanda miche kwenye mistari ya ziada kwaajili ya kurudishia

MIFUMO YA UPANDAJI
1. Mfumo wa mraba mmoja
2. Mfumo wa Miraba miwili

1. MFUMO WA MRABA MMOJA
Nafasi kati ya mraba mmoja na mwingine ni mita 3 hadi mita 4, na vipimo vya 70cm , 80cm na mita 1 hutumika kati ya mche hadi mche
Mfumo huu unampa mkulima hadi miche 3,500 kwa hekta

1654946674982.png



Faida za Mfumo wa Mraba Mmoja
- Ni rahisi kupalilia
-Kukata majani ni rahisi haswa kwa mkataji asiye na uzoefu

Hasara za Mfumo wa Mraba Mmoja
-Matumizi ya mashine wakati wa kufyeka majani ni mgumu kama nafasi itaachwa ndogo
-Gharama kubwa ya palizi

2. MFUMO WA MIRAMBA MIWILI
Miraba miwili huwekwa pamoja na nafasi kati ya jozi/ Nyororo moja ya mkonge na nyingine ni mita 3 hadi 4 wakati nafasi kati ya mche mmoja na mwingine ni mita 1 kwa pande zote
-Mfumo huu Mkulima naweza kupata hadi miche 4,000 hadi 5,000 kwa hekta

1654946735918.png


Faida Zake
-Mimea inakuwa ni mingi kwa eneo
-Kivuli kati ya miche ya miraba sambamba hupunguza utoaji wa magugu

1654946812201.png


Hasara Zake,
-Ni vigumu kuondoa mapotea katikati ya miraba sambamba
-Inahitaji vibarua wazoefu kuchokoa/kupalilia

MAANDALIZI YA SHAMBA LA MKONGE
Utayarishaji wa shamba la mkonge ni muhimu kama ilivyo muhimu katika mazao mengine kama mahindi, mtama, alizeti na pamba. Wakati wa kuandaa shamba ni vizuri kupima udongo.

Hatua zifuatazo ni muhimu kuzingatiwa

-Shamba linapaswa kutayarishwa kabla ya msimu wa mvua kuanza.
-Vichaka vyote vinatakiwa kukatwa na kuachwa vikauke na kuoza au kukusanywa sehemu moja pembeni.
-Visiki vyote ving’olewe ili kurahisisha trekta kupita kwa urahisi.
1654946350171.png


shamba la mkonge lilolimwa vizuri na kusawazishwa
1654946445917.png

-Kila baada ya maboma mawili hadi manne kuwe na barabara ya mita 3.5 hadi 4 kwaajili ya kuzuia moto na kurahisisha usombaji wa mkonge uliokatwa. Pia barabara hizi zinatakiwa ziwe safi muda wote.
 
Soko la mkonge lipo? Wadau wengi kabla ya kuwekeza wanahitaji kujua hilo
 
wananchi wana taka katiba mpya ili wale bata... hawataki shurba za kuangaika kulima lima... hivyo mtuache tuendelee na mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya...

mambo ya kulima tuache wachina, wazungu waje walime kisamvu, mchicha, nyanya na kutembeza madafu mtaani...
 
wananchi wana taka katiba mpya ili wale bata... hawataki shurba za kuangaika kulima lima... hivyo mtuache tuendelee na mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya...

mambo ya kulima tuache wachina, wazungu waje walime kisamvu, mchicha, nyanya na kutembeza madafu mtaani...
Tehetehe.. watu wanadhani katiba mpya iafanya mana zishuke kutoka mbinguni
 
wananchi wana taka katiba mpya ili wale bata... hawataki shurba za kuangaika kulima lima... hivyo mtuache tuendelee na mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya...

mambo ya kulima tuache wachina, wazungu waje walime kisamvu, mchicha, nyanya na kutembeza madafu mtaani...
Asante kwa maoni yako
 
Kilimo cha mkonge kinatumia muda gani? Kwenye upandaji wake hadi mavuno? Heka moja inatoa mavuno kiasi gani?
 
Back
Top Bottom