Kinega Michapo
New Member
- Apr 15, 2013
- 1
- 0
Ni mwaka wa nne huu Asasi za Uwezo na Tweweza zimekuwa zikifanya tathmini ya stadi kuu za kusoma na kuhesabu kwa lugh zote mbili za kiingereza na Kiswahili. Utafiti huu hufanywa na watu wanaochaguliwa na kupewa cheo cha Uratibu wa wilaya (DC). Uoza wa tafiti yao hii kuanzia ukusanyaji wa data hadi matokeo yanayotangazwa kwa Watanzania unakuja kutokana na upatikanaji wa hao waratibu wa wilaya ambao ndiyo wanaoenda kusimamia zoezi zima la kukusanya taarifa zinazohitajika kwa kupitia watafiti wa kujitolea.
Asilimia 90 ya hao waratibu wa wilaya, na kwa mwaka huu wameongezwa wa mikoa hawana sifa zinazoendana na aina ya zoezi hilo na kazi yenyewe ya utafiti huo. Waratibu hawa wa wilaya na mikoa hupatikana kwa njia za ajabu zisizojali merit factor, usishangae umekaa kijiweni nukapigiwa simu "kesho njoo Morogoro kwenye semina, tafuta na marafiki zako watatu uje nao" bila ya kujali elimu, uwezo wa hao watu na sifa zao.
Waratibu hao wa Wilaya na mikoa wengi wao ni waalimu wa upe na diploma holders tena za ualimu. Cha ajabu tayari Uwezo/Tweweza ilishatangaza nafasi hizo za uratibu wa Wilaya na Mikoa na kutaja kuwa sifa ya kielimu ni lazima uwe na Degree kwenye masomo ya Sayansi ya Jamii, kizuri zaidi watu wenye kiwango hicho cha elimu wameomba tena kwa wingi tu.
Wachache walifanyiwa usaili kwa njia ya simu na wengi wao hawajafanyiwa usaili na hao wachache waliofanyiwa usaili kwa njia ya simu wengi wao hawajaitwa na badala yake, Waratibu wenye uzoefu ndiyo wanapewa jukumu la kuwaunganishia kazi hiyo washkaji zao kwa kushirikiana na viongozi wa Uwezo kwa ahadi ya kuwatoa kirushwa hao viongozi wa Uwezo/Twaweza.
Watu hawa ndiyo tunaotarajia waende vijijini kufanya ama kusimamia zoezi hili, lakini tangu wanaingizwa kwenye timu ya Waratibu tayari washaandaliwa mazingira ya CCM yaani Chukua Chako Mapema. Si ajabu mtaribu akajifungia chumbani kwake na washkaji zake watatu wakamaliza kujaza madodoso 30 ukatembezwa mgao watu haoo! Halafu kesho Uwezo inatoa taarifa za uongo kwa Watanzania.
Hakuna mratibu anayeweza kumsimamia mwenzake iwe wa Wialaya au Mkoa ikiwa wote wamemegeana pande la hiyo kazi, unless watakaa pamoja na kujadiliana jinsi ya kuchakachua mshiko na kufichiana siri tu. Twaweza wana jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa waratibu hawa wote wa Wilaya na Mikoa kwa kuangalia upya sifa zao, ila wasishangae watakapojikuta wana waratibu ambao ofisi haina taarifa zao maana walitoka kwao baada ya kupigiwa simu jana na kwenda direct kwenye kwenye mafunzo bila ya kuomba nafasi hizo za kuwatumikia Watanzania.
Kwa uzoefu wangu hata kama na mimi ni mmoja wa waratibu kwenye zoezi hili, lakini sijawahi na sitawahi kuja kuwa na imani juu ya matokea ya tafiti hii ya Uwezo mpaka pale watu sahihi waliomo ndani watakapochanganywa na watu sahihi walioachwa watakapopewa jukumu la kuifanya kazi hii hata kama ni ya kujitolea.