Uozo wa miradi ya ujenzi wa shule..

Uozo wa miradi ya ujenzi wa shule..

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu. Kuna jambo limekuwa linaiumiza sana nafsi yangu.. nimetembea kwenye shule nyingi za serikali hapa Nchini miradi ya ujenzi inayofanyika katika shule hasa ya madarasa na nyumba za walimu ni imetekekelezwa kiwango cha chini mno mpaka unafikia mahali pa kujiuliza hivi hawa waliopewa hizi kazi wana watoto kweli? Na kama wana watoto wao je wanasoma katika hizi shule za serikali.. darasa linajengwa halichukui hata mwaka mmoja sakafu yote imevunjika madarasa yana nyufa kila mahali..
nyumba za walimu na ujenzi mwingine kadharika hivi kweli hawa watu wanakuwa bado wapo uraini hawajakamatwa ama kufungwa?
ni aibu kwa Taifa letu acha Magufuli aendelee kuwanyoosha.!
mfano wa ujenzi wa nyumba za walimu shule ya msingi Hondogo Dar es salaam.
 
Naambatanisha hapa za nyumba za walimu zailizo jengwa shule ya msingi Hondogo
C360_2017-09-20-12-58-07-960.jpg
C360_2017-09-20-12-57-07-420.jpg
 
Kama noma iwe noma kwenye uzi huu nitatupia picha za miradi ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu kwenye kila shule, ya msingi au sekondari.. penye sifa tutasifia lakini kwenye uozo pia tutaonesha...!!!
TUMEWACHOKA..
 
KHAAA! ILA ISHU KAMA HII HATA INJ'... NA MK.. WA HALMASHAURI WANAHUSIKA
Wee acha tu mkuu yangu endapo ndugu yako ni mwalimu halafu unakuta anaishi kwenye nyumba kama hiyo yenye choo kilicho bomoka.. halafu nyumba yenyewe imeshapasuka[emoji22][emoji22]
hebu angalia pazia lile.. halafu eti choo kimewekwa Tiles..
 
Nchi yetu tunaibomoa wenyewe na wasomi wetu
Na hao ndio wanao piga kelele kuwa Magufuli hafai.. imagine hapo alikuwepo engineer wa wilaya kinondoni au ubungo kwa sasa.! Yupo afisa Elimu ipo kamati ya shule... yupo mkuu wa wilaya na nk
 
Wee acha tu mkuu yangu endapo ndugu yako ni mwalimu halafu unakuta anaishi kwenye nyumba kama hiyo yenye choo kilicho bomoka.. halafu nyumba yenyewe imeshapasuka[emoji22][emoji22]
hebu angalia pazia lile.. halafu eti choo kimewekwa Tiles..
kwa hasira zangu hao gwantanamo ndo ingekuwa makazi yao!
 
Mada Nzuri hii,

Iko hivi, hii miradi mpaka inakamilika, watu mbalimbali wa Manispaa wanahusika kuanzia Mhandisi wa Manispaa, Wakaguzi wa Majengo/Miradi ya Ujenzi,Wasimamizi, na Maafisa Ugavi.Hawa ndio "wapigaji" wa hii Miradi.
Nenda shule za PembaMnazi na Somangila Kigamboni, na Tembelea Nyumba za walimu wa shule ya Msingi Msigani, ni aibu.

Kuna wakati nafikiria Rais wa sasa,aongoze nchi mpaka 2035. Hii miaka 10 ni michache sana kuondoa watu takataka kama hawa.
 
Mkuu mi nafikiri tunachopaswa kufanya ni kuwaumbua. Kwa kuweka picha za majengo yote yaliyosimamiwa na kutekelezwa na hawa Mchwa.!!
 
Back
Top Bottom