Uozo Tanesco- Wialaya ya Kyela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uozo Tanesco- Wialaya ya Kyela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Logo, Feb 24, 2012.

 1. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau kuna watu wengine huwa hawawezi kusema matatizo yanayowasumbua badala yake wananyamaza tu. Wacha mimi niliyepita nikawaona niwasaidie kuyasema!

  Nilipita Kyela (Kwenye jimbo la Dr. Mwakyembe)wiki hii kwa siku 3(Jumapili-Jumanne) tangu nifike kulikuwa giza nikauliza kuna nini waksema Umeme umekatika, mpaka siku naondoka umeme ulikuwa umekatika. Wenyeji walisema walishazoea hiyo ni kawaida tu kwao, inasemekana kuna sehemu inaitwa Kasumulu Transformer ilishaungua ina miezi kama 3 hakuna hata inshu, meneja wa wilaya yupo tu amelala anakunywa supu teh teh teh.

  Sasa kwa fani zetu za uandishi wa habari usiombe ndugu yangu nilizama ndani kwa kina kupeleleza nini hasa tatizo. Tatzi kubwa ni miundo mbinu imeharibika sana, Nguzo nyingi zimeoza sana na pia mfumo wao wa umeme hauko vizuri, yaani hata mvua tu ikianza kunyesha wanazima kuepusha short ya umeme.

  Kibaya ni kwamba Meneja wa Tanesco Kyela ni kichwa maji kabisa huyu baba! Yeye hata haumizi kichwa. Kwa taarifa nilizozipata ndani ya boksi zinasema hivi "Huyu Meneja alikuwa Tunduma akatimuliwa sasa hii serikali yetu bana, akawa amefanyiwa deal akaletwa huku Kyela hahaha sasa anakula na kunywa tu hana kazi kabisa! Wana Kyela amkeni akitoka huyo meneja matatizo ya umeme yataisha Kyela, mnahitaji mtu anayejituma siyo kulalala kama nilivyoweza kuchunguza huyo.

  Unganeni pamoja mseme hatumtaki mzembe, Amekataliwa tunduma nyinyi mletewe huyo? Wakati wa DC Manumba ilikuwa umeme ukikatika Meneja aliyekuwepo alikuwa akiwekwa ndani hahahaha huyu sijui wanamuogopa nini. Chonde chonde wana Kyela.
   
 2. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania imeoza jaman tusipoangalia tutaizika wenyewe
   
Loading...