DOKEZO Rais amedanganywa na Mbunge kuhusu Maendeleo ya Miradi Wilayani Kyela

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hii nimeiona kwenye Group linajiita MATAGA ila CHADEMA wamo kibao. Nikaona niwatumie hapa nanyi muione.

====

"CCM Mkoa wa Mbeya wanatamba kuwa Ziara ya Rais Samia Wilaya ya Kyela ilifana sana Jumapili tar.7/8/2022. Ni kweli kwa upande wa idadi ya watu na suti nyeusi za walinzi na wasaidizi wake wengi lakini si kwa taarifa za uongo ambazo Mama alizipokea bila kushituka au kuhoji.

Mara kadhaa Mama alionyesha kuto kujua tofauti kati ya Kyela na Rungwe. Pengine alikuwa amechoka sana au alikuwa hajaandaliwa vizuri na wasaidizi wake.

Pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Mbunge wa Kyela ajiimarishe vizuri kisiasa maana mpaka sasa anahangaishwa na kivuli kikubwa cha Mwakyembe pamoja na kwamba mwanasiasa huyo mstaafu haoneshi nia ya kuendelea na siasa. Amejichimbia Dar es Salaam na wala haonekani Kyela.

Mbunge Alinanuswe (au Ali kama anavyojiita kwa kifupi ili atambulike kama Mwislamu wakati siyo), aliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge Kyela kama project ya Mangula na JPM ili kumng'oa Mwakyembe. Ali alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kyela.

Tofauti na wenyeviti wengine wa CCM wa Wilaya nchini waliozuiwa kugombea ubunge kwenye wilaya zao, yeye aliruhusiwa ili kuking'oa kisiki. Waliompenda Mwakyembe ndani ya "system" walimweleza kuwa atang'olewa, yeye hakuamini kwa imani kubwa aliyokuwa nayo kwa watu wake. Nguvu kubwa ndani ya CCM na vyombo vya dola, ikamng'oa Mwakyembe kwenye kura za maoni za JPM. Katika uchaguzi mkuu wana CCM wenye hasira wakamuunga mkono mgombea wa CHADEMA, lakini ushindi wake ukatwaliwa na vyombo vya JPM, "akashinda" Ali!

Kazi kubwa iliyopo Kyela sasa ni kumbeba Ali kwa porojo mbalimbali. Mfano mzuri ni mradi aliozindua Rais Samia wilaya ya Kyela wa Barabara ya Kikusya - Matema ambao utekelezaji wake ulianza kipindi cha Kikwete na mradi wa Kituo cha pamoja na Malawi cha Forodha Kasumulu ambao vilevile utekelezaji wake ilianza kipindi cha Kikwete!

Miradi yote ya maji, zahanati na ukarabati mkubwa wa hospitali ya Wilaya aliyotaja Mbunge wa Kyela Ali, haikuanza kipindi cha Mama, ila kipindi cha Kikwete na michache sana kipindi cha Magufuli! Lakini kelele za Ali zilimsifia Mama, Mama, Mama kwa kutoa hela bila kueleza mwanzo wake.

Najua wengi msio makini mtaniita CHADEMA, ACT, SUKUMA GANG n.k. lakini ukweli ni ukweli. Kwani Magufuli na Kikwete ninaowataja, walikuwa UKAWA?

Pamoja na kupiga magoti ya kisanii na kuwadanganya wananchi kuwa fedha za miradi yote anazipata kwa yeye mwenyewe Alinanuswe kuongea na Samia na wala siyo kupitia kwa Mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya au DC wa Kyela (wakati wabunge wote wanapelekewa fedha za zahanati, maji na ukarabati wa barabara bila uongo wa kuongea moja kwa moja na Samia) mbona hakuongelea kukwama kwa mafao ya wafanyakazi wa Mgodi wa Kiwira?
Hili nimeambiwa ni suala kubwa sana Kyela ambalo mpaka leo halijatekelezwa.

Wananchi walitaka amweleze Rais kushindwa kwa Mamlaka husika kuchangamkia biashara ya meli mpya za Ziwa Nyasa (mbili za mizigo na moja ya abiria na mizigo) ambazo huu ni mwaka wa nne hazitumiwi ipasavyo? Shida ni kukosa kujituma na ubunifu tu!

Walitaka azungumzie ujenzi wa mradi wa bandari ndogo ya Matema na gati za Mwaya na Ikombe ili meli hizo zitumike vizuri. Lakini hakuweza kwani miradi hiyo inaimba jina la Mwakyembe.

Mbunge Ali alishindwa kuongelea kukosekana kwa meli kubwa ya uvuvi Ziwa Nyasa kunakochangia lishe duni Mkoa wa Mbeya. Bado tunatumia mitumbwi ya karne iliyopita kuvua samaki! Samaki kidogo tunaovua, hawakamatiki kwa bei! Kwa nini Serikali isiwekeze kwenye meli kubwa ya uvuvi na kiwanda cha samaki?

Mbona hakugusia kusimama kwa miradi mikubwa ya pamoja na Malawi ya maji, barabara, uvuvi, umwagiliaji na umeme ya Mamlaka ya Bonde la Mto Songwe?

Mbona hakumweleza Rais kuwa wananchi wanaoishi Ikombe wameona kwa miaka zaidi ya 15 ujenzi wa polepole mno wa barabara ya kuunganisha Ikombe na Matema. Lini Serikali itamalizia barabara hii?

Mbona hakugusia suala la wazee wengi wa Kyela kusahauliwa kwenye mfuko wa TASAF kulinganisha na wilaya zingine?

Mbona hakusema kuhusu shida ya kupata dawa na kupata huduma nzuri kwenye vyombo vya afya vya serikali: hospitali ya wilaya, vituo cha afya, zahanati?

Sawa kamdanganya Mama kwa ulaini sana. Hatushangai kwani anatutambia sana kuwa yuko karibu sana na watu wawil: Mama na Mangula pamoja na kwamba amestaafu. Lakini tunamwambia, wananchi wanaolalamikia kupanda kwa bei ya sukari, mafuta ya kupikia, nauli, tozo nk HAWADANGANYIKI."
 
Hivi kwann wabunge wanajidhalilisha Sana mbele ya watu wanao wawakilisha? Kwann wanaamua kujitwika jukumu lisilokuwa lao la ujenzi wa miundombinu ktk majimbo yao?

Hivi wabunge hawa wanaelewa majukumu yao kweli? Kwann mbunge asitembee kifua mbele hata kama miundombinu haijajengwa ?

Wabunge siyo kazi yao kujenga miundombinu na huduma mbalimbali ktk majimbo yao.

Hivyo jaribio lolote la kujinasibisha na uboreshaji ama ujenzi wa miundombinu majimboni ni kujidhalilosha tu.
 
Uzi huu nadhani umeundwa kwa watu wasio na mapenzi mema na kinanasi kwa malengo yao ya kisiasa na ndio madhara ya kuwa na I'd mbili ndani ya jamii forum. Yapo ambayo nitakubaliana na wewe na mengine nitakupinga maana inaonekana hauelewi.

1. Kinanasi sio tuu zao la magufuli ama mangula ila ni mtu aliyeanza kusaka ubunge mapema kidogo. Mwakyembe hakuangushwa na Magufuli aliangushwa na wanakyela walio kuwa wamechoka mno na siasa zake. Mwakyembe sio kitisho kwa kinanasi ila siasa tuu za kinyakyusa the way zilivyo huwa zinakuwa kitisho kwa mwanasiasa yeyote maana hazina uhakika wa kudumu.. kinanasi anaweza kuwa anamuhofu eng. Mwakalinga ambaye anaungwa mkono na wanakyela wote ila pia anaweza kuwa anamuhofu Daktari Hunter mwakifuna mwenye siasa hatari za kimawindo mawindo.

2 . Miradi iliyozinduliwa ule wa Boda na Barabara ya kikusya matema kweli kilichofanyika ni usanii maana sio ya mama kabisa ila nikukosoe ile miradi uliyoitaja mpaka meli kikwete alipiga danadana miaka kenda rudi ni msukumo mkubwa mno wa Magufuli na Rafiki yake Eng Elius mwakalinga.

3. Mradi wa Hospitali ya Kyela jengo la Ghorofa kwamba ulianza wakati wa kikwete ni UWONGO ulio kubuhu. Mimi ninachofahamu labda aliidhinisha magufuli sijui ila Mama samia ameanza na msingi.

4. Umeandika Mengi mno ya Uongo mtupu yaani kwakifupi huu uzi ni wauongo ndio hayo nimeeleza pale juu kuwa ni Siasa ngumu za kinyakyusa niishie kwa kupinga moja ulilolidanganya kwamba ati kinanasi hakuzungumzia malipo ya stamiko. Kiananasi aliongelea kero mbili tuu mbele ya Rais la kwanza malipo ya Mafao ya Stamiko na mfumo wa mauzo ya kokoa.

huu uzi umekaa kimbea mbea sana inatakiwa upelekwe mataga kwa wachambaji. Uzi wa uongo uongo tuu.

Mwisho:

Kinanasi anakuja vizuri japo speed yake ni ya kawaida. Kwa wanakyela ushawishi wake mpaka sasa ni zaidi ya 95% kutokana na kujikita sana vijijini Na kutatua kwa haraka migogoro iliyokuwa sugu kwa wananchi wake, tofauti kabisa na mtangulizi wake.
 
3.Mradi wa Hospitali ya Kyela jengo la Ghorofa kwamba ulianza wakati wa kikwete ni UWONGO ulio kubuhu. Mimi ninachofahamu labda aliidhinisha magufuli sijui ila Mama samia ameanza na msingi.
4. Umeandika Mengi mno ya Uongo mtupu yaani kwakifupi huu uzi ni wauongo ndio hayo nimeeleza pale juu kuwa ni Siasa ngumu za kinyakyusa niishie kwa kupinga moja ulilolidanganya kwamba ati kinanasi hakuzungumzia malipo ya stamiko. Kiananasi aliongelea kero mbili tuu mbele ya Rais la kwanza malipo ya Mafao ya Stamiko na mfumo wa mauzo ya kokoa.

huu uzi umekaa kimbea mbea sana inatakiwa upelekwe mataga kwa wachambaji. Uzi wa uongo uongo tuu.

Mwisho:
Kinanasi anakuja vizuri japo speed yake ni ya kawaida. Kwa wanakyela ushawishi wake mpaka sasa ni zaidi ya 95% kutokana na kujikita sana vijijini Na kutatua kwa haraka migogoro iliyokuwa sugu kwa wananchi wake, tofauti kabisa na mtangulizi wake.
Kwako tena Erythrocyte
 
Uzi huu nadhani umeundwa kwa watu wasio na mapenzi mema na kinanasi kwa malengo yao ya kisiasa na ndio madhara ya kuwa na I'd mbili ndani ya jamii forum. Yapo ambayo nitakubaliana na wewe na mengine nitakupinga maana inaonekana hauelewi.

1. Kinanasi sio tuu zao la magufuli ama mangula ila ni mtu aliyeanza kusaka ubunge mapema kidogo. Mwakyembe hakuangushwa na Magufuli aliangushwa na wanakyela walio kuwa wamechoka mno na siasa zake. Mwakyembe sio kitisho kwa kinanasi ila siasa tuu za kinyakyusa the way zilivyo huwa zinakuwa kitisho kwa mwanasiasa yeyote maana hazina uhakika wa kudumu.. kinanasi anaweza kuwa anamuhofu eng. Mwakalinga ambaye anaungwa mkono na wanakyela wote ila pia anaweza kuwa anamuhofu Daktari Hunter mwakifuna mwenye siasa hatari za kimawindo mawindo.

2 . Miradi iliyozinduliwa ule wa Boda na Barabara ya kikusya matema kweli kilichofanyika ni usanii maana sio ya mama kabisa ila nikukosoe ile miradi uliyoitaja mpaka meli kikwete alipiga danadana miaka kenda rudi ni msukumo mkubwa mno wa Magufuli na Rafiki yake Eng Elius mwakalinga.

3. Mradi wa Hospitali ya Kyela jengo la Ghorofa kwamba ulianza wakati wa kikwete ni UWONGO ulio kubuhu. Mimi ninachofahamu labda aliidhinisha magufuli sijui ila Mama samia ameanza na msingi.

4. Umeandika Mengi mno ya Uongo mtupu yaani kwakifupi huu uzi ni wauongo ndio hayo nimeeleza pale juu kuwa ni Siasa ngumu za kinyakyusa niishie kwa kupinga moja ulilolidanganya kwamba ati kinanasi hakuzungumzia malipo ya stamiko. Kiananasi aliongelea kero mbili tuu mbele ya Rais la kwanza malipo ya Mafao ya Stamiko na mfumo wa mauzo ya kokoa.

huu uzi umekaa kimbea mbea sana inatakiwa upelekwe mataga kwa wachambaji. Uzi wa uongo uongo tuu.

Mwisho:

Kinanasi anakuja vizuri japo speed yake ni ya kawaida. Kwa wanakyela ushawishi wake mpaka sasa ni zaidi ya 95% kutokana na kujikita sana vijijini Na kutatua kwa haraka migogoro iliyokuwa sugu kwa wananchi wake, tofauti kabisa na mtangulizi wake.
Nitajie migogoro 2 tu aliyotatua kinanasi vijijini , na Je suala la meli ziwa nyasa na ile mipango ya Matema na Mwaya Kinanasi ameiweka wapi kwenye ziara ya Rais ?

Kingine ni mchakato wa Kinanasi kushinda kura za maoni , zile pikipiki alizowagawia makatibu kata alitoa wapi , na wale 18 waliokamatwa na TAKUKURU wakigawa hela usiku wa kuamkia siku ya kura za maoni walishitakiwa mahakama gani ? na Alli Jumbe alikuwa na uwezo ule ? Nani alikuwa nyuma yake ? Hapa ndipo wale wanaosema alibebwa ndio wanapopata nguvu , na je mbona wenyeviti wengine wa ccm wa wilaya nchi nzima walizuiliwa kugombea , wakiwemo MARC na MADC , waliojaribu walivuliwa vyeo akiwemo Makonda , kwanini Kinanasi aliachwa ?
 
Back
Top Bottom