Uozo stendi ya Ubungo

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
1,253
1,028
Hapa nilipo nipo stendi ya basi ya Ubungo,nimepanda basi la Sai baba la kwenda Arusha.
tangu asubuhi wakati nafika nimekutana na wapiga debe wengi ambao wengi wao na kautapeli wanako hivyo hivyo kwa kutowaamini nilinyosha hadi ofisi ya basi tajwa.
Ilikuwa mida ya saa mbili na nusu asubuhi.nikaambiwa saa 3 basi linaanza safari.
maajabu sasa ni saa 4 na dakika 28,hata dalili za basi kuondoka sizioni,2meripoti police,no action has been taken or any information kuwa labda basi bovu na vitu kam. hivyo.
polisi wanajizungusha tu na mavitambi yao.
surely inauma na kukera.
 
Polisi wa leo njaa kali, makampuni ya usafirishaji full kunyanyasa abiria, usalama hakuna na mambo mengi kadha wa kadha.

Kwa kifupi hii 'ndege' yetu imewekwa kwenye autopilot na rubani kauchapa usingizi na kilichobaki ni kujikaza kisabuni hadi 'ndege' itakapotua uwanja wa maamuzi 2015.

Pia tuwe makini ktk kufanya maamuzi yahusuyo mustakabari wa maisha yetu. Pamoja na hayo nawakumbusha tu ya kua bila wananchi hakuna serikali.

Yangu ni hayo tu kwa leo, ila poleni kwa kupata usumbufu wa safari, nawatakieni safari njema.
 
jitahidi kuchagua mabasi ya kupanda, kuna mabasi yana heshima kubwa dar to Arusha
 
Mabasi ya saibaba sio kabisa kwa huduma na hususan kuondoka kituoni. Mnaweza kaa ubungo masaa. Wakati ujao tumia dar express, kilimanjaro au mtei express. Haya yanaondoka kwa wakati. Na ni vizuri ukawa unakata tiketi mapema siku moja kabla inasaidia sana.
 
Hiyo ndiyo Tanganyika, hakuna anayewajibika, kila mtu na kiwazo chake tu cha kupata ugali wa leo! maendeleo tutayasikia tu labda mtume arudi kutuokoa...
 
Back
Top Bottom