Uozo na Ubinafsi Wizara ya Afya

Gamba la Chuma

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,243
340
Ukweli ni kwamba tatizo lililopelekea mgogoro na mgomo wa madaktari ni uongozi mbovu wa Wizara ya afya.

MAT (Chama cha Madaktari) walilenga kuelezea hali ilivyo ikiwamo kucheleweshwa posho za madaktari, Wizara kukata sehemu kubwa ya mafungu (kasma) ya Hospitali, ubinafsi wa Watendaji Wizarani, na matatizo yaliyopo kwa ujumla n.k.

MAT walifanya kila jitihada kuomba kuonana na Uongozi wa Wizara ya Afya ili kuepusha mgomo kwa kupatia ufumbuzi matatizo yaliyopo, lakini si Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu wala Mganga Mkuu aliyekuwa tayari kuwasiliza. MAT walikumbana na kejeli, na dhihaka kutoka kwa Viongozi hao wa Wizara yao.

MAT waliposhindwa madaktari wakaamua kulichukua suala hilo na kuomba kuonana na Uongozi wa Wizara. Hata hivyo hila na fitina ziliendelea na hivyo nao pia hawakufanikiwa.
Madaktari wakaomba kuonana na PM Pinda. Waziri wa afya alipopata habari hiyo akawahi kwa PM na kufanya fitina. Akampotosha PM kuhusu ukweli wa mgogoro ulivyo.
Kutokana na kupotoshwa na Waziri wa Afya, PM akatumia hatua zisizofaa kutatua mgogoro kwa kutoa vitisho kwa madaktari. Pia aliagiza kupelekwa madaktari wa JWTZ kusaidia MNH hali iliyosababisha madaktari bingwa nao kuingia kwenye mgomo.
Maafa yaliyotokea sio madogo, tumewapoteza ndugu zetu wengi kutokana na hujuma, hila, fitina na Uongozi mbovu wa Wizara ya Afya.
Hata hivyo PM Pinda alipata ukweli ulivyo baadaye, baada ya madhara makubwa kutokea. Alipewa ukweli kuhusu hujuma, hila, fitina na upotoshwaji uliofanywa na Waziri wa Afya Mponda.

Alipoongea na madaktari jana (Feb 09, 2012) PM alitumia lugha tofauti na awali. Na pia alionyesha wazi kujua tatizo lilipo na jinsi alivyopotoshwa. Aidha alijulisha kuwa amepata taarifa za uozo uliopo Wizara ya Afya.

PM alichukua hatua ambazo tumejulishwa. Lakini ukweli ni kwamba, hata kama Waziri Mkuu angeamua kutoongeza posho na badala yake kuwawajibisha viongozi hao wabovu wa wizara akiwemo Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu, ni wazi kuwa madaktari wangefurahi, wangeridhika na wangerejea kazini kwa moyo mmoja.

Lakini pia hata kama PM angeamua kuwaongezea posho kwa mara 10 ya kiwango walichohitaji madaktari, na kuwaacha hao viongozi wabovu wizarani, ni wazi kuwa madaktari wangeendelea na mgomo.
Uongozi wa wizara ya afya umesababisha maafa, umelisababishia taifa la Tanzania aibu na fedheha kubwa, na pia umeigharimu serikali na walipa kodi gharama ambazo waliwajibika kuziepusha kwa makuwa wasikivu.
Tuendelee kuishinikiza serikali kuisafisha Wizara muhimu ya afya. Lakini pia serikali isipende kusubiri mpaka maafa yatokee ndipo ichukue hatua.
Wenye nafasi walisimamie hili.
 
Ningewashauri madaktari chama chao -MAT kisiwe chama cha hiari tena,hii itawafanya hata madaktari walio kwenye uongozi kuacha kuwadharau.Kiwe kama bodi ya Wahasibu.Ikibidi kitafute ofisi au jengo tofauti na hapo Wizarani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwa huru kwenye maamuzi yao. Hata ikibidi kufanya mchakato wa kuwa na jengo lao wenyewe kwa kuomba wafadhili au serikali iwajengee,kwa hapo itakuwa imeweza kuondoa kero nyingi za madaktari.
 
Back
Top Bottom