Uongozi wa SAUT wazuru kaburi la Shujaa Magufuli, Prof Mahalu asema JPM alitamani kuiona Afrika inayojitegemea!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Wahadhiri na wafanyakazi wa chuo kikuu cha Mt Augustino Mwanza (SAUT), wametembelea na kuhani msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano nchini, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni kuelekea kumbukizi ya kifo chake huku wakiendelea kukumbuka namna ambavyo aliweza kupiga vita…

Prof. Costa Ricky Mahalu, Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT amesema ''Hayati Dkt. John Magufuli ni kiongozi ambaye alipiga vita sana suala la unyanyasaji, alitamani kuona Afrika inajitegemea kutokana na rasilimali zake lakini bado alikuwa ni mzalendo wa kuchoche watu kupenda kufanya kazi"

Padri Innocent Sanga, Mhadhiri Chuo Kikuu cha SAUT naye amenena haya "Kiongozi mzuri ni yule anayemcha Mungu, Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa ni mtu ambaye alimpenda Mungu, tunakumbuka wakati wa Corona imepamba moto alitusisitiza Watanzania kusimama na Mungu"

Chanzo: Jambo TV
 
Pamoja na madhaifu yake,alikuwa ni moja ya viongozi waliotusaidia kwa asilimia fulani kuutengeneza mfumo wa mtawala na mtawaliwa. Kuna Ile hofu unaona kwa mfanyakazi wa serikali katika utendaji,maana waafrika tumezoea kukalipiwa ndio mambo yaende.
Nyerere,Mkapa na Magu tutaendelea kuwakumbuka daima.
 
Uongozi wa Chuo Kikuu cha SAUT umezuru kaburi la Shujaa Magufuli katika Kumbukizi la miaka miwili ya kifo chake

Makamu Mkuu wa Chuo Prof Mahalu amesema Shujaa Magufuli alitamani kuiona Afrika inayojitegemea kwa Rasimali zake

Source Jambo TV

Huyu huyu Prof Mahalu aliyewahi kuwekwa mahabusu miaka mingi kwa kosa la kukwapua pesa za Tanzania ndiyo rafiki wa Magufuli?

Anyway,mwizi huwa rafiki wa mwizi
 
Huyu huyu aliyetetewa na Rais mstaafu mzee Mkapa mahakamani
 
Pamoja na madhaifu yake,alikuwa ni moja ya viongozi waliotusaidia kwa asilimia fulani kuutengeneza mfumo wa mtawala na mtawaliwa. Kuna Ile hofu unaona kwa mfanyakazi wa serikali katika utendaji,maana waafrika tumezoea kukalipiwa ndio mambo yaende.
Nyerere,Mkapa na Magu tutaendelea kuwakumbuka daima.
Madhaifu ya shujaa niyapi tena. Mbona mnatuchanhanya
 
Pamoja na madhaifu yake,alikuwa ni moja ya viongozi waliotusaidia kwa asilimia fulani kuutengeneza mfumo wa mtawala na mtawaliwa. Kuna Ile hofu unaona kwa mfanyakazi wa serikali katika utendaji,maana waafrika tumezoea kukalipiwa ndio mambo yaende.
Nyerere,Mkapa na Magu tutaendelea kuwakumbuka daima.
Magu hakuwa kiongozi, mwanaizaya, baladhuli na muuaji yule.
 
Uongozi wa Chuo Kikuu cha SAUT umezuru kaburi la Shujaa Magufuli katika Kumbukizi la miaka miwili ya kifo chake

Makamu Mkuu wa Chuo Prof Mahalu amesema Shujaa Magufuli alitamani kuiona Afrika inayojitegemea kwa Rasimali zake

Source Jambo TV
Nisahihi, Aliweza kuishi kwa misingi ya kikatoliki kama ilivyokuwa kwa mwalimu, na ndio huwa tunasema huwezi kuwa mwanamajumui kama huishi au hulijui kanisa
 
Back
Top Bottom