Uongozi wa Rais Magufuli utaacha alama na kukumbukwa kwa ujenzi wa uchumi wa kizalendo na si uzalendo wa uchumi.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Nafarijika kuona kwamba Rais Magufuli anajitahidi sana kufanya uchumi wetu umilikiwe na wazawa. Huu ni mtazamo mzuri kwa kuwa unahakikisha kujenga uchumi wa kizalendo na si uzalendo wa uchumi. Wasio wazawa wana uzalendo wa uchumi kwa maana ya kwamba watakuja kuwekeza na kuondoka wakiangalia faida bila kujali uchumi unakua au laah!, si jukumu lao kukuza uchumi.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema’ uchumi wetu wa leo unakosa utu na usawa na hamjali mzalendo. Katika hali hiyo huwezi kujenga uchumi kwa ajili ya watu. Utajenga uchumi kwa ajili ya wawekezaji- hasa kutoka nje’. Hayo ni maoni ya muasisi wetu ambayo Rais Magufuli anayaishi na kuyafanyia kazi kwa kujenga uchumi ambao unamjali mwekezaji mzawa na sio wawekezaji wa nje. Serikali ya Magufuli kupitia upya mikataba hasa ya madini na kutoa nafasi ya umiliki wa Zaidi ya `50% katika rasilimali za taifa kwa wazawa ni kuhahakia unajengwa uchumi wa kizalendo.

Mwalimu Nyerere alikuwa anapenda kuona wazawa wanapendelewa katika mambo yahusuyo uwekezaji na kutaka kufanya wazawa kuwa wawekezaji wakubwa katika taifa. Kitendo cha wazawa kuwa wawekezaji wakubwa ndio msingi wa kujenga uchumi wa kizalendo ambao Rais Magufuli anaujenga. Mwalimu Nyerere aliichukia kasumba ya kuona watanzania wazawa hawawezi kuwa wawekezaji wakubwa Zaidi ya wazungu.

Katika kuwahakikishia kwamba serikali yake( Rais Magufuli) ina muelekeo mzuri wa kujenga uchumi wa kizalendo kwa kuzalisha wafanyabiashara na wasomi wengi wa biashara, serikali imeyapa kipaumbele kikubwa masomo ya biashara katika mkopo wa elimu ya juu. Nimetafakari sana maana ya jambo hilo nikaona kwamba matokeo ya kitendo ni miaka 10 ijayo na Rais Magufuli atakumbukwa kwa hilo.

Kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua biashara kwangu mimi naona kama njia ya kuzalisha wataalamu wengi katika Nyanja ya uwekezaji, ujasiriamali na uchumi ambao kwa sasa ni kama kuna upungufu mkubwa. Pia, ninaona ni njia ya kuhamasisha wanafunzi wachangamkie masomo ya biashara ili waweze kutumia elimu yao katika kutafuta fursa za biashara na uwekezaji.

Linalohitajika kwa sasa Tanzania ni elimu ya uwekezaji na biashara ambayo watanzania wengi hawana hasa kipindi hiki ambacho ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kimkakati inafanyika. Wataalamu wa biashara watakuwa msaada mkubwa katika kuwasaidia wale wasio na elimu ya kufanya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo. Uwekezaji katika SGR na STIGLER’S GORGE ni fursa nzuri sana kwa watanzania kibiashara.

Kwa wale wanaosema Rais Magufuli anachukia matajiri, je mtaendelea kusema hata baada ya kutaka kukutana nao? Nia ya Rais wetu tangu mwanzo ilikuwa ni nzuri sana kwa matajiri ila ilichukuliwa na kutafsiriwa kisiasa majukwaani. Lengo lilikuwa ni kuwafanya matajiri hasa wazawa wajenge uchumi wa kizalendo na si uzalendo wa uchumi ambao unaangalia faida tu.

Ninaamini katika kutaniko la Rais na Matajiri, watatoa mawazo ya kumsaidia Rais wetu kujenga uchumi wa uzalendo ambao ndio lengo kubwa kiongozi wetu. Ninaamini miaka 10-20 ijayo Tanzania itafika mahali wazawa watachangamkia fursa za kiuwekezaji na za kibiashara, na kufanya uchumi wetu kumilikiwa na wazawa na kazi kubwa anayofanya Rais wetu sasa kuzaa matunda kwa kufanikiwa kuwa na uchumi wa uzalendo. Huu ndio uongozi unaoacha alama na kukumbukwa.
 
Naona mnahangaika sana kusafisha serikali hii baada ya kuona hali halisi mitaani. Mmechelewa sana ngoja tujikusanye ili hata kama ni kuiba kura mwakani mfanye kwa shida kubwa.
 
Wehu sio lazima uvue nguo ,huu wehu unaofanyika awamu hii ndio kujenga uchumi ,kufunga biashara ,kuporoka makusanyo ya kodi ,wawekezaji kuondoka ,mzunguko wa pesa kuporomoka ,kushindwa kuajiri ,kupandisha madaraja ,makampuni na mashirika kufunga shughuli zao ndio kukua uchumi ,na kwenye korosho mmekuza uchumi .
 
Hujui chochote kuhusu Uchumi halafu Mtu unavyoandika pumba ndefu hivi yaani kama vile unapiga story na wajinga wenzio mkichimba choo.
 
Wehu sio lazima uvue nguo ,huu wehu unaofanyika awamu hii ndio kujenga uchumi ,kufunga biashara ,kuporoka makusanyo ya kodi ,wawekezaji kuondoka ,mzunguko wa pesa kuporomoka ,kushindwa kuajiri ,kupandisha madaraja ,makampuni na mashirika kufunga shughuli zao ndio kukua uchumi ,na kwenye korosho mmekuza uchumi .
kampuni linaposhindwa kujiendesha, kufungwa ni lazima na hakuepukiki. wawekezaji wanaoondoka ni kwa sababu ya kushindwa ushindani uliopo na wale wanaoweza kumudu ushindani watabaki kushindana. ajira zipo na zinatangazwa ila sio wote wanaoomba wanapata, ajra ni tatizo la kidunia. makusanyo ya kodi ni takribani trilioni 1.3 kila mwezi, unaposema yameporomoka ni kivipi? makusanyo ya awali kabla ya poromoko yalikuwaje? mzunguko wa pesa haramu ndio umeporomoka
 
mimi ninaujua uchumi matokeo kama haya ya awamu ya tano , huo uchumi makaratasi labda wewe ndio unajua zaidi yangu
 
Naona mnahangaika sana kusafisha serikali hii baada ya kuona hali halisi mitaani. Mmechelewa sana ngoja tujikusanye ili hata kama ni kuiba kura mwakani mfanye kwa shida kubwa.
msijifiche katika chaka la kuibiwa mnaposhindwa na kushindwa kwenu ni dhahiri na hii ndio halisi mtaani. Hali halisi ya mtaani ni uchumi wa viwanda, uchumi wa miundombinu, uchumi wa wajariamali. nyie jikusanyeni tu ila watanzania watampigia kura Magufuli na atashinda
 
Nafarijika kuona kwamba Rais Magufuli anajitahidi sana kufanya uchumi wetu umilikiwe na wazawa. Huu ni mtazamo mzuri kwa kuwa unahakikisha kujenga uchumi wa kizalendo na si uzalendo wa uchumi. Wasio wazawa wana uzalendo wa uchumi kwa maana ya kwamba watakuja kuwekeza na kuondoka wakiangalia faida bila kujali uchumi unakua au laah!, si jukumu lao kukuza uchumi.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema’ uchumi wetu wa leo unakosa utu na usawa na hamjali mzalendo. Katika hali hiyo huwezi kujenga uchumi kwa ajili ya watu. Utajenga uchumi kwa ajili ya wawekezaji- hasa kutoka nje’. Hayo ni maoni ya muasisi wetu ambayo Rais Magufuli anayaishi na kuyafanyia kazi kwa kujenga uchumi ambao unamjali mwekezaji mzawa na sio wawekezaji wa nje. Serikali ya Magufuli kupitia upya mikataba hasa ya madini na kutoa nafasi ya umiliki wa Zaidi ya `50% katika rasilimali za taifa kwa wazawa ni kuhahakia unajengwa uchumi wa kizalendo.

Mwalimu Nyerere alikuwa anapenda kuona wazawa wanapendelewa katika mambo yahusuyo uwekezaji na kutaka kufanya wazawa kuwa wawekezaji wakubwa katika taifa. Kitendo cha wazawa kuwa wawekezaji wakubwa ndio msingi wa kujenga uchumi wa kizalendo ambao Rais Magufuli anaujenga. Mwalimu Nyerere aliichukia kasumba ya kuona watanzania wazawa hawawezi kuwa wawekezaji wakubwa Zaidi ya wazungu.

Katika kuwahakikishia kwamba serikali yake( Rais Magufuli) ina muelekeo mzuri wa kujenga uchumi wa kizalendo kwa kuzalisha wafanyabiashara na wasomi wengi wa biashara, serikali imeyapa kipaumbele kikubwa masomo ya biashara katika mkopo wa elimu ya juu. Nimetafakari sana maana ya jambo hilo nikaona kwamba matokeo ya kitendo ni miaka 10 ijayo na Rais Magufuli atakumbukwa kwa hilo.

Kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua biashara kwangu mimi naona kama njia ya kuzalisha wataalamu wengi katika Nyanja ya uwekezaji, ujasiriamali na uchumi ambao kwa sasa ni kama kuna upungufu mkubwa. Pia, ninaona ni njia ya kuhamasisha wanafunzi wachangamkie masomo ya biashara ili waweze kutumia elimu yao katika kutafuta fursa za biashara na uwekezaji.

Linalohitajika kwa sasa Tanzania ni elimu ya uwekezaji na biashara ambayo watanzania wengi hawana hasa kipindi hiki ambacho ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kimkakati inafanyika. Wataalamu wa biashara watakuwa msaada mkubwa katika kuwasaidia wale wasio na elimu ya kufanya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo. Uwekezaji katika SGR na STIGLER’S GORGE ni fursa nzuri sana kwa watanzania kibiashara.

Kwa wale wanaosema Rais Magufuli anachukia matajiri, je mtaendelea kusema hata baada ya kutaka kukutana nao? Nia ya Rais wetu tangu mwanzo ilikuwa ni nzuri sana kwa matajiri ila ilichukuliwa na kutafsiriwa kisiasa majukwaani. Lengo lilikuwa ni kuwafanya matajiri hasa wazawa wajenge uchumi wa kizalendo na si uzalendo wa uchumi ambao unaangalia faida tu.

Ninaamini katika kutaniko la Rais na Matajiri, watatoa mawazo ya kumsaidia Rais wetu kujenga uchumi wa uzalendo ambao ndio lengo kubwa kiongozi wetu. Ninaamini miaka 10-20 ijayo Tanzania itafika mahali wazawa watachangamkia fursa za kiuwekezaji na za kibiashara, na kufanya uchumi wetu kumilikiwa na wazawa na kazi kubwa anayofanya Rais wetu sasa kuzaa matunda kwa kufanikiwa kuwa na uchumi wa uzalendo. Huu ndio uongozi unaoacha alama na kukumbukwa.
Tutolee upumbavu wako hapa..
 
msijifiche katika chaka la kuibiwa mnaposhindwa na kushindwa kwenu ni dhahiri na hii ndio halisi mtaani. Hali halisi ya mtaani ni uchumi wa viwanda, uchumi wa miundombinu, uchumi wa wajariamali. nyie jikusanyeni tu ila watanzania watampigia kura Magufuli na atashinda

Mimi ni kati ya watu wasipenda kutoa/kupokea rushwa; ila kama Jamii Forums wangekuwa wanashawishika hata kwa kahela ka mboga tu, ningewahonga ili wewe Karlo Mwilapwa na ndugu yako Elitwege mfungiwe milele na msionekane kabisa humu jf!

Mada zenu siku zote zimekua ni za kuleta maudhi maudhi tu!
 
Yaani ukisomaga Watanzania wengine utafikiri tulikuwa na uchumi mzuri wakati wa Nyerere kumbe Nyerere alishidwa uchumi mpaka akangatuka na kutuacha na ugali wa yanga😲. Angalieni video za Mwingi muone anavyosema nchi ilikuwa 1984. Hivyo acheni kabisa kumuongelea Nyerere kwenye uchumi maana si ukweli ni bora mnge mwongelea Mwinyi
 
Mimi ni kati ya watu wasipenda kutoa/kupokea rushwa; ila kama Jamii Forums wangekuwa wanashawishika hata kwa kahela ka mboga tu, ningewahonga ili wewe Karlo Mwilapwa na ndugu yako Elitwege mfungiwe milele na msionekane kabisa humu jf!

Mada zenu siku zote zimekua ni za kuleta maudhi maudhi tu!
huo unaitwa mchanga wa machoni, huoni mbele unaishia kupapasa tu
 
Back
Top Bottom