Uongozi wa Nchi Yetu na Karata ya Udini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa Nchi Yetu na Karata ya Udini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LordJustice1, Apr 21, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tangu JK aliambie taifa kwamba eti kuna "udini" baada ya kushindwa kwa kishindo katika uchanguzi mkuu wa Oktoba, 2010, bado haijafahamika hasa alimaanisha nini kuhusu hilo!

  Bahati mbaya sana JK ameacha hoja hiyo hewani bila kuitolea ufafanuzi mpaka ikadakwa na baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wakidai kwamba eti JK anapigwa vita "kwa sababu ya Uislamu wake!" Kuna walioenda mbali kwa kudai eti kwamba kila anapoingia Rais Mwislamu anapigwa vita "kwa sababu ya uislamu wake!"

  Inawezekana kabisa JK alikuwa na hoja, lakini kwa sababu ya woga na udhaifu wake alishindwa kuifafanua hadi sasa inaonekana kwamba badala ya kupambana na aliouita udini amejikuta anausambaza bila kujijua kwa maana kwamba ameacha Vituo vya Redio vya Kiislamu na baadhi ya magazeti kuendeleza ngoma ya "JK kuonewa kwa sababu ya uislamu wake!"


  Aidha, JK angeenda mbali kidogo kwa kueleza kwamba UDINI ni nini na una sura na tabia gani!

  Najua watu wengi hawakupendezewa pake JK alipoingiza mambo ya Mahakama za Kadhi kwenye Ilani ya Uchaguzi, 2005, kwa kudai kwamba alikuwa anavunja Ibara ya 19 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inayosema kwamba "Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi."

  Baadhi ya Waislamu wanaamini kimakosa kwamba wasio Waislamu hawapendi maendeleo ya Waislamu kwa kuwazuia wao kuwa na Mahakama zitakazoshughulikia mambo ya Waislamu tu! Cha ajabu wanataka Serikali isiyokuwa ya Waislamu iwaundie na kugharamia chombo hicho huku wakijua kwamba Mambo ya Kadhi ni Ibada Kamili ya Waislamu!


  Jambo jingine linalofanana na hilo ni OIC!

  Masuala yote mawili huwa yanajitokeza kila anapoingia Rais Mwislamu kwa ajili ya kutetea maslahi ya Waislamu! Rejea suala la OIC lilipoingia mwaka 1993 kwa Zanzibar kujiunga kinyemela na baadaye kujitoa kwenye OIC! Tunaambiwa kwamba Rais Mwinyi alitaka hata kuiingiza Tanzania yote kwenye OIC bila hata Bunge kuwa na taarifa!

  Nayazungumzia yote haya mawili (OIC na Mahakama za Kadhi) kwa sababu ndio hasa mzizi mmojawapo wa udini ulipo!


  Marais Waislamu walipoingia Ikulu (1985 - 1995, 1995 - 2005) walikuwa na "Islamic Agenda" vichwani mwao! Mwinyi hakuionesha hiyo agenda hadi alipokamata madaraka kwa awamu ya pili, lakini Kikwete aliipachika agenda hiyo kwenye Ilani ya Uchaguzi, 200 -2010 lakini baadaye alii-disown na kudai kwamba eti ilipachikwa na Kingunge na Mkapa! Hili suala la ku-disown mambo sio geni kwa Kikwete maana alituhakikishia Watanzania kuwa haijui kabisa DOWANS ambayo mawaziri wake wanaipigia debe kila uchao hadi kutaka kubadili Sheria ya Manunuzi, 2004, Na. 21/2004 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo chakavu ya DOWANS! Hizo "Islamic Agenda" huwa wanatumwa na Wanadini wenyewe na pindi wanapoona kwamba zinakataliwa hukimbilia kudai kwamba eti "kuna udini!"

  Kama JK anajidai kuwa na macho makali ya kuuona "udini" ambao watu wengi hawauoni, angekuwa wa kwanza kutangaza "vita dhidi ya udini" pale Viongozi wa dini ya Kikristo walipomwita yeye kuwa eti ni "Chaguo la Mungu!" Hapo tungemwona kweli Kikwete anakerwa sana na "udini!"

  UDINI NI NINI BASI?
  Kwa mazingira ya kwetu kwa sasa udini ni gamba ambalo baadhi ya Viongozi huvaa wanapoona support waliyonayo inazidi kupotea! Kikwete ni Rais dhaifu sana katika Historia ya Marais wa Nchi yetu! Hana vision zaidi ya kupanga namna ya kuendeleza ubabe wa CCM wa kubaki Ikulu kwa hila! Kwa sasa hatuoni anazungumza lolote kuhusu ahadi alizotoa kwa Watanzania bali kujivua "magamba" ili CCM iendelee kubaki madarakani 2015, only that! Mtu yeyote, esp asiyekuwa Mwislamu, anayezungumzia madhaifu ya Kikwete anaonekana kwamba ni mdini!
  Laiti kama Wakristo wangedai kwamba Mkapa kuitwa FISADI ni "udini" sijui mambo yangekuwaje! Hivyo na Edward Lowasa naye ingedaiwa kwamba kujiuzulu kwake ni kwa sababu ya "udini," tungekuwa tunazungumzia mengine kwa sasa!Kilicho dhahiri ni kwamba kwa Waislamu "mtu wao" ni safi siku zote as long as ataendelea kuwa Mwislamu, whether ni fisadi or otherwise!


  "GAMBA LA UDINI" NI HATARI KULIKO MAGAMBA YOTE!
  Wakuu sina haja ya kuelezea kwamba umoja wa nchi yetu kwa sasa unazidi kudhoofika sana kwa sababu kadhaa:
  a. Gamba la udini,
  b. Gamba jembamba la ukabila,
  c. Tofauti kubwa sana kati ya walio nacho na wasio nacho!

  Lakini mtakubaliana na mimi kuwa mawili ya kwanza ni hatari zaidi kwa umoja wa nchi yoyote na yanastahili kupigwa vita kwa gharama yoyote na si kwa unafiki kama anavyofanya Rais wetu Kikwete kwa kuutaja udini pale tu mambo yanapoharibika na yanapokunyookea unakuwa kimya!
  Vyombo vya habari vya kidini viangaliwe upya, bila kuingilia sana uhuru wa vyombo vya habari na si kuachwa kama ilivyo sasa!


  Otherwise, future ya nchi yetu iko hatarini kuliko tunavyofikiri, maana mambo ya Somalia na Nigeria yanainyemelea nchi yetu kwa sasa!
   
 2. MLAU

  MLAU JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2017
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 4,481
  Likes Received: 3,062
  Trophy Points: 280
  Udini
   
 3. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2017
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
 4. Victor wa happy

  Victor wa happy JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2017
  Joined: Apr 24, 2013
  Messages: 8,680
  Likes Received: 5,683
  Trophy Points: 280
  Kikwete mwenyewe ni mdini

  Angalia alivyosovu mgogoro wa kuchinja ni wazi aliegemea upande mmoja

  Angalia uhasama uliozuka wa waislam na wakristo wakat wake

  Viongozi wa afrika wanchohubiri ni tofauti na wanachokifanya

  mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
   
 5. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 6,716
  Likes Received: 6,155
  Trophy Points: 280
  Acha porojo, wewe mleta Uzi.

  Hakuna cha udini wala ufuasi hapo Tanzania.

  Dini zenyewe ni hizo dini uchwara za wazungu koko na warabu pori au unazungumzia dini zipi!?

  Maana, wenye hizo dini ndiyo mafisadi, walevi, wala rushwa na kila aina ya uchafu sasa unazungumzia dini feki hizo!?

  Kwa kifupi, huo upupu wa kuwa dini zinagawa Taifa ni upuuzi na porojo zinazotakiwa kupingwa kwa nguvu zote na kuondolewa ujinga huo mionngoni mwa wananchi.

  Utakuta mtu ana mikufu mirefu ya swala za warabu pori mikononi na wengine mikufu ya maombi shingoni ya wazungu koko ila ni mchafu kupindukia.

  Wazungu koko, wenyewe dini wameisha ziacha kila mtu anapiga kazi tu.

  Tuacheni, ujinga wa dini za wazungu koko na warabu pori tujenge nchi yetu.
   
 6. sergio 5

  sergio 5 JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2017
  Joined: May 22, 2017
  Messages: 8,885
  Likes Received: 9,160
  Trophy Points: 280
  Wanchohubiri hili neno umelitoa wap?
   
Loading...