Uongozi wa CHADEMA Ukerewe wahamia CCM jioni hii

Vipi hili la madiwani wa Chadema ubungo kukamatwa na Takukuru kwa rushwa.

Rushwa ni jinai haina chama. Kamata yoyote ila kama wengine wanaachwa tunaona ni muendelezo wa siasa chafu za awamu hii ya tano. Mfano Ngeleja lakini tunamuona anadunda tu.
 
Saa ikifika hata TL m'bwatukaji atahama tu.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwa nini watu wanahama Chadema kwenda ccm sehemu zile zenye umasikini na kiwango cha juu cha ujinga? Mbona hayo hayatokei mijini na kule kwenye maendeleo?

ccm wanahaha tu ,hela kama zipo wakajenge hospitali na vifaa vya St scan kila hospitali ya wilaya ili wananchi wasiendelee kufa kwa magonjwa ambayo yanatibika badala ya kuendeha siasa mflisi
 
Mwenyekiti wa Wilaya ya Ukerewe, Katibu wa Wilaya, wenyeviti watano (5) wa Serikali za mitaa wakisindikizwa na wanachama 200 wa CHADEMA wilayani Ukerewe wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi muda huu.

Katibu mwenezi Wilaya ya Ukerewe {CHADEMA} Ndg Magambo akizungumza kwa niaba ya viongozi hao waliohama, amesema kuwa "kwa biashara aliyoifanya Mbowe na Lowasa ya kuuza Chama hicho, mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kubaki Chadema, wanaobaki Chadema hawajitambui na kwamba muda si mrefu watajitambua tu"

Ameendelea kusema "sisi wakerewe tuna akili sana, tumeshagundua hawa jamaa (CHADEMA) ni matapeli wakubwa sana"

kumekuwepo na wimbi kubwa la Viongozi wa Chadema kukihama chama hiko kwa kasi kubwa kia uchao, tunawatakia kila la heri wazalendo wote wanaoendelea kujiunga na CCM na kuukataa UFISADI na FISADI aliyeinunua CHADEMA.
Kwa kuwa mchezo huu ni wa kutengenezwa believe me mwisho wake utawashanhaza wengi sana. Kwa njaa na ukata wa sasa MTU anapewa 70m anaziachaje? swali ni je umeununia moyo na utashi wake? kesho akiamua kukukana c utajinyonga? picha natamani niione mpaka mwisho. nione inaishaje....
 
Saa ikifika hata TL m'bwatukaji atahama tu.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
Sio tundu lisu tu lowasa na sumaye wako njiani kurudi CCM mark my words Chadema anzeni kujiandaa kisaikolojia msije ruka kichaa au kupata presha
 
Acha MAKINIKIA yaondoke fuata upepo hao

Sent from my ALE-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Hii sishangai kwasababu Kuna jambo kubwa linaendelea huku mitaani na vijijini. Yaani kuna hela za mikopo zinataka kutolewa sijui ndo zile za ahadi ya milioni 50 au vp hapo sina uhakika. Yani hizo hela zitakopeshwa kuanzia Laki mbili hadi tano, na maejesho yake kidogo kidogo ndani ya miaka 5. Sasa mie mkopo huu umeniacha hoi ktk masharti yake ni ya kibaguzi sanna. Yani ili Uwe na sifa ya kupata huo mkopo, moja ya sifa lazima uwe na kadi ya CCM. Kwamba kama hauna kadi hupati. Ali hiyo kumeamka taharuki kubwa kitaa watu wanatafuta kadi za CCM kwa nguvu kubwa. Na baadhi washaufanya mradi, wanaziuza hadi TSH 10 kila moja. Lkn yote haya yanaendelea huyo DK mashinji sijui yupo kimyaaaaaa km hayupo vile.
Hilo LA hela lipo mitaani wanatoa kwanachama kama mikopo
 
Ccm wanacheza mpira wenyewe wanajigunga wenyewe na wanashangilia wenyewe

Sent from my Fero L100 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwa nini watu wanahama Chadema kwenda ccm sehemu zile zenye umasikini na kiwango cha juu cha ujinga? Mbona hayo hayatokei mijini na kule kwenye maendeleo?
Uwe unafanya utafiti kabla ya kuongea! Wilaya ya ukerewe inaongoza Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya professors!

How dare u unasema hili ni eneo lenye umaskini wa kiwango cha juu cha ujinga!?

A person who says something is impossible should not interrupt the person who is doing it.
 
kaka inaitwa kura kwa huyu kula kwa yule
ili ujue aina ya chama unachodhani kinasimamia sheria na maadili andalia bunge lililowasamaka akina ngereja na kujiuzuru kwa Escrow ,leo mtu na akili zake anakuja na agenda kwenye taifa na chama kilichompa dhamana na kumuahisha uwaziri eti natubu nitarudisha hela zote.HII NDIO CCM
 
Hakuna chama kinachokufa kwa makada kuhama....chama kinakufa kwa viongozi wa juu wenyenguvu sawa kufarakana na wanachama kugawanyika...wapinzani hawaibuki kwa kupendezwa na rangi nzuri za bendera ya chama wala maneno matamu ya viongozi wa chama hicho wala kuwekewa hela mfukoni...wapinzani wanaibuliwa na mfumo
kandamizi, uonevu na kutotendewa haki kama
wengine....binadamu akikosa uhuru hata
mletee tani za dhahabu zilizo jaa lory atageuka mnyama na atakupinga bila kupepesa macho.
 
Hii sishangai kwasababu Kuna jambo kubwa linaendelea huku mitaani na vijijini. Yaani kuna hela za mikopo zinataka kutolewa sijui ndo zile za ahadi ya milioni 50 au vp hapo sina uhakika. Yani hizo hela zitakopeshwa kuanzia Laki mbili hadi tano, na maejesho yake kidogo kidogo ndani ya miaka 5. Sasa mie mkopo huu umeniacha hoi ktk masharti yake ni ya kibaguzi sanna. Yani ili Uwe na sifa ya kupata huo mkopo, moja ya sifa lazima uwe na kadi ya CCM. Kwamba kama hauna kadi hupati. Ali hiyo kumeamka taharuki kubwa kitaa watu wanatafuta kadi za CCM kwa nguvu kubwa. Na baadhi washaufanya mradi, wanaziuza hadi TSH 10 kila moja. Lkn yote haya yanaendelea huyo DK mashinji sijui yupo kimyaaaaaa km hayupo vile.

Mkuu hata mimi huu mchezo mchafu nimeuona wala sio kuhadithiwa. Unapewa huo mkopo ukiwa mwanaccm tu. Na nijuavyo ccm haina hela ya kugawa kirahisi hivyo hiyo lazima ni hela ya umma inafanyiwa ubaguzi wa wazi.
 
Back
Top Bottom