Uongozi wa CCM umeelemea upande mmoja

Samia alipaswa kuzingatia usawa wakati wa uundaji baraza la Mawaziri.Tanzania ina mikoa 27 - 30.

Ni haki Mkoa mmoja kutoa Mawaziri 5 huku mikoa mingine ikiambulia patupu.

Ushauri alipewa Late Mkapa Mama alitakiwa kufanya rejea na si vinginevyo.

Sasa kuna hili suala la uongozi wa kitaifa CCM wote ni swala tano.
Mzee hebu jaribu kufikiri hata kidogo. Mkoa kama Mbeya utampatia nani Uwaziri? Mkoa kama Mtwara nani atafaa japo unaibu?!
 
Wakati B W Mkapa anataka kuunda Baraza la Mawaziri alimfuata Mwl Nyerere na kumuuomba ushauri wa kumsaidia kuunda Baraza la Mawaziri.

Mwl Nyerere alimkatalia Late Mkapa kuunda Baraza la Mawaziri.Mwl alimwambia Mkapa Niki kusaidia maana yake hilo baraza litakuwa langu.

Mwl Nyerere alimsaidia Mkapa namna bora ya kuunda Baraza la Mawaziri.

Mosi lazima Baraza lizingatie maeneo mbali mbali ya Nchi.Kwa maana ni muhimu kutazama mikoa yote kuepuka Mawaziri kutoka sehemu moja na kuyaacha maeneo mengine ya nchi.Lazima baraza liwe na sura ya kitaifa.Leo hii Mkoa wa Pwani na Tanga wana Mawaziri 8.

Mwl Nyerere pia alimtaka Mzee Mkapa kuzingatia dini mbili kuu.

Chama mapinduzi kimemteua Lt Col Kinana kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.Tukitazama safu za uongozi wa juu (Taifa) Mwenyekiti,Makamu wa Mwenyekiti Bara na Visiwani wote ni swala tano hakuna Mgalatia!.

Jambo hili limetokea kwa bahati mbaya au chama kimeamua kupuuza ushauri wa Mwl Nyerere.

Ngongo kwasasa Ukraine 🇺🇦
Acha udini wewe
 
Unequal distribution of Opportunities to eat according to the length of the rope.

Kwahiyo mkuu unataka kusema vikao vikianza wanaambiana saramaleko saramaleko?
 
Back
Top Bottom