Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,654
- 41,309
Uongozi wa awamu ya 5, uligubikwa na kila aina ya uovu, kuanzia kwenye mauaji, utekaji, utesaji, ubambikiaji watu kesi, ugandamizaji wa haki, demokrasia na haki za watu.
Watawala waliostahili kuwalinda raia dhidi ya dhuluma wakageuka kuwa wadhulumaji.
Ben Sanane akapotezwa moja kwa moja baada ya kuhoji uhali wa PhD yake.
Azory Gwanda akapotezwa moja kwa moja baada ya kuandika kuwa kulikuwa na mauaji ya watu wasio na hatia kwenye operesheni za Kibiti.
Tundu Lisu akamiminiwa risasi baada ya kutoa angalizo kuwa ukiukaji wa mkataba na Accacia kutasababisha nchi kushtakiwa, na pia kwa kutamka kuwa tulikuwa na rais wa ajabu.
Kuna taarifa pia kuwa Mo alitekwa baada ya kutaka fidia kutokana na ardhi aliyokuwa anamiliki huko Rufiji ambako sasa kungejengwa bwawa la umeme.
Madiwani kupitia CHADEMA wa Dar na huko Morogoro waliishia kuchanjwa na mapanga kama wanyama wa kitoweo.
Kuhoji utendaji wa Serikali au kumkosoa Rais, hiyo ilikuwa ni death penalty au kutekwa.
Waliotakiwa kuunga mkono juhudi halafu wakakataa, baadhi waliishia kwenye mahabusu kwa muda mrefu, wakitafutiwa makosa ya kubambikwa ili wafungwe.
Chaguzi katika maana halisi zikafutwa. Wagombea wa ubunge kupitia CCM, 75% ya waliopitishwa na wajumbe, majina yao yalikatwa na mtu mmoja, na kupachikwa aliyemtaka. Na hao waliopachikwa, wakapewa ubunge kwa agizo lake kwa wakurugenzi, na ikawa hivyo.
Ukikubali kusifu na kuwa msaidizi kwa uovu ulikula mema ya nchi utakavyo na kuwa huru hata kumpora mtu yeyote uliyetaka.
Kutokana na mtu mmoja, nchi ikafutiwa pesa za misaada, kuanzia zile za MCC mpaka za Jumuia ya Madola. Hizi pesa hazikuwa za.mikopo, na ndiyo zilizotumika kupeleka umeme vijijini kwa karibia 75%.
Mwisho wa yote akajitafutia utajiri kwa kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi matajiri kwa kuwaweka magerezani kwa muda mrefu, halafu mwishoni akawaambia kama wanataka kuwa huru watoe pesa, na watakaokataa wateswe zaidi. Pesa walizozitoa akazifanya zake binafsi na washirika wake, akiamini kuwa hata siku akitoka madarakani awe na utajiri wa kutosha.
LA KUJIFUNZA
Umetesa watu ili upate pesa. Umewaua wasio na hatia, ukiamini pesa ulizozikusanya siku za mbeleni zitakupa nafasi ya kustarehe kwenye utajiri mkubwa. Je, pamoja na uwingi huo wa pesa, aliweza kuzitumia? Aliweza kustarehe? Jibu ni HAPANA.
Tuliobakia, hata kama tuna madaraka, jamani tuchukue kilicho halali yetu, kupora visivyo vyetu, na kuwadhulumu wengine kwa sababu tu ya uchoyo na tamaa ya utajiri, tusidhani kama ndiyo uhakika wa maisha.
Hata pale tunapotafuta mali, hata kama ni kwa njia halali, utajiri na mali visitupofushe akili na mioyo yetu. Tusifanane na yule wa kwenye andiko hili kwenye biblia:
Luka 12: 13 - 21
13 Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14 Yesu akamwambia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mgawanyaji wa urithi wenu?”
15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”
16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18 Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Na nitasema moyoni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20 Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21 Hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”
ANDIKO HILO NI KWAAJILI YA TULIO HAI SIYO KWAAJILI YA MAREHEMU.